Njia rahisi ya kupata mtaji wa kuanzisha biashara

Working hard depends on wat ur working for,wakulima vijijin wanawork hard miaka yote,du they have money?
 
4Corners Alliance Group ni kampuni inayotokana na kampuni mama ya Cornerstone LLC iliyopo Las Vegas Marekani. Imeanzishwa mwaka 2012 na mwanzilishi wake akiwa ni David Harrison ambaye alikuwa ni mfanya biashara ya aina ya mtandao (network marketing) katika kampuni ya Herbal Life.

4Corners Alliance Group ni kampuni ambayo imejikita katika kutoa elimu ya ujasiriamali, uchumi, fedha, uwekezaji na biashara kwa kutumia bidhaa mbili kuu:

1. Vitabu vya mtandaoni (e-books)
2. Jarida la kila mwezi la mtandaoni (e-newsletter)

Bidhaa ya vitabu imegawanyika katika madaraja sita, ambavyo ununuliwa kadiri biashara inavyosonga.

Kwakuwa 4Corners ni biashara ya mtandao, unaweza kujenga timu ya watu watakaoangukia kwenye vizazi (levels) vyako tofauti tofauti.

Level 1 inakuwa na watu 4 tu.
Level 2 inakuwa na watu 16 tu.
Level 3 inakuwa na watu 64 tu.
Level 4 inakuwa na watu 256 tu.
Level 5 inakuwa na watu 1,024 tu.
Level 6 inakuwa na watu 4,096 tu.

Kila ngazi ina seti yake ya vitabu vikiwa na dhima tofauti na kwa bei tofauti.

Level 1 ni $10
Level 2 ni $10
Level 3 ni $25
Level 4 ni $60
Level 5 ni $150
Level 6 ni $300

Unaweza kuvinunua vitabu vyoote hivi kwa hela yako mwenyewe ukajisomea mwenyewe.

Lakini pia unaweza kuvinunua kwa malipo unayoweza kuyapata kwa kujenga timu ya watu chini yako.

Hapa ndo unakuja mpango wa kuunda timu ili kujenga kipato cha kukuwezesha kununua vitabu zaidi na kujipatia ziada kubwa kabisa.

Inafanyaje kazi?

Unapojiunga tu kwa $18, $8 ni ya usajili na $10 inanunulia vitabu vya level 1.

Unapoanza kujenga timu hiki ndicho kinatokea kati yako na kampuni:

Watu walioko level 1 wakinunua level 1 (wakati wa kujiunga) kwa $10, utalipwa jumla ya $4 x 4 = $16, na mdhamini wako atalipwa $16 bonus ya 100%. $2 x 4 = $8 inabakia kwa kampuni kama faida yake.

Watu walioko level 2 wakinunua level 2 kwa $10, utalipwa jumla ya $4 x 16 = $64, na mdhamini wako atalipwa $64 bonus ya 100%. $2 x 16 = $32 inabakia kwa kampuni.

Watu walioko level 3 wakinunua level 3 kwa $25, utalipwa jumla ya $10 x 64 = $640, na mdhamini wako atalipwa $640 bonus ya 100%.
$5 x 64 = $320 inabakia kwa kampuni.

Watu walioko level 4 wakinunua level 4 kwa $60, utalipwa jumla ya $24 x 256= $6,144 na mdhamini wako atalipwa $6,144 bonus ya 100%. $12 x 256 = $3,072 inabakia kwa kampuni.

Watu walioko level 5 wakinunua level 5 kwa $150, utalipwa jumla ya $60 x 1,024= $61,440, na mdhamini wako atalipwa $61,440 bonus ya 100%. $30 x 1,024 = $30,720 inabakia kwa kampuni.

Watu walioko level 6 wakinunua level 6 kwa $300, utalipwa jumla ya $120 x 4,096 = $491,520, na mdhamini wako atalipwa $491,520 bonus ya 100%. $60 x 4,096 = $245,760 inabakia kwa kampuni.

Nadhani hadi hapo umeelewa kampuni inanufaikaje.

