BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,119
Afisa Mtendaji wa Kata ya Sagata katika Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Solomom Dunga Mbise, amefikishwa Mahakamani kwa mashtaka 4 ikiwemo Wizi wa Tsh. Milioni 1.62, Ubadhirifu na Ufujaji, Matumizi Mabaya ya Madaraka na Kuisababishia Serikali Hasara.
Katika Kesi ya Msingi, mtuhumiwa akijua ni Mtumishi wa Umma, anadaiwa kufanya Wizi kwa kukusanya fedha za mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Itilima kwa kutumia mashine za Point Of Sale (POS).
Mshtakiwa alikana makosa yote na kuomba mazungumzo ya 'Plea Bargaining' katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ambapo Kesi imeahirishwa hadi Februari 19, 2024 ili aweze kukamilisha hatua hizo.