Kwanini sekta ya usafiri imegoma kuingia katika mifumo ya kidijitali

Kwanini sekta ya usafiri imegoma kuingia katika mifumo ya kidijitali

contask

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2021
Posts
965
Reaction score
1,972
Habari wakuu.

Leo natamani tujadili mapinduzi ya mifumo ya malipo kwenye sekta yetu ya usafiri wa umma, hasa hapa mjini ambapo kero ya chenji imekuwa ya kudumu. Kila siku tunashuhudia mabishano yasiyo na tija kati ya abiria na makondakta, jambo ambalo linaweza kuisha kabisa tukiamua kubadilisha namna tunavyolipa nauli zetu.

Chukulia mfano unaotokea kila siku, Nauli ni mia Saba, unatoa buku. Kondakta anakuuliza papo hapo "Masta, una mia mbili hapo nikupe jero?" Ukimwambia huna, anakwambia subiri mbele nitakupa. Unasafiri hadi unafika kituo chako cha kushuka, chenji huna na gari linaondoka, mwisho wa siku unaamua tu kumuachia ile mia mbili yako kwa unyonge kwa sababu ya haraka. Piga hesabu abiria ishirini wakiacha mia mbili zao kwa siku, huu unakuwa wizi wa kistaarabu kwa kisingizio cha uhaba wa chenji mtaani.

Sasa tuko kwenye karne ya uchumi wa kidijitali na sasa hivi huduma za Lipa Namba na Selcom Pay zimekuwa sehemu ya maisha yetu, kuanzia kwa mama ntilie hadi kwa wauza mshikaki.

Swali langu la msingi ni kwanini tunashindwa kuleta huu mbadala wa malipo kwenye daladala, bajaji na bodaboda? Inashindikana vipi kila chombo kuwa na sticker yake ya Lipa Namba ili abiria akipanda anahamisha nauli kamili ya mia sita au mia saba bila kuhitaji kubeba fedha taslimu?

Mbadala huu wa kidijitali una faida kubwa sana kiuchumi maana utaondoa kabisa migogoro ya chenji, na utawasaidia wamiliki wa magari kupokea mapato yao moja kwa moja kwenye akaunti zao bila usumbufu.

Zaidi ya hayo, utaratibu huu utarahisisha mzunguko wa fedha na kuokoa muda mwingi unaopotea vituoni wakati wa kuhesabu sarafu na noti zilizochakaa.

Je, kikwazo kikubwa cha sekta hii kutofanya mabadiliko ya malipo kiko wapi? Ni gharama za miamala? uvivu wa jamii kubadilika, au kuna watu wanaona mifumo hii itabana mianya yao ya kupiga hela ya juu?

Wadau na wataalamu wa mifumo ya kifedha humu ndani, hebu tushushe hoja hapa ni mbinu gani zikitumika tutafanikiwa kuachana na malipo ya mkononi kwenye usafiri wa umma.
 
Apa bongo ukiwa unafanya bishara au kua mteja akikisha njia yakwanza ya malipo ni cash money sababu apa mifumo ya mtandao sio ya huakika,siasa sio zakuaminika,uaminifu ni 40% so huo ndio mtihan
 
Apa bongo ukiwa unafanya bishara au kua mteja akikisha njia yakwanza ya malipo ni cash money sababu apa mifumo ya mtandao sio ya huakika,siasa sio zakuaminika,uaminifu ni 40% so huo ndio mtihan
Yeah ni changamoto na ni upi mbadala katika kuongeza mifumo hii ya ufanisi mkuu
 
Bora isiwepo maana kuna muda tunapanda hadi kwa afu20 na tiket online ni 54k bora vshoka wanasaidia kupunguza makal
 
IMG-20260523-WA0000.jpg
 
Bora isiwepo maana kuna muda tunapanda hadi kwa afu20 na tiket online ni 54k bora vshoka wanasaidia kupunguza makal
Sasa mkuu vishoka watoke wapi na nauli zinajulikana na latra
 
Askari atapataje mgao?
Mpiga debe?
Vipi ikifika jioni, konda na dereva watagawana vipi ikiwa hela imeshafika kwa tajiri?

Bila kusahau wazee wa "mke wangu bandika ugali, mboga naleta sasa hivi"
 
Vipi ikifika jioni, konda na dereva watagawana vipi ikiwa hela imeshafika kwa tajiri?

Bila kusahau wazee wa "mke wangu bandika ugali, mboga naleta sasa hivi"
Hapo sio lazima account iwe ya boss inaweza kua ya dereva wanaangalia mapato ya siku then wanagawana
 
Back
Top Bottom