UKUMBUKE KUWA HELA YOTE HIYO ITATOKANA NA MALIPO UNAYOPATA KWA KUJENGA TIMU YAKO NA SIO MFUKONI MWAKO.

KIKUBWA ZAIDI ni 100% bonus.
Hii hutolewa kwa kila kila mtu uliyemuingiza chini yako moja kwa moja.

Baada ya wale wanne tulioona pale mwanzo kila utakayemwingiza atakupatia $4 lakini hatakaa kwenye level 1 yako. System itatafuta pengo itamuweka huko.

Nini faida ya kuingiza watu zaidi?
Unapokuwa na watu wengi zaidi chini yako utafaidi zaidi ile bonus ya 100%. Bonus hii utolewa pindi pale mtu uliyemwingiza moja kwa moja anapoliwa. Chochote atakacholipwa unalipwa kwa 100% wewe ukiwa ndo mdhamini wake.

Mfano: Ukiwa na watu 20 na kila mmoja akawa amelipwa $50, ina maana utalipwa $50 x 20 = $1,000 papo hapo.

..sio utani..ni kweli...

Vitu muhimu:

1. Hakuna kikomo cha uanachama.
2. Hakuna kukimbizana na deadlines. Kila mtu anafanya kwa starehe zake. Spidi yako mafanikio yako.
3. Bidhaa inajiuza yenyewe.
4. Hakuna kutoa hela nyingine mfukoni mwako baada ya $18.

JARIDA LA KILA MWEZI (e newsletter):

Hili jarida utoka kila mwezi mara moja na gharama yake ni $29.95. Ya kuzingatia ni haya:

1. Sio la lazima.
2. Hautalipwa kamisheni zake kama hulichukui.
3. Inashauriwa kulichukua pindi unapokea malipo ya level 4.
4. $29.95 inakatwa kwenye kamisheni zako.

Kwa kila anayelichukua jarida hili unalipwa ifuatavyo:

Level 1: $1 x 4 = $4
Level 2: $1 x 16 = $16
Level 3: $1 x 64 = $64
Level 4: $1 x 256 = $256
Level 5: $2 x 1,024 = $2,048
Level 6: $2 x 4,096 = $8,192
Level 7: $4 x 16,384 = $65,536

Hiki ni kipato cha kila mwezi..ndioo...kila mwezi!

NINALIPWAJE?

Uapojiunga unapewa ofisi yako ya mtandaoni (backoffice), ambayo utatumia kuangalia maendeleo yako, ya timu yako, mapato yako na kutoa pesa. Pia, vitabu ulivyokwisha kuvilipia unaweza kuvichukia (download) na kuvisoma ukipenda.

Maombi ya kutoa hela yanafanyika siku ya J2, J3 na J4, na malipo yatafanyika J4 itakayofuata kupitia Visa/Mastercard ya benki yako, na utaweza kutoa kupitia ATM za hapa hapa kwetu au akaunti yako ya benki.

Naanzaje kufanya kazi?

Kinachohitajika ni:
1. $18
2. Email (isiwe Yahoo au AOL)
3. Link/jina la mdhamini wako

Hakikisha fursa hii haikupiti! Ni ya kipekee sana katika ulimwengu wa biashara za mtandao.
how much have you made so far chief..
 
Ndugu wanajamvi poleni na majukumu!!!
Jamani hii "BIADHARA YA MTANDAO" iacheni hivi hivi. Kuna mada nyingi humu kuihusu lakini watu walizipondaaaa!!! na mm nikiwemoooo!!!!
Lakini sasa nimenyoosha mikonoooo!!! Wameshindaaaaa!!
Cha ajabu zaidi haijalishi Elimu, Jinsia, Maumbile n.k. Yeyote yule anafanyaaaaaa!!
Watanzania hivi tumepofushwa na nn hadi tusiione au hata tukiiona hatuielewiiiiii hii "FURSA"?????? Nashangazwa na vilio vya kutafuta ajira kila siku humu ndani wakati fursa za kujiajiri zipooooo!!!!!! Mara utasikia mm nina pHd sina ajira wakati wanafunzi wa mwaka wa 1 wanaingiza hadi mil 5 kwa mwezi katika hii biashara!!! Duuuuuuh!!!
Kuna watu zaidi ya mil 58 duniani wanafanya hii kitu na kufanya mauzo kati ya dola BILIONI 80 _ 110 Sawa na Tshs. TRILIONI 176 _ 242 kwa mwaka. HUKU NDIPO WANAPOKAA MABILIONEAAAAAAA!!!!
Hebu cheki hivi vidude vichache tu utakavyopata ukiwa mfanya hii Business!!!**
1. Mtaji mdogo unakufanya MILIONEA!!
2. Kipato kisicho na kikomo
3. Kujipatia kipato kikubwa kila mwezi.
4. Kupata nafasi ya kupata vipato vya njia
nyingi kama mapato ya timu, uongozi, gsri,
afari za kimataifa na gawio la faida na
mikutano ya viongozi.
5. Biashara yenye mafanikio isiyoumiza
kichwa,isiyohitaji kuajiri, kupangiwa masaa
ya kufanya kazi, mtaji mkubwa naelimu
kubwa. Ni biasharanzuri na iliyo nyepesi
6. Kumiliki biadhara yako na kuwa bosi wako
mwenyewe
7. Kupata nafasi ya kushirikiana na watu wenye
upendo, upeo na mawazo makubwa
8. Kupata nafasi ya kukua bila mipaka na
kutambulika
9. Kuwakilisha bidhaa za pekee na zenye ubora
wa hali ya juu.
10. Kufanya kazi kwa uwezo ulionao.
11. Kujinunulia gari ninalotaka.
12. Kujenga nyumba yenye thamani.
13. Kusaidia na kushirikisha wengine popote!!!
ATAKAYEHITAJI KUIFANYA AU MAELEZO ZAIDI
NI 0768577654 (sms/whatsapp)
 
Nitajiunga na mimi nadhani tuna uelewa mdogo wa haya mambo. Nimeshuhudia watu walio kwenye networking business wakinufaika sana. $18 nitakubali kuzi risk bila ku risk huwezi kufanikiwa zikipotea na zipotee nishapoteza zaid ya hizo.
 
Heshima kwenu wadau,
Kibiashara kuna njia nyingi za kupata mtaji wa biashara hasa kwa zile zinazoanza ingawa nyingi kati ya hizo ni NGUMU sana, hivyo kupelekea watu wengi kuwa na mawazo mazuri ya kibiashara lakini hushindwa kuyafanikisha kutokana na mitaji. Kwa mtazamo wangu, naona kama ukitumia njia ya kuomba fedha kidogo kidogo kutoka kwa watu wengi walio karibu yako, wanaokuamini, kukuheshimu, kukufahamu na wenye uwezo kiasi itakuwa njia rahisi ukilinganisha na mikopo kutoka taasisi za kifedha ambapo utajikuta unafanya biashara kwa presha na hofu ya kurejesha deni. unaweza kufanya kama ifuatavyo kwa kuchukulia uhitaji wa mtaji wa Tsh 10,000,000:

1 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 100,000 kutoka kwa watu 100 = Tsh 10,000,000
2 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 200,000 kutoka kwa watu 50 = Tsh 10,000,000
3 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 350,000 kutoka kwa watu 30 = Tsh 10,000,000
4 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 500,000 kutoka kwa watu 20 = Tsh 10,000,000
5 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 1,000,000 kutoka kwa watu 10 = Tsh 10,000,000

NB: - Naamini tunafahamiana na watu wengi sana tangu mtoto unakua hadi hapo ulipo, kuanzia uliocheza nao, marafiki wa primary, sekondary, vyuo, kazini, majirani, ndugu, jamaa, marafiki, marafiki uliojuana nao kwenye mitandao kama JF, Facebook, Twitter nk..nina hakika hutakosa watu wasiopungua 100 wenye nia, uelewa na uwezo wa kukufanikishia hili.
- Uhitaji, madhumuni ya kuomba, muda wa kurejesha, malengo ya matumizi inategemea na makubaliano yako na unayemuomba, na si lazima hao watu utakao waomba wajue kusudio lako la njia hii ya kupata mtaji, pia usiombe kama msaada, omba kama mkopo ili baada ya muda mfupi kama miezi miwili ama mitatu uahidi kurejesha.
- Nina imani kiasi cha Tsh 10,000,000 ni mtaji tosha kwa biashara ndogo ndogo kwa kuanzia. Mfano: jiko la baa, kibanda cha chips, salon ya kiume, stationary, internet cafe, duka la jumla, duka la kawaida, genge, grecery, bajaji, duka la nguo hasa mitumba bomba nk.. ambapo itakuwa rahisi kwako kwa muda wa miezi mitatu kuweza kurejesha fedha ulizoomba.

