No control over Religious radio stations over hate speeches

Mkuu Waberoya Maneno yako ni makali na hatari mno...Kwa msimamo huo naona unaeneza chuki kuliko kutafuta njia mwafaka ya kutatua Tatizo. Sina sababu yoyote ya kuamini maneno yako kuhusu hiyo redio "kheri",lakini kama huyo Muhubiri ametamka maneno hayo,ni vyema uyachukulie kuwa ni maneno ya huyo muislamu mmoja na sio msimamo wa Waislamu wote.Hapo juu kuna mwanachama mmoja (Msongoru) ametoa mawazo mazuri,Kama kweli umesikia maneno hayo,andika malalamiko yako kwa tume ya mawasiliano.Taja jina la hiyo redio,tarehe na siku ya hayo maneno ya uchochezi...ni wazi kabisa Tume itawasiliana na hao wamiliki wa hiyo redio,na hatua za kisheria zitachukulia pale inapobidi!!!!!

Tujitahidi kuepuka malumbano yanayobeza na kutukana Imani za wengine...vinginevyo tutakuwa tunachochea moto ambao utasababisha mapigano na umwagaji wa damu.....Tuwe kitu kimoja kwa Utanzania wetu bila kujali Makabila, Imani za Dini,Itikadi za vyama au rangi ya Ngozi.

Mkuu Waberoya nikiwa kama Muislamu nachukulia kauli yako kwa uzito wake...ingekuwa vyema kama ungepunguza Jazba na kuomba radhi...SIO KWELI, narudia tena kuwa SIO KWELI kwamba Waislamu ni watu wa vurugu kama unavyotaka tuamini.Nipo wazi kukosolewa!!

wewe ni mmoja kati ya 1000!, na kweli sina maana wote! sorry for ay problem I might have caused so far!, vipi maoni yako kuhusu hii Redio inayoeneza chuki?

waberoya
 
Hivi wale wahubiri wa Biblia Ni Jibu, wapo wapi siku hizi...? Maana nao Mmmh!

Asante! In fact, mimi nakerwa sana na wahubiri wote (Wakristo na Waislamu au hata dini nyingine) wanaoenda nje ya mahubiri yao na kuanza kuwashambulia wengine. That's offpoint! Na haya siyo mahubiri ila 'prejudice' na 'value judgement' ya mtu.

When you are preaching you are conveying God's message to your audience or congregation and this is different from trampling on other people's belief systems. God's message is about love, conversion (moral, social, political, cultural, pyschological, etc), compassion, forgiveness, reconciliation, reciprocal, dialogue, peace, solidairty, justice (fairness, honesty, etc)...

Every religion has imperfections because religions are human institutions and human institutions are limited - they need purification. So, there is no reason to magnify the imperfections found in other people's religions or belief systems to the extent of forgetting one's own religion and imperfections.
 
Hivi sasa kuna move nzuri inaendelea hapa tanzania Labda wengine hamjaipata au bado hamjaona kama maendeleo ya kukua kuvumiliana...

Kumekuwa na Mihadhara ya Kidini ikifanyika kitaalam na Bila Vurugu hapa ktk Ukumbi wa DIAMOND, hadi sasa imefanyika 2. kwa waliopo DSM wazitafute kwa wauza kanda. Pia Wahubiri Wakistro wamekuwa wakipewa Nafasi ya Kuhubiri Iman yao ktk REDIO KHERI, Sina Hakika kama Wahubiri wa Kiislam nao wamekuwa wakipewa Nafasi...ila Redio WAPO imekuwa ikiitangaza Mihadhara hii...
 
Moderator turuhusu tukalumbane haya kule kwenye jukwaa la dini. Hapa si pake maana hapatatosha kwa hasira za wanadini fulani...... wao siku zote usiseme dini yao hata kama inafanya uovu. Screen zetu zinaweza kupata hata crack
 
Hivi yule shehe Dogo yuko wapi siku hizi? maana nae yule kwa zuga hajambo

shehe Dogo..!? Duh ndo yupi huyo ebu nifahamishe kidogo, hivi hana jina lingine...! Maana nimimaliza source zangu zote bado kumpata...!
 
