bampami
JF-Expert Member
- Nov 5, 2011
- 5,700
- 4,126
Leo mida ya jioni narudi kutoka kazin, nimefika Mwenge nasubiria usafiri kwenda Tegeta, mfukoni nina Tshs 900/= tu >> Coins 2 za 200/= >> Noti ya 500/= Nikawa nimepanga zangu kwamba, kutoka Mwenge - Tegeta nalipa 300/= then 500/= nachukua Bajaj mpaka home.
Nipo stand ya Mwenge pale ndani, mara basi hiloooo likaingia.Konda anashuka na kuanza kupiga debe .. . ."Tegetaaaaaaa elfu mojaa
mojaaaa . . . . . Tegetaaaa elfu mojaaaaaa" Nikawaza sana . . . .nikaamua kuzamia ndani ya gari vivo hivyo!Gari ikajaa, dreva akaanza kuwasha gari na kuondoka. Ile amevuka tu geti la kutokea mabasi paleMwenge konda akazoza . . . . ."Abiria tumalizane hapa hapa kabla hatujaenda mbali . . . "
Gari ilikuwa imejaa kabisa watu waliokaa ktk viti, na wawili waliosimama Akaanza kukusanya Tshs 1,000/= za nauli. Kufika kwangu nikampa zile coins 2 za mia mbili mbili . . . .Konda akaniangalia weeee,kisha ananijibu . . ."Oyaa brazaaa, masihara hayo . . . . Inamaana hukusikia nilivyosema nauli buku au unajifanyishamakusudi?" Nikamjibu "Ningesikia Mwakyembe amepandisha nauli wala nisingekuwa na ubishi, ila ninachojua mimi nauli ni 300/= tu, hapo nirudishie mia yangu" Konda ikabidi amwambie dereva wake " Oyaaa mwanangu, kimeshanuka, simamisha gari, kuna jamaa analeta mizinguo mwanangu".
Dereva akasimamisha kweli na akazima gari kabisa,kisha akajibu "Siendeshi gari mpaka alipe nauli iliyotajwa" Abiria si wakanigeukia,
tena hasa akina mama na akina dada na sauti zao kaliii na makelele kibao "Weeee kaka, kama huna hela shuka banaa, usitucheleweshe hapa, si tumeshachoka saa hizi" Nikawajibu "Kushuka sishuki na kama vp tulale humu humu ndani ya gari' Basi mabishano yakaendelea kama dk 10 hivi huku mi nikiendelea kushikilia msimamo wangu.
Mwisho konda akamwambia dereva wake "Oyaa mwanangu twen'zetu, achana nae huyo ----". Konda akasusa kabisa nauli yangu na akaanza kumalizia wengine wanaotoa hizo buku buku.
Ile tumefika krk round-about nikamsikia dada mmoja akisema "Kondaaaaa, chukua hela hii hapa namlipia huyo mkaka aliyeshindwa
kulipa jianaume liziiiimaaaa, linashindwa kulipa elf moja, loooh.Hata aibu haoni"
Nikamwangalia yule dada weeee, nikamjibu "Ewala dada, nashukuru we tajiri kwa kunilipia, ni masikini tu, asante" Yakasemwa maneno kibao ya kunikashifu mule ndani mi nikawa kimya tu nasoma novel yangu mpaka tukafika stand ya Mwenge ktk BP Shell (Pale karibu na Benk ya Efatta) na kulikuwa na kafolen kidogo kabla ya kufika.
Kufika tu, konda anashuka na kuanza kupiga debe "Tegetaaaaaaa mia tatuuuuuuuuu ." " Tegeta hiyoooooooo mia tatuuuu" Si abiria wakaanza kulalamika, "Weee konda turudishie chenji zetu basiii we kondaaaa, Konda akagoma kurudishachenji.
Mi nikawa kimya tukama vile sijuikinachoendelea.