NMB haya makato yenu kwenye mobile app ni makubwa sana na wizi uliovuka mipaka. Ushahidi huu hapa

Ushauri wangu kama umesahau ATM card yako tumia huduma ya CARDLESS kwani makato yake ni madogo kuliko kutoa kwa mawakala wao au hizi Tigopesa na Mpesa
 
Siku zote nimekuwa nikitoa hela kwa kutumia application ya NMB Mobile Bank na mara zote hizo sikuwai kuwa makini na masuala ya ada ya makato ambayo inachukuliwa na hawa NMB, mpaka pale nilipoamua niangalie huwa wanachukua shilingi ngapi ndipo niliposhangazwa zaidi.

Nilianza kutoa laki moja na makato yake yakawa elf 5 na 800+.

Ikaja elf 50-1000000 nikaona wanakata elf 4++

Mwisho nikamaliza na elfu moja tu ambapo walinikata mia nane. Embu fikiria kama utatoa elfu moja kwa kutumia app yao ya kwenye simu basi wao watagawana na wewe hela kwa asilimia 90 yaani iliwezekanaje duniani mtu akatoa elfu moja halafu akakatwa mia nane? hata kama una hela kiasi gani huu ujinga hauwezi kukubaliana nao.

Haya ni makato makubwa zaidi duniani kuwahi kufanywa na benki moja kwa wateja wake.

Ni vyema na ni haki kwa kila Mtanzania mwenye akili timamu akaachana na huu upuuzi wa kukatwa almost asilimia 90 ya fedha anazozitoa hadi asilimia 6 ya kiasi kikubwa, so hizi mobile app za NMB tuzitumie kuangalizia tu salio.

Anayelalamikia dhuluma hizi ni tajiri, hivyo isihusishwe na hila zozote kupoteza lengo.
Ndugu yangu hata kuangalia salio wanakata wanakata wanakata wanakata
 
Back
Top Bottom