SHEHE DOGO, ni yule mtoto wa jini, aliyezaliwa anaijua kuran. ni mtoto wa maajabu, babayeke ni jini mahaba. well, nafikri hapa tz tunatakiwa kuwa makini na vita vya kidini. period.
 
Fundi Mchundo,Mwawado,Waberoya,Magobe T,X-Paster,

..nakubaliana na mawazo ya wachangiaji kwamba hizo kauli za kichochezi haziwakilishi msimamo wa majority ya Wakristo/Waislamu.

..nakubaliana nao kwamba hatuna budi kuhukumu WAISLAMU/WAKRISTO woote kutokana na kauli ya MCHOCHEZI MMOJA.

..lakini nadhani tuna wajibu wa kuonya kwamba tukiendelea kuwapa nafasi hawa wachochezi, kuna hatari kwamba mbele ya safari watakuja kusomba wafuasi wengi.

..tunapaswa kuuhami UMOJA WETU WA TANZANIA kutokana na mahubiri ya chuki na uchochezi bila kujali yanatolewa na wachochezi wa imani gani.

..hizo redio zilazimishwe kupinga na kukanusha kauli za kichochezi zilizotolewa. vilevile wahusika wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria zetu.
 
Maneno yako mazuri Fundi Mchundo..., thanx kwa kuliona hilo. Ila tambua kuwa watu wengi huwa hawaangalii kilicho wadondosha... Wanacho angalia wapi wameangukia. Na hili ndo tatizo la watu wengi sana.

Suwala likija kwa jina au anuani ya Uislam, utasoma mambo mengi na hata matusi kisa mwandishi au mzungumzaji ana jina lenye asili ya kiarabu au Kiyahudi. Utasoma au kusikia WAISLAM haoo...Inferiority complex.... na maneno kadha wa kadha.

Kwenye jukwaa la dini mambo yalianza kidogo kidogo...! Wapendwa walipoona wanazidiwa kwa hoja wakaja na style mpya ya matusi. Na hii ni mojawapo ya mbinu zinazotumiwa sana kwenye mijadala ya kwenye internet ili kupoteza mwelekeo wa mada husika. Na ukikosea tu ukajibu kwa asira lawama zote zitakushukia wewe uliye jibu yale matusi kuwa ndo ulioanza. (Na hilo ndio lengo lao).

Na huko mitaani tunayaona haya sana. Wakristo wanajuwa kuwa waislam hawawezi kumtukana Nabii Yesu, mama yake au mtume yoyote aliye tajwa kwenye mkusanyiko wa vitabu vya Biblia. Na wanalijuwa hilo ndo maana wao wanajiona kuwa wana bahati kubwa sana ya kuwatukana Waislam na imani yao. Sasa ikitokea mtu mmoja kausema vibaya Ukristo lawama zinawaendea waislam wote duniani.

Soma jinsi vile ninavyo jibishana nao hawa wapendwa kule kwenye jukwaa la dini kisha kuwa mkweli na nafsi yako na mbele ya yule unaye amini kuwa ndo mungu wako. Kisha utajuwa nina maanisha nini.

Insha'Allah M'Mungu akuongoze.
 
Matatizo ni kuwa sisi ambao tuko dini moja na hao wachochezi ( awe mkristu, muislamu, baniani n.k) tunachelea sana kuwakana kuwa hawatuwakilishi.

Mimi ningekuamini zaidi kama huko kwenye jukwaa la dini ungekuwa unawakemea waislamu wenzako wachache wanaotoa lugha ya matusi dhidi ya wakristu. Kuwashupalia wapuuzi wakikristu wakati unawaonea aibu wapuuzi wa dini yako hakutatupeleka mbali. Tunatakiwa WOTE kama jamii kukemea na kuvikana vitendo hivyo badala ya kujificha nyuma ya kivuli kuwa ni wachache tu wenye mawazo kama hayo. Tutajuaje kama wote mko kimya wakati wanayasema.

JokaKuu yuko sawa kabisa. Panatakiwa kuwa na zero tolerance vitendo kama hivi vinapotokea. Si kwa dini tuu. Uchochezi wa aina yoyote ( kikabila, rangi, jinsia, ulemavu n.k.) usipewe nafasi katika jamii yetu.
 
Ni kweli unalilosema. Jana nilipita Kariakoo jioni pale wanaposubiria magari ya kwenda Mtongani/Mbagala, loo...! Kulikuwa na lugha hizo! "Waambie 'makafiri' wenzako kuwa Ukristo siyo dini... uliletwa na paulo" Huwa inaniuma kuitwa kafiri kwa vile naamini ni tusi ni kama kumwambia mtu shetani.

Binafsi, siamini kuna kafiri duniani. As long as people exist, they must beileve in a religion. Even atheists have a religion because to say "God does not exist" is itself an affirmation of his existence for if he didn't exist they couldn't even have thought of his "non-existence". i.e Atheists also believe in God even if they think he doesn't exist.

Kurudi kwa hao jamaa wa Kariakoo, nilichowaambia ni kwamba wanapoteza muda bure kuanza kuhubiri kuhusu dini ya wenzao na kusahau kabisa wanachotakiwa kufanya katika dini yao.

Binafsi, naona ni 'projection' ya 'weaknesses' wanazoshindwa kuzishughulikia katika maisha au dini yao na kuzifanya kuonekana ziko nje ya maisha au dini yao wenyewe. Kwenye Uislamu kuna mambo mengi sana ya kuwahubiria watu na 'imagine' yote hayo taratibu yanaanza kupuuzwa au kusaulika na waumini au wahubiri wanaoshupalia Ukristo.

Dini yoyote 'legitimate' haidhoofiki kwa kupingwa na watu fulani hata kama wataweza kujieleza kuliko wengine. In fact, what those guys are doing is just to strengthen Christianity and weaken their own religion.

Kwangu mimi dini inajengwa wakati waumini wake wanashirikiana kuiimarisha zaidi na siyo kushirikiana kuongea kuhusu dini nyingine. Kila mtu ana uhuru wa kuamini kile anachoamini. Kama Wakristo wanaamini Yesu ni Mungu waache waamini na kama Waislamu hawaamini hivyo waache waendelee kutoamini. Kwangu mimi hakuna tofauti kwani naona wote hawa wako sahihi!

Lakini kutopeza muda kuonyesha nani anaamini kweli na nani haamini haisaidii kitu. Binafsi naamini wote tunaamini Mungu mmoja yuleyule lakini 'interpretations' zetu ndiyo tofauti.

Niilishatoa mfano wa chupa kuwa: 'suppose' chupa ipo mezani na watu wameizunguka pande zote. Je, wakiambiwa kila mmoja achore jinsi anavyoiona pale alipo, wote watachora picha zinazofanana? Si kila mmoja atachora kutoka upande aliopo?

Anayeiangalia kutoka juu, picha yake haitakuwa sawa na yule anayechora kutoka chini au pembeni.

Lakini wote watakuwa wamechora kuhusu chupa. Hata Mungu ni hivyohivyo: Ni Mungu mmoja, lakini tunamg'amua (experience him) kwa namna tunavyomu'conceive' hata kama 'we conceive him wrongly but at least we conceive him'.

Na hizi 'perceptions' zetu kuhusu Mungu zinabadilika (boreka) kulingana na jinsi watu wanvyozidi kumng'amua zaidi.

Vilevile, Mungu anaendelea kujifunua kwetu siku hadi siku. Kwa hiyo, hakuna njia kamilifu ya kuweza kumwelezea Mungu jinsi alivyo.. he's beyond our philosophies and understanding! Kitu kimoja ambacho kingetusaidia ni hiki: LOVE WHAT YOU BELIEVE IS TRUE AND RESPECT WHAT OTHERS BELIEVE IS TRUE!

Tukifanya hivyo, tutaondokana na mizozo tuliyo nayo. Mtu akinihubiria kuwa nimepotea, anajisumbua - anapoteza muda bure kwani naamini niko katika njia sahihi.

Ila akinielekeza namna ya kumpenda Mungu na watu zaidi, kunionyesha njia 'positively', kudumisha amani na ushirikiano, kuongeza uadilifu, kutenda matendo ya fadhila au kuwatendea watu haki - hapo nitamsikiliza. Kwani hayo ndiyo mahubiri haswa!
 
Matatizo ni kuwa sisi ambao tuko dini moja na hao wachochezi ( awe mkristu, muislamu, baniani n.k) tunachelea sana kuwakana kuwa hawatuwakilishi.

Mimi ningekuamini zaidi kama huko kwenye jukwaa la dini ungekuwa unawakemea waislamu wenzako wachache wanaotoa lugha ya matusi dhidi ya wakristu. Kuwashupalia wapuuzi wakikristu wakati unawaonea aibu wapuuzi wa dini yako hakutatupeleka mbali. Tunatakiwa WOTE kama jamii kukemea na kuvikana vitendo hivyo badala ya kujificha nyuma ya kivuli kuwa ni wachache tu wenye mawazo kama hayo. Tutajuaje kama wote mko kimya wakati wanayasema.

JokaKuu yuko sawa kabisa. Panatakiwa kuwa na zero tolerance vitendo kama hivi vinapotokea. Si kwa dini tuu. Uchochezi wa aina yoyote ( kikabila, rangi, jinsia, ulemavu n.k.) usipewe nafasi katika jamii yetu.

Well said mkuu.
 
Maneno yako mazuri Fundi Mchundo..., thanx kwa kuliona hilo. Ila tambua kuwa watu wengi huwa hawaangalii kilicho wadondosha... Wanacho angalia wapi wameangukia. Na hili ndo tatizo la watu wengi sana.

Suwala likija kwa jina au anuani ya Uislam, utasoma mambo mengi na hata matusi kisa mwandishi au mzungumzaji ana jina lenye asili ya kiarabu au Kiyahudi. Utasoma au kusikia WAISLAM haoo...Inferiority complex.... na maneno kadha wa kadha.

Kwenye jukwaa la dini mambo yalianza kidogo kidogo...! Wapendwa walipoona wanazidiwa kwa hoja wakaja na style mpya ya matusi. Na hii ni mojawapo ya mbinu zinazotumiwa sana kwenye mijadala ya kwenye internet ili kupoteza mwelekeo wa mada husika. Na ukikosea tu ukajibu kwa asira lawama zote zitakushukia wewe uliye jibu yale matusi kuwa ndo ulioanza. (Na hilo ndio lengo lao).

Na huko mitaani tunayaona haya sana. Wakristo wanajuwa kuwa waislam hawawezi kumtukana Nabii Yesu, mama yake au mtume yoyote aliye tajwa kwenye mkusanyiko wa vitabu vya Biblia. Na wanalijuwa hilo ndo maana wao wanajiona kuwa wana bahati kubwa sana ya kuwatukana Waislam na imani yao. Sasa ikitokea mtu mmoja kausema vibaya Ukristo lawama zinawaendea waislam wote duniani.

Soma jinsi vile ninavyo jibishana nao hawa wapendwa kule kwenye jukwaa la dini kisha kuwa mkweli na nafsi yako na mbele ya yule unaye amini kuwa ndo mungu wako. Kisha utajuwa nina maanisha nini.
Insha'Allah M'Mungu akuongoze.

Duu hii kazi kweli kweli... Just thinking aroud: Sijui ni lini tutaacha unafiki...?
 
X-PASTER,

..sina access ya kuingia kwenye ukumbi wa dini, kwa hiyo siwezi kujua una-experience kitu gani huko.

..halafu hii mihadhara na malumbano imekuwepo kwa muda mrefu sasa, na mpaka leo hii imeshindikana kwa upande wowote ule "kushinda kwa HOJA."

..Dini ni suala la IMANI. sasa usitegemee kwamba unaweza ukajenga hoja za kumbadilisha yule anayeamini DINI/IMANI nyingine.

..ukiona muumini amesalimu amri kwa imani nyingine ujue huyo alikuwa hajahitimu au hajakomaa kiimani. huo ndiyo mtizamo wangu, labda nimekosea.

..halafu nadhani kuna kundi kubwa la wasioamini Uislamu au Ukristo, na imani hizo mbili ni vizuri zika-concentrate kwenye kundi hilo.

..katika kuli-target hilo kundi ambalo ni "neutral[non-Muslim/no-Christian]" itakuwa vizuri kama waumini wa imani hizi mbili[Uislamu,Ukristo] watajielekeza zaidi ktk kuelezea mazuri, mema, yaliyo ktk imani zao, kuliko kasoro wanazoziona ktk imani za wenzao.

..kuendelea kulumbana, kutoana kasoro, na kujaribu kupokonyana waumini, kati ya dini za Kikristo/Kiislamu kunatishia amani ya nchi.

..mwisho, Wakristo wengi tu, pamoja na wenzao Waislamu, hawazingatii mafundisho ya dini zao. kuna mmomonyoko mkubwa sana wa kimaadili ktk jamii yetu na dini hizi mbili zingetusaidia kuwarudisha waumini wao ktk mstari.

..wahubiri na wana-mihadhara wangeanza kwa kuelekeza nguvu zaidi ktk kuwahimiza waumini wa dini zao kuzingatia mafundisho na masharti ya dini zao.
 
Duu hii kazi kweli kweli... Just thinking aroud: Sijui ni lini tutaacha unafiki...?

Mkuu upo? Kwanza nilidhani kuna vijana pale Karikaoo (wanposubiria magari ya kwenda Temeke/Mtongani/Mbagala) wanaoanzisha mjadala wakidai wakristo kama wapo waeleze maana ya vifungu wanavyowasomea: mafano imeandikwa wapi kuwa Yesu alisema alikuwa Mungu, Yesu hakuanzisha Ukristo ila Paulo, Yesu hakusali kwenye kanisa ila msikiti na imeandikwa kwenye Biblia, etc.

Leo asubuhi nilikuwa mitaa ya ndani ya Kariakoo karibu na Congo Street na huko nikakuta mabishano makubwa yakiambatana na matusi - "Ndiyo maana mimi nawaita Wakristo wote makafiri. Maana unawaelekeza waamini dini ya kweli hawakuelewi.

Na mimi nitaendelea kuwaambia tu kuwa Ukristo siyo dini, dini ni Uislamu..." Yaani ukisikiliza hata unaanza kupata hasira kwa kashfa zinazotolewa na hao jamaa. Sijui wametumwa? Maana, hawakuachii ueleze kitu bali wao wakueleze na hivyo mwisho inaishia kuwa kelele na kutukanwa.

Naona inabidi wakuu wa dini na serikali walikee hili. Baadaye litakuja kuleta mtafaruku. Maana kila kitu kibaya kinaanza kidogokidogo na kisipokemea kinaongezeka na kuwa kibaya zaidi na hatimaye kuanza uharibifu.
 
Nipo mkuu, Well said. Tusipoangalia hii mihadhara ya kipuuzi itatupeleka pabaya. Watu huwa wanafika mahala wanachoka uvumilivu.

Nimeishi katika moja ya nchi za asean (singapore). Kuna waislamu (maleys) wahindu, wabudha washinto wakristo nk (other races). Hawa jamaa wana amani sana, na kuna religious harmony kubwa mno. Hii inatokana na serikali kuwa na msimamo na kuwa wakali katika issues za dini. Upuuzi kama huo hapo hauna nafasi hata chembe mkuu. Samahani kwa kuuita upuuzi, maana ndivyo navyouona...
 
Hauna haja ya kuomba radhi. Ni upuuzi na ahustahili kupewa nafasi hata chembe. Walio tutangulia walituonya; usipoziba ufa, utajenga ukuta. Ufa ndio huo tunauangalia. Inabidi tuandae basi matofali ya kujenga ukuta!
 
Wakubwa nataka kusema kitu mara moja. Nimesoma malalamiko ya Ubungo. Kusema kweli kitu kimoja watu wafahamu kwamba kuna tofauti kati ya UISLAM na MUISLAM. Muislam ni mtu, na mtu anaweza kusema chochote kilicho kwenye mind yake. Na uislam ni dini ambayo ina guide peace and harmony. Ni deen ambayo inataka muislam aangalie jirani zake, ni deen ambayo iliingia mkataba na Jews in Maddinah kuhusu kupigania madinna pindi itakapoingiliwa na watu wa nchi nyingine kwani ni nchi huru.

Sasa one thing nitawaambia ambayo hata mimi nilikuwa victim Tanzania watu wache wana knowledge ya deen. Majority ni wafuata Imam kasema nini. Something which Islam doesn't entertain.

So, sababu mtu mmoja kasema something against other religion, that doesn't make every muslim to be out of touch. Ni sawa na kusema Evangelical christians wote wanahubiri hate crime sababu Pastor John Hagee amesema "those who live by the Qur'an have a scriptural mandate to kill Christians and Jewse".

Inconclusion, i think watu wanachanga frustration zao za maisha na deen. Those are two different things,
Wasalam Aleikum.
 
Tatizo letu Wa-Tanzania ni moja:-
Imani za kiislam, kikristo na nyinginezo (isipokuwa zile za asili) tumeletewa na 'Wakuja'.
Hawa wakuja katika kueneza imani zao walizieneza kwa njia ya 'shari' ili wapate wafuasi.

Nasi Wa-Tanzania, wengi wetu ni 'vichwa vya wendawazimu' huwa hatuangalii na kutafakari jambo kwa mapana na marefu yake tunafuata tu hata tukiambiwa tuwauwe ndugu zetu ambao hawaamini tunachoamini tunatekeleza mara moja.

Mungu Muumba wa Mbingu na Nchi atusaidie na kutuelimisha Wa-Tanzania.
 
Wakubwa nataka kusema kitu mara moja. Nimesoma malalamiko ya Ubungo. Kusema kweli kitu kimoja watu wafahamu kwamba kuna tofauti kati ya UISLAM na MUISLAM. Muislam ni mtu, na mtu anaweza kusema chochote kilicho kwenye mind yake. Na uislam ni dini ambayo ina guide peace and harmony. Ni deen ambayo inataka muislam aangalie jirani zake, ni deen ambayo iliingia mkataba na Jews in Maddinah kuhusu kupigania madinna pindi itakapoingiliwa na watu wa nchi nyingine kwani ni nchi huru.

Sasa one thing nitawaambia ambayo hata mimi nilikuwa victim Tanzania watu wache wana knowledge ya deen. Majority ni wafuata Imam kasema nini. Something which Islam doesn't entertain.

So, sababu mtu mmoja kasema something against other religion, that doesn't make every muslim to be out of touch. Ni sawa na kusema Evangelical christians wote wanahubiri hate crime sababu Pastor John Hagee amesema "those who live by the Qur'an have a scriptural mandate to kill Christians and Jewse".

Inconclusion, i think watu wanachanga frustration zao za maisha na deen. Those are two different things,
Wasalam Aleikum.

Nakubaliana na yote uliyoyasema. Tatizo ni ukimya wa walio wengi inapotokea mmoja wao anatokeza kuisemea ovyo dini nyingine.

Wakristu wengi wemesema wazi kuwa Pastor John Hagee hawazungumzii. Hata John McCain ilibidi ajitenge nae ilipoonekana kuwa itam-cost kura za wakristu wengi. Ni wajibu wetu sote kusema wazi na kwa sauti kubwa pale ambapo mmoja wetu anapotaka kupandikiza chuki ndani ya jamii yetu. Kukaa kwetu kimya kuna hatari ya kumfanya afikirie tunakubaliana nae na jamii kudhani kuwa anatuwakilisha. Kukaa kimya hakufai. Hatuwezi kutumia kisingizio cha kuwa hawa wanachanganya frustration zao na deen. Ni shurti tuwaeleze ukweli na tuwakanye wasifanye hivyo.
 
Back
Top Bottom