Nawasilisha.

Mkuu januari hukuifanyia utafiti .
Ningumu sana hio hata kuliko kupata mkopo bank.

Hebu ndugu jaribu wewe azima laki kwa watu Mia tena waambie baada ya miezi 6 nitarudisha.

Ukifanikiwa tuletee jawabu hapa.
 
Habari wana JF!..
Mimi ni mwanafunzi wa chuo kidogo jijini Arusha ambaye nimekuwa na wazo la kuanzisha biashara itakayonipatia kipato endelevu bila kuathiri masomo yangu lakini "Mtaji" umekuwa kikwazo na changamoto kwangu... Tafadhali kwa yeyote ambaye anaweza kunishauri ni kwa vipi naweza kufanya kitu kikanitengenezea walau kiasi kidogo kidogo mwisho wa siku nikapata pesa ya kutosha ili nianze ujasiriamali... Ushauri wako ndiyo jibu la tatizo langu.. Ahsante
 
Habari wana JF!..
Mimi ni mwanafunzi wa chuo kidogo jijini Arusha ambaye nimekuwa na wazo la kuanzisha biashara itakayonipatia kipato endelevu bila kuathiri masomo yangu lakini "Mtaji" umekuwa kikwazo na changamoto kwangu... Tafadhali kwa yeyote ambaye anaweza kunishauri ni kwa vipi naweza kufanya kitu kikanitengenezea walau kiasi kidogo kidogo mwisho wa siku nikapata pesa ya kutosha ili nianze ujasiriamali... Ushauri wako ndiyo jibu la tatizo langu.. Ahsante

Anza na biashara ndogo ambayo itahitaji mtaji mdogo na ambayo haitaathiri masomo yako.
Nunua voucher za simu halafu wauzie wanafunzi wenzako. Kopesha wanafunzi wenzako wakulipe mwisho wa mwezi kwa riba ya asilimia 10-20%. Endelea kufanya hivi ukiizungusha pesa na hatimaye utapata idea nyingine kubwa kubwa.
Kumbuka kufanikiwa sio lazima uanze na mtaji mkubwa. Angalia 'demand' ya vitu wanavyovihitaji wanafunzi wenzio halafu watimizie.

Good luck!
 
Habari za leo ndugu zangu,

Bila shaka mu bukheri wa afya na mpo katika mapambano ya kuhakikisha uchumi binafsi na uchumi wa nchi unakuwa na kuzifikia ndoto zenu. Nimekuwa nikikutana na maswali kadha wa kadha kuhusu mtaji ambapo wengi husema kwamba kila mtu ana mawazo na ndoto nzuri sana lakini tatizo kubwa likiwa ni mtaji. Leo nitajikita zaidi Kwenye kujibu hoja hizo kwa kutumia hoja zenye mashiko mahususi. Ni kweli isiyopingika kwamba wengi wanaoongea hivyo hawana mbinu yoyote ya kupata mtaji na mawazo yao yakagota ukutani na kuona kizingiti kikubwa mbele yao, yote ni kwasababu wengi huwaza kuwa matajiri sana kutoka sifuri mpaka kuwa milionea ndani ya muda mfupi yaani kwa kifupi hakuna anayetaka kujitoa jasho na kuumiza akili zaidi hivyo hutaka mpaka wapate mtaji ndipo wanaweza kutimiza azma yao ya kufanya biashara. Hapa chini nitaelezea kipengele kimoja baada ya kingine na namna ya kukabiliana na hali hiyo ili kuweza kupata mtaji.

1) WEKA AKIBA HELA YAKO MWENYEWE
Bila kubisha si kwamba watu hawapati hela, vijana wanaweza kujiingiza kwenye biashara au vibarua na kujipatia shilingi mbili tatu ila tatizo kubwa huibuka kwamba hela wanayoipata huiona ndogo sana hivyo kuamua kuitumia tu na hatimaye kuishia kulaumu kwamba mtaji hawana na hawawezi kujiendeleza pasipo kuwa na mtaji wa maana. Njia moja kubwa ya kupata mtaji ni kuweka hela yako mwenyewe akiba ambapo hakikisha unabana matumizi vilivyo na kuweza kuweka angalau 50% ya hela unayoipata mahala ambapo huigusi kisha ndani ya mwaka mmoja utajikuta una hela nzuri tu. Mfano mdogo tu iwapo utaweka akiba shilingi 2000 kwa kila siku ndani ya mwaka mmoja tu wa siku 365 itakuwa ni shilingi laki saba na elfu thelathini (730,000) je mpaka hapo hujapata kianzio cha biashara yako au tatizo huna wazo zuri la biashara ndio maana.

2) ANZA KWA BIASHARA YENYE MTAJI MDOGO
Kiuhalisia watu hudhani kwamba biashara ni lazima uanzie mtaji wa mamilioni ndio uweze kutajirika lakini leo nataka nikupinge kwa hoja. Miaka kadhaa iliyopita nilifanya utafiti mdogo tu na kutambua mtaani kwetu kuna bar nyingi na pia wavuta sigara ni wengi wahiyo nilichokifanya ni kwamba nilienda bar kadhaa na kuongea na meneja wahusika na wamiliki ili waniruhusu kuweka biashara yangu ya sigara katika bar zao. Ombi langu lilikubaliwa na nilichokifanya nilichukua elfu sabini (70,000) nikaingia duka la jumla nikanunua bunda moja moja la sigara ambapo bunda la embassy lenye pakti 10 nikanunua kwa 25,000 kisha bunda la SM kwa 22,500 na bunda la Sports kwa 22,500. Baada ya hapo nikasambaza bunda sita yaani bunda mbili mbili kwa kila sigara kwa bar tano tofauti, kwa hesabu za haraka haraka nilikuwa napata faida ya shilingi elfu 15 kila siku na kwa siku 30 nikawa nina laki nne na nusu je mpaka hapo hujaona nilianza kuwaza kwa mtaji mdogo kisha nikajikuta naingiza hela nyingi kwa kila mwezi? Tatizo letu tunataka mpaka tuwe na mtaji wa milioni kadhaa ndio biashara ifanyike, waza kwa kuanzia chini kisha upasnde taratibu mpaka kufikia pale unapotarajia kufika.

3) JENGA MAZOEA YA KUJITOLEA
Watanzania sisi ni wavivu sana na ndio huishia vijiweni nkumwaga lawama kwa sekta mbalimbali za nchi hii, ulikwishawahi kujiuliza kwamba umefanya nini kwenye jamii yako angalau watu wakakujua? Hebu nikudadafulie kidogo mtaani kwetu kuna kaka mmoja tumezoea kumuita mandevu kutokana na ndevu zake kuwa kama za waarabu. Alianza kuzoa takataka mtaani kwetu ila hapo alishapata vibali husika kutoka kwa mwenyekiti wa mtaa na mtendaji wa kata, akawa anazunguka na toroli lake kuchukua uchafu kila nyumba kisha anawalipisha hela kadhaa kwaajili ya huduma hiyo. Huu ni mwaka wa tatu tangu nimeanza kumuona akizoa takataka na sasa hivi ana maduka yake yapo kimara na ubungo pia ameongeza idadi ya vijana sasa wapo wanne. Kuna mashirika mengi tu Tanzana yetu fanya kujitolea kuweza kupata mbinu mbalimbali na kuongeza uwezo wa kufikiri, unadhani kwa kukaa mtaani ukilalamika unamkomoa nani kama sio wewe mwenyewe? Wawekezaji wengi hupenda kuwekeza kwa mtu ambaye tayari ameshafanya kitu katika jamii, yaani kama ni biashara basi uwe umeianzisha na inaonekana ndio maana hata benki hawawezi kukupa mkopo kama huna biashara na ifikishe miezi sita ndio huamini umekomaa na unaelewa upepo wa biashara ndipo hukupa mtaji, hawawezi kukupa mtaji au mkopo na wakati kutwa upo mtaani unamwaga lawama tu

4) NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI
Hapa ni kuhusu kupata mtaji wa kufanya biashara yako ambapo wengi hushindwa kuwaconvince watu wao wa karibu ili waweze kuwapatia mitaji ya biashara zao. Iwapo huwezi kuwaconvince hao watu wa karibu wakupatie mtaji unadhani utaweza kumconvince mtu wa mbali akupatie mtaji? Nikupe mfano labda wewe ni mwanafunzi wa chuo na unawaza kufanya aina fulani ya biashara ambayo mtaji unaweza kuwa milioni moja au mbili, jenga mazoea na wanachuo wenzako. Mtu kukupa milioni moja ni jambo ambalo haliwezekani kamwe bali kukupa elfu moja inawezekana kabisa, mfano chuo chenu kina wanafunzi elfu mbili jitahidi kufanya kitu kitaalamu ambapo orodhesha majina yao na kozi wanazosoma na pembeni weka kiasi. Mfate mmoja mmoja akusaidie elfu moja moja bila shaka hawezi kukataa kutoa elfu moja, mpaka hapo watu elfu mbili kwa elfu moja moja huoni tayari una milioni mbili? Kama upo mtaani orodhesha majina ya wakazi wa mtaani kwako ambao unaona kabisa kukusaidia elfu moja inawezekana. Wafate kisha kila ukipewa unaiweka mahala mpaka hapo hujapata mtaji wa kuanzia biashara yako? Je tatizo ni huna mtaji au huna mbinu ya maana ya kukusongesha mbele? Kila kitu kinawezekana tatizo sisi tumelaza ubongo na kuishia kuona matatizo tu Zipo njia nyingi sana za kupata mtaji acha kumwaga lawama badala yake utumie muda huo kuwaza kwa kina na kuvumbua mbinu ambazo zitakukwamua kimaisha, epuka sana kuanza kwa kuwaza kuwa na mtaji mkubwa ambao ni ngumu kupata badala yake anza kwa biashara yenye mtaji mdogo na kupanda taratibu mpaka kufikia juu. Kumbuka hata roma haikujengwa kwa siku moja vivyo hivyo hakuna mafanikio yanayokuja kwa usiku mmoja ni lazima uhangaike na kuumiza akili yako zaidi. Asanteni sana kwa kusoma makala hii bila shaka imekupa mwanga wa kipi unachopaswa kukifanya kuweza kupiga hatua ya juu zaidi ya hiyo uliyopo hapo.

Imeandaliwa na
Mtenga Gerald
Mkurugenzi Mtendaji wa
TAECO LTD
taecoltd@yahoo.com, taecoltd@gmail.com, gmtenga@gmail.com www.taecoltd.webs.com
0713332606
 
Poleni na majukumu. Mimi nina ujuzi ambao unaweza ukanizalishia laki nane kwa wiki mbili kama faida ila sina mtaji lengo nikutaka kujua je ninaweza kupata mkopo maana benki wanahitaji dhamana kubwa.
Je wapi naweza pata msaada?
 
poleni na majukumu. mm nina ujuzi ambao unaweza ukanizalishia laki nane kwa wiki mbili kama faida ila sina mtaji lengo nikutaka kujua je inaweza kupata mkopo maana benk wanahitaji dhamana kubwa je wap naweza pata msaada?
Ni ujuzi upi huo ndugu tujue kwanza wa kukuzalishia laki 8 per wiki mbili?
 
Lete dhamana upewe pesa,hapa mjini hakuna wa kumuamini,watu wapo kiujanjajanja tu
 
niwa kutengeneza viatu vya kimasai ndani ya wiki mbili naweza kuzalisha pea 200 na zikaisha pea 200=1600000
 
Back
Top Bottom