Njombe: Lori lapata ajali na kusababisha vifo vya wahamiaji haramu 6 waliokuwa wakisafirishwa kwenye tela

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Tela.png

Polisi mkoa wa Njombe wanamsaka dereva na kondakta wa gari aina ya Scania yenye namba za usajili T.501 AGJ waliosababisha ajali eneo la Iyai na kupelekea vifo vya watu sita na majeruhi nane wote Raia wa kigeni wakisadikika kuwa ni kutoka Ethiopia.

Akizungumza katika eneo la tukio kamishna msaidizi wa Polisi John Makuri Imori amesema ajali hiyo imetokea mapema alfajiri ya kuamkia hii leo, huku watu sita raia wa kigeni, wakiripotiwa kufariki dunia na wengine nane wakiwa majeruhi, ambao wanapatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya wanging'ombe.

"Ajali hii ilihusisha gari namba T 501 AGJ aina ya Scania iliyokuwa na tela lake lenye namba T595 ANJ iliyokuwa inatoka Makambako kuelekea Zambia baada ya kufika hapa tumekuta ndani ya gari kuna mizigo mingi sana ya vifaa vya ujenzi lakini pia baada ya kufungua tela tumekuta watu ambao ni raia wa kigeni na bahati mbaya hatujapata hati zao zozote za kuwatambulisha"amesema Kmanda Makuri

Bado raia hao hawajabainika wazi ni kutoka nchi gani, licha ya kwamba taarifa za awali zinabainisha kuwa ni raia wa Ethiopia.

Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Cloudia Kita ametoa onyo kwa watu wote wanaojihusisha na biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu.

Chanzo: Jambo
 
Hii inanikumbusha story za Nimekusamehe lakini sitasahau za Radio Free Africa
 
Daah,hivi Ethiopia maokoto ni duni sana eeh?
 
Back
Top Bottom