Njombe: Mtendaji wa Kijiji ashtakiwa kwa kupokea Rushwa ya Tsh. 200,000

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,026
1,622
Mery James Numbi, ameshtakiwa kwa kosa la kuomba na kupokea Rushwa kinyume na Kifungu cha 15(2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (cap 329 Re 2022)

Mshtakiwa akiwa Mtendaji wa Kijiji cha Lupembe Wilayani Njombe aliomba na kupokea rushwa ya Tsh. 200,000 kutoka kwa Irine Justine ili asimchukulie hatua za Kisheria kwa Mtoto wake kutopelekwa shule

Mshtakiwa alikana makosa yote na kupewa dhamana. Shauri hilo limepangwa kusikilizwa tena Aprili 17, 2024

Chanzo: TAKUKURU
 
Uchunguzi uendelee kufanyika akithibitika achukuliwe hatua maana watendaji nao dhurma nyingi sana
 
Hii sheria ipo kwa hawa viongozi wa chini tu ama na viongozi wa juu, Maana kesi za mabilioni zinafunikwa tu !!😊
 
Back
Top Bottom