Nlichokifanya Mwenge Stand Leo... (Toa Maoni Yako)

Nlichokifanya Mwenge Stand Leo... (Toa Maoni Yako)

Bongo ukidai haki yako kama kugoma kulanguliwa eti wanakuona roho mbaya badala ya kukuunga mkono. Tuache ufala
 
Leo mida ya jioni narudi
kutoka kazin, nimefika
Mwenge nasubiria usafiri
kwenda Tegeta, mfukoni
nina Tshs 900/= tu
>> Coins 2 za 200/= >> Noti ya 500/=
Nikawa nimepanga zangu
kwamba, kutoka Mwenge -
Tegeta nalipa 300/= then
500/= nachukua Bajaj
mpaka home. Nipo stand ya Mwenge pale ndani, mara
basi hiloooo likaingia.
Konda anashuka na kuanza
kupiga debe .. . .
"Tegetaaaaaaa elfu mojaa
mojaaaa . . . . . Tegetaaaa elfu mojaaaaaa"
Nikawaza sana . . . .
nikaamua kuzamia ndani ya
gari vivo hivyo!
Gari ikajaa, dreva akaanza
kuwasha gari na kuondoka. Ile amevuka tu
geti la kutokea mabasi pale
Mwenge konda
akazoza . . . . .
"Abiria tumalizane hapa
hapa kabla hatujaenda mbali . . . "
Gari ilikuwa imejaa kabisa
watu waliokaa ktk viti, na
wawili waliosimama
Akaanza kukusanya Tshs
1,000/= za nauli. Kufika kwangu nikampa zile coins
2 za mia mbili mbili . . . .
Konda akaniangalia weeee,
kisha ananijibu . . .
"Oyaa brazaaa, masihara
hayo . . . . Inamaana hukusikia nilivyosema nauli
buku au unajifanyisha
makusudi?"
Nikamjibu "Ningesikia
Mwakyembe amepandisha
nauli wala nisingekuwa na ubishi, ila ninachojua mimi
nauli ni 300/= tu, hapo
nirudishie mia yangu"
Konda ikabidi amwambie
dereva wake
" Oyaaa mwanangu, kimeshanuka, simamisha
gari, kuna jamaa analeta
mizinguo mwanangu".
Dereva akasimamisha kweli
na akazima gari kabisa,
kisha akajibu "Siendeshi gari mpaka alipe
nauli iliyotajwa"
Abiria si wakanigeukia,
tena hasa akina mama na
akina dada na sauti zao
kaliii na makelele kibao . . . . "Weeee kaka, kama huna
hela shuka banaa,
usitucheleweshe hapa, si
tumeshachoka saa hizi"
Nikawajibu "Kushuka
sishuki na kama vp tulale humu humu ndani ya gari'
Basi mabishano
yakaendelea kama dk 10
hivi huku mi nikiendelea
kushikilia msimamo wangu.
Mwisho konda akamwambia dereva
wake . . . "Oyaa mwanangu
twen'zetu, achana nae huyo
----". Konda akasusa kabisa
nauli yangu na akaanza
kumalizia wengine wanaotoa hizo buku buku.
Ile tumefika krk round-
about nikamsikia dada
mmoja akisema
"Kondaaaaa, chukua hela
hii hapa namlipia huyo mkaka aliyeshindwa
kulipa . . . . . jianaume
liziiiimaaaa, linashindwa
kulipa elf moja, loooh. Hata
aibu haoni"
Nikamwangalia yule dada weeee, nikamjibu "Ewala
dada, nashukuru we tajiri
kwa kunilipia, ni masikini
tu, asante"
Yakasemwa maneno kibao
ya kunikashifu mule ndani mi nikawa kimya tu nasoma
novel yangu mpaka
tukafika stand ya Mwenge
ktk BP Shell (Pale karibu na
Benk ya Efatta) na
kulikuwa na kafolen kidogo kabla ya kufika.
>> Kufika tu, konda
anashuka na kuanza
kupiga debe . . .
"Tegetaaaaaaa mia
tatuuuuuuuuu . . . . . . ." " Tegeta hiyoooooooo mia
tatuuuu . . . . . . "
Si abiria wakaanza
kulalamika . . . .
"Weee konda turudishie
chenji zetu basiii . . . . we kondaaaa . . . . . "
Konda akagoma kurudisha
chenji. Mi nikawa kimya tu
kama vile sijui
kinachoendelea@

..........Laiti kama mngepatikana watu watano wenye msimamo kama wa kwako Makonda wangekomaje!!!! tatzo la Wa Bongo waoga na hawajui kudai haki zao

 
..........Laiti kama mngepatikana watu watano wenye msimamo kama wa kwako Makonda wangekomaje!!!! tatzo la Wa Bongo waoga na hawajui kudai haki zao


Jamaa mwiz wa status za watu
 
bampami , ungekua na elfu 2 ungelipa hio buku? Mimi nafkiri ulikomaa kwa sana kwasbabu hukua na options. Lakini resistance yako isingekua kubwa hivyo kama ungekuwa nayo hio hela? Au nakosea?
nyamgluu ni kweli kabisa lakini yale maamuzi design kama yalikuja automatical, yamkini kwa sa7bu nlikuwa na hela kidogo mfukoni.
 
