Njia ya kuongeza kipato: Kilimo cha pilipili kichaa kinavyoweza kumfaidisha kijana wa Kitanzania

Jamani mi ndo nimeanza nimelima kama heka moja hivi by July ndio matarajio ya kuanza kuvuna nitawapa mrejesho juu ya hili

Inakuwa ni miezi 3 kwani ndio unavuna mkuu...?

Kwenye Uzi wa mleta mada mbona nimeona kila mwezi unaweza ukavuna mkuu...?

CHASHA FARMING tunaomba utie meno hapa kiongozi naona mwenye nyumba katuachia nyumba wapangaji bila ya funguo wakati watu wanahitaji kuingia ndani mkuu...!

NAWASILISHA.
 
Inakuwa ni miezi 3 kwani ndio unavuna mkuu...?

Kwenye Uzi wa mleta mada mbona nimeona kila mwezi unaweza ukavuna mkuu...?

CHASHA FARMING tunaomba utie meno hapa kiongozi naona mwenye nyumba katuachia nyumba wapangaji bila ya funguo wakati watu wanahitaji kuingia ndani mkuu...!

NAWASILISHA.
Ndo nimeanza mwezi wa pili nilipanda na saizi zimeanza maua matarajio june-july ndo ntaanza kuvuna
 
Nafanya kazi katika kampuni inayohusika na ulimaji na ununuz wa pilipil kichaa

Mie nipo kama afisa kilimo kwa ataehitaj ushaur kuhusu hili zao aje PM nimpe namba aniulze chochote ni Bure

Na hata sasa niko shamban ni zao linalolipa sn
20220417_111940.jpg
20220417_112026.jpg


Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Habari wanajamvi wenzangu!

Tatizo la ajira limekuwa sugu lakini nimekuja na suluhisho ambalo litaweza kuongeza kipato kwa sisi watu wa chini na hasa waliomaliza chuo na kukosa posts.

Naeleza hiki kutokana na Experience yangu na jinsi nilivyofanikiwa kwa kilimo hiki cha pilipili kichaa (African birds eyes chills).

Kwa sasa mimi nauza pilipili hizi madagascar na nachukua Tani 4 mpaka Tano ila kwa mkulima anayetaka kuanza anaweza akaingia mikataba na hawa wannunuzi wa ndani (na ntajikita zaidi kwa wanunuzi wa ndani).

View attachment 1862097
Picha: Pilipili kichaa ikiwa imetoka kuvunwa

BEI YA SASA KWA WANAOUZA PILIPILI:
Kuna makampuni mengi sana yananunua pilipili kichaa ila kuna kampuni moja ambayo mimi ilinitoa hvyo naiamini sana inaitwa BREDAS TRADERS AND GENERAL SUPPLY CO.ltd
Ambao kwao unaingia nao mkataba kuhusu ukishalima wao ndo watanunua Bidhaa zako na wananunua kwa gharama ya Kilo moja Tsh 5000/=

Kwa heka moja unaweza kutoa Kilo 400 kwa mwezi.

Na ukiweka mkataba nao mbegu watakupa na utakatana nao kwemye manunuzi (bei ya mbegu ni Tsh 200,000/=)
.
400x5000= 2,000,000/= ambayo utaipata kwa heka moja kila mwezi na bidhaa hii baada ya kupandwa hudumu kwa miezi 18 sio uongo ni ukweli nilioupitia mpka sasa naweza kuuza mwenyewe Madagascar.


NINI CHA KUFANYA ILI UFAIDIKE NA FURSA HII
  • Uwe na shamba la heka 3 au muungane watu mtimize heka 3
  • Shamba liwe sehemu yenye kuweza kufikika maji (kwaninkilimo hiki kinaweza kuhitaji maji kwa ajili ya kumwagilia
  • Weka mkataba na mashirika kujihakikishia ununuzi wa bidhaa zako baada ya kulimo
  • Mkataba wako utakufanya upate ushauri wa jinsi ya kulima kwa ubora na ufatiliaji wa mara kwa mara kutoka shirikani

