Wana jf nimekuwa nikisoma habari nyingi zinazo andikwa na magazeti ya waislam kama vile: Al-Huda, Al-nuur na mengineyo ila pia hua nasikiliza redio zao kama Radio kheri na Iman radio, pamoja na matamko ambayo mara nyingi wanayatoa. Sasa kinacho nishangaza ni jinsi habari zao nyingi zinakuwa na chuki kubwa kwa wakatoliki, utadhani wamewahi labda kuwafanyia kitu kibaya miaka ya nyuma. Nimekuwa nikiliona hili kwa muda mrefu sasa ila nimeshindwa kupata majibu kwamba mbona hivyo. Kilicho nisukuma kuandika hi mada hapa ni habari ambayo nimeiona kwenye gazeti la Al-Huda. Imeandikwa kwa herufi kubwa mbele. Wizara ya utumishi wa uma wizi mtupu.
Wakatoliki wamesheni sekta nyeti.
.
Nimekuwa nikiona habari za namna hii kwenye mapazeti yao. Pia wiki hii niliona gazeti la Al-nuur limeandika. Mbowe na Slaa wameonyesha mrengo wao wa ukatoliki. Kwa ujumala habari za wakatoliki huwezi kuzikosa haya magazeti kwa muda mrefu. Nadhani wana jf wanaopitia vichwa vya habari vya magazeti haya na hizo radio ni mashahidi. Sasa nachotaka kujua kwanini hizi media zinaandama wakatoliki/ukatoliki. Naomba mlio humu mtujuze kidogo manake naona kuna utofauti mkubwa ukilinganisha na radio za wakatoliki kama radio maria na gazeti la kiongozi ambayo daina zinatoa habari za wakatoliki tu. Naomba kupata sababu hasa ni zipi.