Njia sahihi za kuwakwamua wazazi wasiwe wategemezi kwako siku za mbeleni

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
11,164
15,841
Wazazi wetu ni watu muhimu sana ambao hakuna ambae aliwaomba wamlete hapa duniani,kila mmoja alikuja duniani kwa sababu wazazi wake walitamani mtoto hivyo tumekuja duniani kwa mapenzi ya wazazi na sio mapenzi yetu.

Katika siku za karibuni kumekuwa na malalamiko mengi ya vijana tunaotafuta maisha kusema kuwa wazazi wamekuwa tegemezi,hasa wale walioajiriwa wanaona wazazi wao ni mizigo.

Vijana wengi wanaishia kuwapa wazazi sehemu ya mshahara kila mwisho wa mwezi huku huo ndio ukiwa mfumo wa maisha huku wakitarajia ipo siku wazazi watakuja kujitegemea,hiyo sahau.

Twende wote pamoja tuone jinsi ambavyo unaweza kutumia njia zitakazofanya wazazi wasiwe wategemezi wako hapo baadae.


1. Hakikisha unamfundisha mzazi wako namna ya kuvua samaki,usimpe samaki ikawa ndio mazoea.

2. Ongea na wazazi wako uwaulize kuna fursa gani hapo wanapoishi,fursa ambayo itawafanya wao wapate kipato cha kila siku au cha kuwasogeza.

3. Kubali jinyime jikaze japo kwa miezi kadhaa uwatafutie mtaji wazazi wako kisha unawapa kwa ajili ya kufanyia kazi ile fursa waliyoiona.

Hakikisha wameshaplan jambo ndio uwape pesa,usiwape pesa kwanza kisha ndo watafute cha kufanya.

4. Ukishawapa mtaji hakikisha miezi kadhaa ya mwanzo wa biashara ambayo wameifungua hakikisha unawatoa pesa ya chakula na mambo madogo madogo huku ukisubiria mtaji ukue.

Wengine wakishatoa mtaji wanawakata kabisa wazee wako wakidhanni biashara inaanza kulipa hapo hapo.

5. Wavumilie na usiwaone wasumbufu wakikuambia biashara haiko vizuri,usianze lawama kwamba wanajiendekeza kumbuka biashara nyingi tu zinakufa,hivyo kuwapa mtaji usione umemaliza kazi bado wanakuhitaji.

HITIMISHO.
unapowafungulia wazazi mtaji unawapunguzia kazi ya wao kujidhalilisha kwako kila mwisho wa mwezi.

Haiwezekani mshahara unaopata na wewe unawalipa watu wengine mshahara,kufanya hivyo ni kuzidi kujitia umasikiini katika kazi ama ajira yako.

Kuwa nao bega kwa bega wazazi wako,usiwatupe mkono jio,ee fahari wazazi kuwa na kijana kama wewe.
 
Back
Top Bottom