Juzi nimepanda daladala wakati wa kushuka nimeshatoa nauli konda akatoa gari nikawaambia wanirudishie nauli au wanirudishe kituoni wakati nabishana nao akatokea abiria mmoja akawa anawaunga mkono dreva na konda kwanini sikushuka mapema kwa sababu najua haki yangu niliwakomalia ikabidi warudishe nauli ila kuna watu wanaona kama wamezaliwa ili wanyanyaswe wanashindwa hata kusimamia haki zao ndogo tu na mbaya zaidi wanasapoti huo upuuzi
 
si haba ata na hao ambao wamejifaka kutoa hizo 1000/= zao fundisho wamelipata i hope next time hawatajipendekeza tena, ila pole sana kwa mashambulizi uliyoyapata kutoka kwa hao ma-mama kitendo cha wewe kukaa kimya zaidi ya kutoa shukrani kwa mama aliyekulipia japo amekulipia kwa kukusimanga nacho ni cha kijasiri hongera sana.
 
...... dada
mmoja akisema "Kondaaaaa, chukua hela hii hapa namlipia huyo mkaka aliyeshindwa kulipa . . . . . jianaume liziiiimaaaa, linashindwa kulipa elf moja, loooh......

huyu dada hiyo pesa ama kahongwa na kidume fulani, au ndio anakwenda kudungwa apate mshiko so akaona unataka kumcheleweshea mingo yake.......
 
Sina mbav umeniacha hoi sana ile ya “kulala humuhumu” lkn ndo vizuri safi sana mwanang maana kuna watu hawajui haki zao za msingi
 
hahahahaha...kaka nikija huko kwenu nitakupa soda...aise una akili nyingi sana
 
Leo mida ya jioni narudi
kutoka kazin, nimefika
Mwenge nasubiria usafiri
kwenda Tegeta, mfukoni
nina Tshs 900/= tu
>> Coins 2 za 200/= >> Noti ya 500/=
Nikawa nimepanga zangu
kwamba, kutoka Mwenge -
Tegeta nalipa 300/= then
500/= nachukua Bajaj
mpaka home.
@
Vipi kama ungekuwa na pesa ya ziada ungefanya kama ulivyofanya? Au mefanya hivo kutokana na tight budget?
 
Kama watanzania wote tungekua kama ww tungemaliza upuuzi unaofanywa na makondakta na madereva wa daladala,
Mimi niliwahi kupelekwa kariakoo peke yangu na costa kutoka magomeni mwembechai baadaya ya daladala kukata route kuwa inaishia mwembechai, mi nikakataa kushuka wala kurudishiwa nauli, ingawa tangu napanda pale sinza kwa remi alishatangaza mwisho mwembechai,
Tulipofika makomeni niwaambie wanioneshe leseni ya sinza- mwembechai wakasema wanaenda gereji gari mbovu nikawaambia tuende polisi wakatoe maelezo kwanini wanpakia abiria kwenye gari mbovu, wakaogopa wakanipeleka mpaka kariakoo peke yangu.
 
Daahh....long time mazee...nafurahi kukusoma........unajua nini mkuu.....hata mimi mwanzo sikuelewa.......nilielewa kama vile anatoka Mwenge halafu akafika tena Mwenge!!......mpaka mwenyewe bampami akanielewesha.......kuwa kuna "Mwenge ndani"....duuh......na "Mwenge BP karibu na Efatha".....duuh!

hii lugha yetu ya Kiswahili ngumu kuielewa wakati mwingine aisee.....lol

Ah Compadre nambie mazee. Tunazeekaje? Hehehe fabulous to here from u as well! Keep keepin on!!
 
kuna abiria wana viherehere ndio hao hawapigi kura kutwa kulalamikia serikali

kwahiyo kutoka ndani ya geti hadi nje ya geti ni 700 da,ni kweli wakumlaumu ni sisi wenyewe na wahusika wa usafiri hapa jijini,ni kweli huo ndio usafiri usio rasmi wa Tegeta,tegeta kuna shida kubwa ya usafiri ifikapo mida ya jioni na ni abiria wenyewe wakulaumiwa,siku hizi hata kutoka Posta kuja mwenge ni 2000 kwa kutumia vi Noah,na Mwakie kaka kimya kua wakati alisema hili jambo atalifanyia kazi,lakini kalala usingizi wa pono,yeye akitoka kunduchi ni full AC
 
Du hiyo inakumbusha route ilikatishwa nikagoma kushuka peke yangu, abiria wengine wanashuka huku wanalalamika hawa makonda wajinga sana, nikawaambia, makonda wana akili sana, wajinga nyie mnaoshuka wakati hamjafika kwenye kituo cha mwisho, konda ana akili anajua akifaulu kukatiza route anaserve time, mafuta na anaongeza trip zake, sasa linakuja suala la willing buyer, willing seller kama buyer mjinga analiwa kwa hiari yake mwenyewe
 
kivipi Pilau ni mwizi CPU?

Acha wizi wa post za watu weweeee . . . . kujifanya tukio limekutokea wewe wakati hujui lolote, ume copy na ku paste
Yaani mpaka watu wanakuita we Mpeli . . . . wewe ni Mpeli wewe?
 
Sasa nauli 400.

Hata kujibu hoja za watu inakushinda, maana umelala tu kitandani halafu unadai eti KILICHONITOKEA LEO MWENGE?
Heheheheh . . . . . unaiba hadi post?? Kweli wewe mufilisi kabisa kimawazo
Kaibe zingine, zipo kibao nimeziweka
 
We need Aggressive people as you gentlemen,many thanks 2u!
 
Back
Top Bottom