Wakubwa nataka kusema kitu mara moja. Nimesoma malalamiko ya Ubungo. Kusema kweli kitu kimoja watu wafahamu kwamba kuna tofauti kati ya UISLAM na MUISLAM. Muislam ni mtu, na mtu anaweza kusema chochote kilicho kwenye mind yake. Na uislam ni dini ambayo ina guide peace and harmony. Ni deen ambayo inataka muislam aangalie jirani zake, ni deen ambayo iliingia mkataba na Jews in Maddinah kuhusu kupigania madinna pindi itakapoingiliwa na watu wa nchi nyingine kwani ni nchi huru.
Sasa one thing nitawaambia ambayo hata mimi nilikuwa victim Tanzania watu wache wana knowledge ya deen. Majority ni wafuata Imam kasema nini. Something which Islam doesn't entertain.
So, sababu mtu mmoja kasema something against other religion, that doesn't make every muslim to be out of touch. Ni sawa na kusema Evangelical christians wote wanahubiri hate crime sababu Pastor John Hagee amesema "those who live by the Qur'an have a scriptural mandate to kill Christians and Jewse".
Inconclusion, i think watu wanachanga frustration zao za maisha na deen. Those are two different things,
Wasalam Aleikum.
Mkuu, usituchanganye! Wasingekuwapo Waislamu usingekuwapo Uislamu pia. Watu ndio wanaounda dini, dini haiundi watu. Kwa hiyo, hao tunaowasema ni Waslamu (wakorofi) kwani Waislamu wastaarabu wapo na tunawafahamu. Kwani tungesema Waislamu fulani ni wastaarabu napo ungesema tutofautishe dini na mtu?
Ikiwa Wakristo nao watafanya upuuzi tutasema pia kwani sisi tunataka tuishi pamoja kwa amani na kila mtu awe na uhuru wa kuabudu kupitia dini anayoiamini.
Hao vijana wanaokashifu Ukristo niliwaambia ni wajinga kupindukia kwani "hamwezi kuacha kuhubiri mambo yanayofundishwa na dini yenu na kuanza kuhubiri kuhusu dini nyingine isiyowahusu. Hata mmeacha kusoma Qur'an yenu na kubakia kutafuta mistari kwenye Biblia mnayofikiri mkiwaambia Wakristo waisome halafu muwazomee mnajiona mmefanya kitu cha heri. Huo ni upuuzi mtupu na mnapoteza muda bure," nilisema Jumapili mitaa ya Kariakoo nilipiwakuta hao vijana wanawashambulia Wakristo kwa kuwatusi.