Njombe: Majambazi wateka Magari na kupora fedha, simu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Watu wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi wamevamia magari zaidi ya saba (7) ikiwemo magari ya mizigo pamoja na basi la abiria katika eneo la Nyaliva katikati ya kijiji cha Nyombo na Kidegembye barabara ya Njombe - Lupembe Halmashauri ya Wilaya ya Njombe wakidaiwa kupora fedha na simu za Abiria.

Baadhi ya Mashuhuda wa tukio hilo Mwamini Hongoli ambaye ni Kondakta wa Basi na Bernad Kawogo Dereva wa Basi ambaye amejeruhiwa kwa kupigwa na bapa la panga amesema uvamizi huo ulitokea wakiwa safarini huku Wavamizi wakiwa wamejiziba usoni kwa mask.

Dereva huyo amenukuliwa akisema “Nilipofika eneo lile nilikuta magari yamepaki sasa Mimi nikawa napita pembeni, mbele yangu tena nikaona zimepaki gari za mnada niliposimama tu nikapigwa na panga kwenye shavu huku wakiniambia rudi kwenye gari yako wakati huo Kondakta wangu akiwa ameshalazwa chini"

Naye Mwamini Hongoli Kondakta wa gari hilo ameeleza yafuatayo ——— > “Kwa kuwa lengo lao lilikuwa ni pesa waliokuwa Wabishi walipigwa sana mimi niliwapa Tsh. Elfu 13 na kulala kifudifudi kwahiyo baada ya dakika kadhaa tukaona pako kimya ndio tukatoa magogo yaliyokuwa yametegwa ili magari yaweze kupita"

Dr. Ayubu Mtulo ambaye ni Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mji Njombe amekiri kupokea majeruhi huyo mwenye umri wa miaka 39 ambaye anaendelea na matibabu huku RPC wa Njombe Hamisi Issa akiongea na AyoTV kwa ufupi kwa njia ya simu na kusema kuwa kwa sasa yupo eneo la tukio wakiendelea na uchunguzi.
 
Kamanda yupo sehemu ya tukio analiangalia hili pia. Kuweni na subira...

Hawa watu ni wa hovyo sana ndio wanaoshinda kutwa nzima mtandaoni kumtukana JPM. Ngoja sasa jambo lao liangaliwe watakoma tu.😳
 
Usinikunbushe wale waliokuwa wakiteka magari njia ya njombe songea, walishawahi teka costa miaka ile wakawavua nguo abilia wote na kutokomea nazo bila kusahau mizigo yao, ilikuwa fedheha isiyo kifani
 
Watu wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi wamevamia magari zaidi ya saba (7) ikiwemo magari ya mizigo pamoja na basi la abiria katika eneo la Nyaliva katikati ya kijiji cha Nyombo na Kidegembye barabara ya Njombe - Lupembe Halmashauri ya Wilaya ya Njombe wakidaiwa kupora fedha na simu za Abiria.

Baadhi ya Mashuhuda wa tukio hilo Mwamini Hongoli ambaye ni Kondakta wa Basi na Bernad Kawogo Dereva wa Basi ambaye amejeruhiwa kwa kupigwa na bapa la panga amesema uvamizi huo ulitokea wakiwa safarini huku Wavamizi wakiwa wamejiziba usoni kwa mask.

Dereva huyo amenukuliwa akisema “Nilipofika eneo lile nilikuta magari yamepaki sasa Mimi nikawa napita pembeni, mbele yangu tena nikaona zimepaki gari za mnada niliposimama tu nikapigwa na panga kwenye shavu huku wakiniambia rudi kwenye gari yako wakati huo Kondakta wangu akiwa ameshalazwa chini"

Naye Mwamini Hongoli Kondakta wa gari hilo ameeleza yafuatayo ——— > “Kwa kuwa lengo lao lilikuwa ni pesa waliokuwa Wabishi walipigwa sana mimi niliwapa Tsh. Elfu 13 na kulala kifudifudi kwahiyo baada ya dakika kadhaa tukaona pako kimya ndio tukatoa magogo yaliyokuwa yametegwa ili magari yaweze kupita"

Dr. Ayubu Mtulo ambaye ni Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mji Njombe amekiri kupokea majeruhi huyo mwenye umri wa miaka 39 ambaye anaendelea na matibabu huku RPC wa Njombe Hamisi Issa akiongea na AyoTV kwa ufupi kwa njia ya simu na kusema kuwa kwa sasa yupo eneo la tukio wakiendelea na uchunguzi.
Kuna wanaosema mkoani kuna vijana wanaojua kupigana.. haya mambo yasikieni tu sio kuyaexperience
 
Back
Top Bottom