MAZINGIRA YA KILIMO HIKI
Zao la pilipili/pilipili kichaa hupendelea mazingira yenye joto la wastani kuanzia nyuzijoto 18°C - 30°C, joto likiwa chini ya nyuzijoto 16°C au zaidi ya nyuzijoto 30°C huathiri utengenezaji wa matunda. Pia kitu muhimu cha kutilia maanani hapa ni kwamba pilipili kichaa hufanya vizuri maeneo yenye joto. Kadiri joto linavyokua kubwa (mpaka kufikia nyuzi joto 30°C) ndivyo jinsi pilipili inavyozidi kuwa kali na yenye ubora zaidi. Ili kupata pilipili yenye ubora inatakiwa joto lisipungue chini ya nyuzi joto 15°C.

Pia mwanga wa jua ni muhimu sana kwa ukuaji wa mazao mengi ikiwemo zao la pilipili kichaa, hakikisha unapanda zao hili mazingira yenye mwanga wa kutosha, usipande mazingira yenye kivuri, zao hili halitafanya vizuri.

Zao hili hufanya vizuri kwenye udongo tifutifu usiotwamisa maji na wenye kiasi cha tindikali kuanzia pH 5.5 - 7.5

Vilevile hufanya vizuri kwenye maeneo yenye muinuko wa mita 1500 kutoka usawa wa bahari.

Kiasi cha mvua kinachohitajika kwa mwaka ni mm 600 hadi mm 1250. Pia njia mbalimbali za umwagiliaji zinaweza kutumika kuzalisha zao hili kama kutumia mifereji (Stream irrigation), njia ya matone (Drip irrigation), mithiri ya mvua (Sprinkler irrigation) n.k. Chamsingi hapo ni kwamba hakikisha shamba lako lina unyevu wa kutosha wakati wote, maji yakizidi shambani au kukiwa na ukame uzalishaji utaathirika kwa kiwango kikubwa.

AINA YA UDONGO
Hufanya vizuri katika aina tofauti za udongo, lakini zingatia usiwe udongo wa kutuamisha maji.Mmea huu hufanya vizuri unapotumia samadi.

MBEGU
Tumia mbegu iliyothibitishwa na kampuni Utalayoweka nayo mkataba .

KUTAYARISHA KITALU
  • Weka kitalu mita moja upana kwa urefu upendao kulingana na mbegu yako.
  • Elekeza kitalu chako upande ambao jua lisiunguze miche.
  • Piga mistari ya 10 cm na weka mbegu, funika udongo kidogo. Weka manyasi makavu na nyunyizia maji asubuhi na jioni.Zinapoanza kuota, ondoa nyasi na weka kivuli mita moja juu na endelea kunyunyizia maji.

KUPANDA
Panda kachachawa miche ikiwa na majani halisi manne. Itakuwa imefika wiki sita.

PALIZI
Palilia mara mbili kwa msimu kuapata mavuno mengi zaidi
Kwa mazao bora panda mmea huu pekee yake 1 meter x 1 meter. Lakini ukitaka unaweza kuchanganya na mmea mingine.
Weka samadi na baada ya wiki moja weka DAP kuongeza rutuba ya udongo. Pia weka CAN baada ya wiki tatu zaidi.

KUHIFADHI UNYEVU
Tandika manyasi makavu ili kuhifadhi unyevu na kuthibiti hali ya joto la udongo.

MATUMIZI YA PILIPILI KICHAA
Umejiuliza kwanini iwe ni zao la gharama sana wakati wengi tunatumia kuongeza kionjo kwenye Chakula (mboga)
Matumizi ya pilipili dunia ni kama ifuatavyo-
1. Hutumika (Baada ya kufanyiwa chemical production) kuwa kitunzio cha vyakula vya watoto
2. Hutumika katika kutengenezea mabomu ya machozi
3. Hutumika katika kutengenezea maji ya kuwasha kwa polisi
4. Hutumika kutengeneza Dawa za kuua wadudu shambani
Na mengine mengi

SOKO LA PILIPILI BADO KUBWA SANA HIVYO TUJIKITE HUMO
Idea nzuri sana Boss
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom