Njombe: Mwanasheria wa Halmashauri afikishwa Mahakamani kwa Kuomba Rushwa ya Tsh. Milioni 1

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,379
8,123
Ni Apolo Elias Laiser ambaye amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya na kufunguliwa Shauri la Kuomba na Kupokea Rushwa ya Tsh. 1,000,000 kinyume na kifungu cha 15(1),(a) na (2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329.

Mwanasheria huyo ameshtakiwa kwa kuomba Rushwa kutoka kwa Ffreday Henrick Mligo ili aweze kuliachia gari lake lililokuwa na Kesi nyingine ya kusafirisha Wahamiaji Haramu kutoka Ethiopia.

Mshtakiwa amekana kuhusika na Makosa yote na yupo nje kwa dhamana hadi Septemba 22, 2023 Kesi hiyo itakarejea Mahakamani kwaajili ya kusikilizwa.

============

Bw. APOLLO ELIAS LAISER ambaye ni Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya Makete mkoani Njombe, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Makete Septemba11, 2023 na kufunguliwa Shauri Na. 27/2023 kwa kosa la kuomba na kupokea Rushwa ya shilingi 1,000,000/=, kinyume na kifungu cha 15(1),(a) na (2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329.

Kesi hii imefunguliwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Makete Mhe. DENIS RWERAMILA MUJWAHUZI ambapo Mshatakiwa anashtakiwa kwa kuomba Rushwa kutoka kwa Mwananchi mmoja (Dereva) - FREDAY HENRICK MLIGO ili aweze kuliachia gari lake lililokuwa na Kesi nyingine mahakamani hapo.

Kesi hiyo nyingine ilifunguliwa na Jeshi la Uhamiaji baada ya gari hilo kukutwa na Wahamiaji haramu kutoka Ethiopia.

Mshtakiwa amekana kosa na yupo nje kwa dhamana hadi Septemba 22, 2023 Kesi hiyo itakaposikilizwa.
 
Rushwa ni adui wa haki, haifai.

Ila sasa mwanasheria wa Halmashauri anakamata vipi gari lililobeba wahamiaji haramu (yaani anapata wapi mamlaka hayo)? Anapata wapi mamlaka ya kuliachia?
 
Rushwa za Serikali ya Samia Suluhu Hassan na magenge yao ya CCM
Rudisha kadi ya Uanachama ya CCM uondokane na Aibu hii.
 
Rushwa ni adui wa haki, haifai.

Ila sasa mwanasheria wa Halmashauri anakamata vipi gari lililobeba wahamiaji haramu (yaani anapata wapi mamlaka hayo)? Anapata wapi mamlaka ya kuliachia?
Labda Mwanasheria alitaka pesa ya kuvuruga ushahid, ili kesi ikose nguvu!!
 
Labda Mwanasheria alitaka pesa ya kuvuruga ushahid, ili kesi ikose nguvu!!
Huyu Mwanasheria ni lazima atakutwa na hatia huko Mahakamani, siku hizi DPP hapandishi kesi za Jinai Mahakamani bila ya Upelelezi kukamilika,na ukiona DPP anakupandisha Mahakamani ujuwe upelelezi umekamilika,na vile vile kama ushahid wako una mashiko!!
 
Back
Top Bottom