Leo mida ya jioni narudi
kutoka kazin, nimefika
Mwenge nasubiria usafiri
kwenda Tegeta, mfukoni
nina Tshs 900/= tu
>> Coins 2 za 200/= >> Noti ya 500/=
Nikawa nimepanga zangu
kwamba, kutoka Mwenge -
Tegeta nalipa 300/= then
500/= nachukua Bajaj
mpaka home. Nipo stand ya Mwenge pale ndani, mara
basi hiloooo likaingia.
Konda anashuka na kuanza
kupiga debe .. . .
"Tegetaaaaaaa elfu mojaa
mojaaaa . . . . . Tegetaaaa elfu mojaaaaaa"
Nikawaza sana . . . .
nikaamua kuzamia ndani ya
gari vivo hivyo!
Gari ikajaa, dreva akaanza
kuwasha gari na kuondoka. Ile amevuka tu
geti la kutokea mabasi pale
Mwenge konda
akazoza . . . . .
"Abiria tumalizane hapa
hapa kabla hatujaenda mbali . . . "
Gari ilikuwa imejaa kabisa
watu waliokaa ktk viti, na
wawili waliosimama
Akaanza kukusanya Tshs
1,000/= za nauli. Kufika kwangu nikampa zile coins
2 za mia mbili mbili . . . .
Konda akaniangalia weeee,
kisha ananijibu . . .
"Oyaa brazaaa, masihara
hayo . . . . Inamaana hukusikia nilivyosema nauli
buku au unajifanyisha
makusudi?"
Nikamjibu "Ningesikia
Mwakyembe amepandisha
nauli wala nisingekuwa na ubishi, ila ninachojua mimi
nauli ni 300/= tu, hapo
nirudishie mia yangu"
Konda ikabidi amwambie
dereva wake
" Oyaaa mwanangu, kimeshanuka, simamisha
gari, kuna jamaa analeta
mizinguo mwanangu".
Dereva akasimamisha kweli
na akazima gari kabisa,
kisha akajibu "Siendeshi gari mpaka alipe
nauli iliyotajwa"
Abiria si wakanigeukia,
tena hasa akina mama na
akina dada na sauti zao
kaliii na makelele kibao . . . . "Weeee kaka, kama huna
hela shuka banaa,
usitucheleweshe hapa, si
tumeshachoka saa hizi"
Nikawajibu "Kushuka
sishuki na kama vp tulale humu humu ndani ya gari'
Basi mabishano
yakaendelea kama dk 10
hivi huku mi nikiendelea
kushikilia msimamo wangu.
Mwisho konda akamwambia dereva
wake . . . "Oyaa mwanangu
twen'zetu, achana nae huyo
----". Konda akasusa kabisa
nauli yangu na akaanza
kumalizia wengine wanaotoa hizo buku buku.
Ile tumefika krk round-
about nikamsikia dada
mmoja akisema
"Kondaaaaa, chukua hela
hii hapa namlipia huyo mkaka aliyeshindwa
kulipa . . . . . jianaume
liziiiimaaaa, linashindwa
kulipa elf moja, loooh. Hata
aibu haoni"
Nikamwangalia yule dada weeee, nikamjibu "Ewala
dada, nashukuru we tajiri
kwa kunilipia, ni masikini
tu, asante"
Yakasemwa maneno kibao
ya kunikashifu mule ndani mi nikawa kimya tu nasoma
novel yangu mpaka
tukafika stand ya Mwenge
ktk BP Shell (Pale karibu na
Benk ya Efatta) na
kulikuwa na kafolen kidogo kabla ya kufika.
>> Kufika tu, konda
anashuka na kuanza
kupiga debe . . .
"Tegetaaaaaaa mia
tatuuuuuuuuu . . . . . . ." " Tegeta hiyoooooooo mia
tatuuuu . . . . . . "
Si abiria wakaanza
kulalamika . . . .
"Weee konda turudishie
chenji zetu basiii . . . . we kondaaaa . . . . . "
Konda akagoma kurudisha
chenji. Mi nikawa kimya tu
kama vile sijui
kinachoendelea@