Kutoa hela imekua anasa makato ni makubwa app za mikopo kurejesha usikatwe na ya kutuma

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
5,795
2,000
kutoa hela imekua anasa makato ni makubwa app za mikopo kurejesha usikatwe na ya kutuma

Kutoa hela imekua ni anasa sana na gharama ni kubwa sana haya matigopesa,mpesa,airtelmane,yamegeuka kuwa vichinjio kwa wananchi


Mtu anatoa 5000 mnamkata buku

Mtu anatoa 3000 mnakata 600

Kwanini kusiwe na kanuni kwamba kutoa kuanzia 0 hadi 10000 iwe bure?


Kwanini biashara ya miamala makampuni yawanyonye watu kiasi hiki?Kwamba watu wanakamuliwa tu halafu mamlaka husika wamekaa kimya

Kingine ni app za mikopo na marejesho yake mfano unakuta mtu kakopa elfu 5 branch ila kurejesha anatakiwa arejeshe 6000 halaf kutuma kutoka mtandao husika tu branch ada ya kutuma wanakukata elfu 2 means unatakiwa uwe na 8000 hivi kwa hali hii tutakaa tuendelee kweli?

Hiyo sio hivyo tu unakopa 5000 branch au mpawa bado ukitoa unakatwa

Kwanini kusiwe na kanuni kwamba pesa zote tunazokopa kwenye app za mikopo zisiwe na makato ya kutoa au makato ya kutuma wakati wa kurudisha deni?

Hili linawezekana kbs mfano kuna makampuni ya visimbusi yana makubaliano na kampuni za simu kwamba ukilipia makato ni 0 yaani hakuna makato

Nawasilisha
 

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
16,740
2,000
Waziri wa fedha ni Mwigulu Nchemba

Waziri wa Mawasiliano ni DAKTARI WA BINADAMU.

Mkuu wa BOT ni mtu asiye na taaluma ya uchumi/fedha.

Unatarajia nini?
 

Mtoto halali na hela

JF-Expert Member
Aug 10, 2012
33,696
2,000
Hatari, niliwahi kuhamisha pesa mpesa kwenda bank nilikua nalipia kiwanja nilikatwa 3000 iliniuma maana nilikua nipo kinondoni na bank ipo hapo magomeni ni daladala 400 tu. Hyo ilikua mwanzo na mwisho wa kutumia hizi mobile banking
Pole sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom