Nlichokifanya Mwenge Stand Leo... (Toa Maoni Yako)

Nlichokifanya Mwenge Stand Leo... (Toa Maoni Yako)

....., nimefika
Mwenge nasubiria usafiri
kwenda Tegeta, mfukoni
nina Tshs 900/= tu
............

Yakasemwa maneno kibao
ya kunikashifu mule ndani mi nikawa kimya tu nasoma
novel yangu mpaka
tukafika stand ya Mwenge
ktk BP Shell (Pale karibu na
Benk ya Efatta) na
kulikuwa na kafolen kidogo kabla ya kufika.
>> Kufika tu, konda
anashuka na kuanza
kupiga debe . . .
"Tegetaaaaaaa mia
tatuuuuuuuuu . . . . . . ." " Tegeta hiyoooooooo mia
tatuuuu . . . . . . "
..........

.......mimi bado sijaelewa.....nikiangalia hizo point mbili hapo juu.......yaani untaoka Mwenge halafu unafika tena Mwenge.....au kuna Mwenge nyingine siku hizi.....naomba mnieleweshe......
 
Ukiweka kando suala la nauli, mimi hapo nimeendelea kupata uthibitisho kwamba Watanzania wengi wanasumbuliwa na wivu! Mtu anakubali kulipa sh. 1000, lakini anaanza kuleta ubishi eti kwa kuwa imetokea mtu mwingine ametozwa sh. 300, na sio kwa kuwa yeye amekuwa overcharged! Kwa hiyo mkuu Bampani, hata hao waliokuwa wanataka ulipe 1000, wengi wao walikuwa wanataka 'mfanane'
 
Mie huwa naparuana na makonda daily ninapotoka Buguruni kurudi kwangu Lumo, ikifika usiku kwa kuwa kunakuwa na shida ya usafiri kila konda anataja nauli atakayojiskia, basi mie huwa tunanyooshana humohumo ndani ya gari... Imefikia hatua baadhi ya makonda wamenikariri, utaskia we mzee mtata usiguse gari yangu na mie nawajibu ntapandaje bila kuigusa...!??
 
thankx mkuu! Lakini chama changu nacho hakiishi migogoro.

Mkuu kama chama chako ni cdm basi usiogope! hakina mgogoro wowote ule...
yote unayoyasikia ni mipango ya ccm kujinasua kwenye kifo..
si unajua tena kitu kikiwa kinakufa lazma kitapetape sana!
Migogoro yakupandikiza haina maana!
 
Mie huwa naparuana na makonda daily ninapotoka Buguruni kurudi kwangu Lumo, ikifika usiku kwa kuwa kunakuwa na shida ya usafiri kila konda anataja nauli atakayojiskia, basi mie huwa tunanyooshana humohumo ndani ya gari... Imefikia hatua baadhi ya makonda wamenikariri, utaskia we mzee mtata usiguse gari yangu na mie nawajibu ntapandaje bila kuigusa...!??

Aisee Mwenyekiti... Boxer (motorcycle)!! Itakufikisha Lumo haraka bila bugudha yoyote...
rudi jukwaa unaloliongoza..
Uongee na members! Tuanze mpango kabambe wakukutoa kwenye daladala..
 
Big up bro hakika umeonyesha kwamba watanzania wengi tunaendelea kuwa maskini kwa vile hatujui kudai haki zetu
 
Nakupongeza, ila sasa yule dada nae alidai hela na mimaneno aliyokuwa akikutolea?
 
SOKO huria kasema elfu moja moja
kama ukiona huna si ungojee la kufanana na hela yako,
but
hata hivyo pole sana mtu mzima yakikukuta kama hivyo ni lazima unatahayarika
lakini ningekuwa nimekaa jirani na wewe ningekulipia tu hiyo hela wala usingeaibika,
pole sana lakini.
 
.....wangejua siri ya wewe kukataa kulippa buku!!! hahahahaaa ni kukosa mia!!!
ila hongera kwa kujua hakiyo na kuisimamia!!!
 
Huwa naamini 90% ya watanzania ni wajinga na ndo maana hii nchi ipo hivi.Samahanini kama nimewakwaza
 
Haaaa haaaa......"ama kweli ukitaka kujua kipaji chako subiri ufulie"!!!!!!
 
Sijui niseme watanzania wamerogwa! au ni ufinyu wa uelewa; tunashindwa kabisa kuwa na msimamo wa kusimamia hata bei za nauli zinazotuhusu moja kwa moja! ndani ya daladala unamkashifu mwenzio anayeng'angania kutoa nauli halali! konda tena teja linawapangia nauli linalotaka nanyi mnalishangilia....... loh
 
Mkuu safi sana yaani wewe ni Kamanda wa ukweli,ningekuwa karibu ningekupa namba yangu ya simu unitafute tukale bia na kupiga stori kuhusu nchi yetu inavyoendeshwa na wajinga kama hao abiria na huyo dada aliyekulipia nauli na kuanza kutoa mapovu hawa watu wa aina hii ndio wanaifanya nchi hii irudi nyuma kabisa,kuna jamaa kasema kweli kasema mijidada na miabiria ya aina hiyo hata haipigi kura utaisikia ikisema aah mie namaliza kazi yangu then home na mwisho wa mwezi mshahara wangu kibindoni na maisha yanakwenda ngoja wakachague mie simo,pia mijitu kama hiyo unakuta imesoma lakini pia haijui nini maana ya bajeti pia.Kweli wajinga ndio waliwao kama kweli wana hela sana iweje waombe Chenji baada ya kusikia Tegeta mia tatu 300Tsh?
Ahsante ndugu@lakini sinywi pombe. Ntashukuru ukinipa soda.GBU!
 
.......mimi bado sijaelewa.....nikiangalia hizo point mbili hapo juu.......yaani untaoka Mwenge halafu unafika tena Mwenge.....au kuna Mwenge nyingine siku hizi.....naomba mnieleweshe......
Nlipandia ndani mwenge, kwenye stand ya magari ya tegeta. Then c unazunguka kufika mwenge (stand ya tegeta) kwa nje. Kama ni mwenyeji/unapita mara kwa mara mwenge ni rahisi kuelewa. Ahsante
 
bampami

Umefanya vema sana........


Swali langu kubwa ni hili, je ungekuwa na 10,000/= mfukoni bado ungekomaa na miatatu au ungejitutumua na kuona aibu na kuitoa tu hiyo fedha bila shaka?


Regards
 
Last edited by a moderator:
SOKO huria kasema elfu moja moja
kama ukiona huna si ungojee la kufanana na hela yako,
but
hata hivyo pole sana mtu mzima yakikukuta kama hivyo ni lazima unatahayarika
lakini ningekuwa nimekaa jirani na wewe ningekulipia tu hiyo hela wala usingeaibika,
pole sana lakini.

Hili li kichaka la Soko Huria hili....wenye nacho hunufaika kwa mgongo wa wasionacho....so pathetic
 
Back
Top Bottom