Mkuu Waberoya Maneno yako ni makali na hatari mno...Kwa msimamo huo naona unaeneza chuki kuliko kutafuta njia mwafaka ya kutatua Tatizo. Sina sababu yoyote ya kuamini maneno yako kuhusu hiyo redio "kheri",lakini kama huyo Muhubiri ametamka maneno hayo,ni vyema uyachukulie kuwa ni maneno ya huyo muislamu mmoja na sio msimamo wa Waislamu wote.Hapo juu kuna mwanachama mmoja (Msongoru) ametoa mawazo mazuri,Kama kweli umesikia maneno hayo,andika malalamiko yako kwa tume ya mawasiliano.Taja jina la hiyo redio,tarehe na siku ya hayo maneno ya uchochezi...ni wazi kabisa Tume itawasiliana na hao wamiliki wa hiyo redio,na hatua za kisheria zitachukulia pale inapobidi!!!!!
Tujitahidi kuepuka malumbano yanayobeza na kutukana Imani za wengine...vinginevyo tutakuwa tunachochea moto ambao utasababisha mapigano na umwagaji wa damu.....Tuwe kitu kimoja kwa Utanzania wetu bila kujali Makabila, Imani za Dini,Itikadi za vyama au rangi ya Ngozi.
Mkuu Waberoya nikiwa kama Muislamu nachukulia kauli yako kwa uzito wake...ingekuwa vyema kama ungepunguza Jazba na kuomba radhi...SIO KWELI, narudia tena kuwa SIO KWELI kwamba Waislamu ni watu wa vurugu kama unavyotaka tuamini.Nipo wazi kukosolewa!!
Hivi wale wahubiri wa Biblia Ni Jibu, wapo wapi siku hizi...? Maana nao Mmmh!
Hivi yule shehe Dogo yuko wapi siku hizi? maana nae yule kwa zuga hajamboHivi wale wahubiri wa Biblia Ni Jibu, wapo wapi siku hizi...? Maana nao Mmmh!
Hivi yule shehe Dogo yuko wapi siku hizi? maana nae yule kwa zuga hajambo
Fundi Mchundo,Mwawado,Waberoya,Magobe T,X-Paster,
..nakubaliana na mawazo ya wachangiaji kwamba hizo kauli za kichochezi haziwakilishi msimamo wa majority ya Wakristo/Waislamu.
..nakubaliana nao kwamba hatuna budi kuhukumu WAISLAMU/WAKRISTO woote kutokana na kauli ya MCHOCHEZI MMOJA.
..lakini nadhani tuna wajibu wa kuonya kwamba tukiendelea kuwapa nafasi hawa wachochezi, kuna hatari kwamba mbele ya safari watakuja kusomba wafuasi wengi.
..tunapaswa kuuhami UMOJA WETU WA TANZANIA kutokana na mahubiri ya chuki na uchochezi bila kujali yanatolewa na wachochezi wa imani gani.
..hizo redio zilazimishwe kupinga na kukanusha kauli za kichochezi zilizotolewa. vilevile wahusika wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria zetu.
Maneno yako mazuri Fundi Mchundo..., thanx kwa kuliona hilo. Ila tambua kuwa watu wengi huwa hawaangalii kilicho wadondosha... Wanacho angalia wapi wameangukia. Na hili ndo tatizo la watu wengi sana.
Suwala likija kwa jina au anuani ya Uislam, utasoma mambo mengi na hata matusi kisa mwandishi au mzungumzaji ana jina lenye asili ya kiarabu au Kiyahudi. Utasoma au kusikia WAISLAM haoo...Inferiority complex.... na maneno kadha wa kadha.
Kwenye jukwaa la dini mambo yalianza kidogo kidogo...! Wapendwa walipoona wanazidiwa kwa hoja wakaja na style mpya ya matusi. Na hii ni mojawapo ya mbinu zinazotumiwa sana kwenye mijadala ya kwenye internet ili kupoteza mwelekeo wa mada husika. Na ukikosea tu ukajibu kwa asira lawama zote zitakushukia wewe uliye jibu yale matusi kuwa ndo ulioanza. (Na hilo ndio lengo lao).
Na huko mitaani tunayaona haya sana. Wakristo wanajuwa kuwa waislam hawawezi kumtukana Nabii Yesu, mama yake au mtume yoyote aliye tajwa kwenye mkusanyiko wa vitabu vya Biblia. Na wanalijuwa hilo ndo maana wao wanajiona kuwa wana bahati kubwa sana ya kuwatukana Waislam na imani yao. Sasa ikitokea mtu mmoja kausema vibaya Ukristo lawama zinawaendea waislam wote duniani.
Soma jinsi vile ninavyo jibishana nao hawa wapendwa kule kwenye jukwaa la dini kisha kuwa mkweli na nafsi yako na mbele ya yule unaye amini kuwa ndo mungu wako. Kisha utajuwa nina maanisha nini.
Insha'Allah M'Mungu akuongoze.
Matatizo ni kuwa sisi ambao tuko dini moja na hao wachochezi ( awe mkristu, muislamu, baniani n.k) tunachelea sana kuwakana kuwa hawatuwakilishi.
Mimi ningekuamini zaidi kama huko kwenye jukwaa la dini ungekuwa unawakemea waislamu wenzako wachache wanaotoa lugha ya matusi dhidi ya wakristu. Kuwashupalia wapuuzi wakikristu wakati unawaonea aibu wapuuzi wa dini yako hakutatupeleka mbali. Tunatakiwa WOTE kama jamii kukemea na kuvikana vitendo hivyo badala ya kujificha nyuma ya kivuli kuwa ni wachache tu wenye mawazo kama hayo. Tutajuaje kama wote mko kimya wakati wanayasema.
JokaKuu yuko sawa kabisa. Panatakiwa kuwa na zero tolerance vitendo kama hivi vinapotokea. Si kwa dini tuu. Uchochezi wa aina yoyote ( kikabila, rangi, jinsia, ulemavu n.k.) usipewe nafasi katika jamii yetu.

Duu hii kazi kweli kweli... Just thinking aroud: Sijui ni lini tutaacha unafiki...?
Mkuu upo? Kwanza nilidhani kuna vijana pale Karikaoo (wanposubiria magari ya kwenda Temeke/Mtongani/Mbagala) wanaoanzisha mjadala wakidai wakristo kama wapo waeleze maana ya vifungu wanavyowasomea: mafano imeandikwa wapi kuwa Yesu alisema alikuwa Mungu, Yesu hakuanzisha Ukristo ila Paulo, Yesu hakusali kwenye kanisa ila msikiti na imeandikwa kwenye Biblia, etc.
Leo asubuhi nilikuwa mitaa ya ndani ya Kariakoo karibu na Congo Street na huko nikakuta mabishano makubwa yakiambatana na matusi - "Ndiyo maana mimi nawaita Wakristo wote makafiri. Maana unawaelekeza waamini dini ya kweli hawakuelewi.
Na mimi nitaendelea kuwaambia tu kuwa Ukristo siyo dini, dini ni Uislamu..." Yaani ukisikiliza hata unaanza kupata hasira kwa kashfa zinazotolewa na hao jamaa. Sijui wametumwa? Maana, hawakuachii ueleze kitu bali wao wakueleze na hivyo mwisho inaishia kuwa kelele na kutukanwa.
Naona inabidi wakuu wa dini na serikali walikee hili. Baadaye litakuja kuleta mtafaruku. Maana kila kitu kibaya kinaanza kidogokidogo na kisipokemea kinaongezeka na kuwa kibaya zaidi na hatimaye kuanza uharibifu.
Nipo mkuu, Well said. Tusipoangalia hii mihadhara ya kipuuzi itatupeleka pabaya. Watu huwa wanafika mahala wanachoka uvumilivu.
Nimeishi katika moja ya nchi za asean (singapore). Kuna waislamu (maleys) wahindu, wabudha washinto wakristo nk (other races). Hawa jamaa wana amani sana, na kuna religious harmony kubwa mno. Hii inatokana na serikali kuwa na msimamo na kuwa wakali katika issues za dini. Upuuzi kama huo hapo hauna nafasi hata chembe mkuu. Samahani kwa kuuita upuuzi, maana ndivyo navyouona...
Wakubwa nataka kusema kitu mara moja. Nimesoma malalamiko ya Ubungo. Kusema kweli kitu kimoja watu wafahamu kwamba kuna tofauti kati ya UISLAM na MUISLAM. Muislam ni mtu, na mtu anaweza kusema chochote kilicho kwenye mind yake. Na uislam ni dini ambayo ina guide peace and harmony. Ni deen ambayo inataka muislam aangalie jirani zake, ni deen ambayo iliingia mkataba na Jews in Maddinah kuhusu kupigania madinna pindi itakapoingiliwa na watu wa nchi nyingine kwani ni nchi huru.
Sasa one thing nitawaambia ambayo hata mimi nilikuwa victim Tanzania watu wache wana knowledge ya deen. Majority ni wafuata Imam kasema nini. Something which Islam doesn't entertain.
So, sababu mtu mmoja kasema something against other religion, that doesn't make every muslim to be out of touch. Ni sawa na kusema Evangelical christians wote wanahubiri hate crime sababu Pastor John Hagee amesema "those who live by the Qur'an have a scriptural mandate to kill Christians and Jewse".
Inconclusion, i think watu wanachanga frustration zao za maisha na deen. Those are two different things,
Wasalam Aleikum.