Njia rahisi ya kupata mtaji wa kuanzisha biashara

nawashukuru woote kwa mawazo yenu jamani, mmenifumbua macho na kunitoa lile dukuduku lillikua moyoni mwangu,. Mungu awabariki
 
Watu wengine huponda sana hii mitandao lakini kuna maarifa tele. Ahsante wadau kwa nondo zenu
 
Baada ya kuangalia sehemu ya kwanza wiki iliyopita ya jinsi ya kujiajiri bila kuwa na mtaji pesa leo tunaendelea na sehemu ya pili. Kama imetokea umeshindwa kugundua kipaji chako bado kuna uwezekano wa kuanzisha biashara yako bila ya kuwa na mtaji pesa haya kitu cha kwanza ni unatakiwa ujitambue wewe ni nani kati ya mfanyabiashara au mjasiriamali halafu ona aina ya biashara ambayo ndani ya uasili wako mwenyewe ichague kwa umakini halafu andika chini vitu ambavyo unavihitaji ili biashara yako ifanikiwe au ionekane andika pembeni ( Sio mpango biashara)halafu anza kufanya utafiti wa hivyo vituulivoandika kwa kutafutia mbadala wake sehemu zote ambazo zinahitaji pesa ziorodheshe pembeni halafu anza kutafuta mbinu mbadala kwa kila kimoja usikurupuke chukua muda ili ufanye maamuzi mazuri kama ulichochagua kikondani ya sehemu yako ya kujitambua kupata njia mbadala sio kazi ngumu.( Safari ya mafanikio huanzia mbali sana hakuna tajiri ambae alianza huku akiwa tajiri au alianza na mtaji mkubwa )anza kufanya na kushughulikia biashara yako kwa ngazi yako usilazimishe ianzie juu. Kama ulichochagua kweli kiko kwenye damu yako kufeli ni kugumu mfano: Asili ya kabila la wachaga ni biashara hivyo kwa mchaga kuwa mfanyabiashara ni kitu rahisi kuliko msukuma, Mmasai asili yake ni ufugaji ( Mjasiriamali) hivyo kwa huyu kufanya ujasiriamali ni kitu ambacho kiko ndani ya damu yake hivyo ni rahisi kupata mbadala wa changamoto.

Baada ya kupata mbadala wa kila sehemu ya fedha anzisha biashara yako kwa kutumia mibadala hiyo ambayo itakusaidia wewe kukamilisha malengo yako bila ya kugusa pesa yako. Katika biashara kuna mafanikio aina mbili , yanayoonekana na yasiyoonekana watu wengi huangalia mafaniko yanayoonekana tofauti na yasiyoonekana mafanikio yasiyoonekana ndio mafanikio ya kweli kwani mafanikio ya kuonekana ni matokeo ya mafanikio yasiyoonekana. Na mara nyingi unapoanza biashara yako mafanikio yasiyoonekana ndio mengi kuliko mafanikio yanayoonekana watu wengi huishia hapa pia sababu tu yeye anataka mafanikio yakuonekana au watu alionao wanahitaji mafanikio hayo basi anaamua kuachana na hiyo biashara kwa kuona haina matokeo chanya japo yapo hayo matokeo chanya katika maisha yake mwenyewe. Kama unachokifanya unakifanya kwa moyo mmoja mafanikio yake utayaona kwanza wewe ndio wengine watakuja kuyaona lakini wewe kwanza. Pia tatizo kubwa wengi wanahitaji kuwa mabilionea ndani ya miaka au muda mchache . Asilimia kubwa ya matajiri ni wajasiriamali ambao waliwekeza katika biashara, biashara ya ujasiriamali ikikubalika sokoni mafanikio yake ni makubwa .

Usiwe na papara ya mafanikio wakati hauna hata mtaji angalia vitu gani unavyoweza vifanya kwa hatua na uwezo wako kwanza acha kufikiria kama waliofanikiwa wakati hata haujafanikiwa bado.chini hapa ni mfano wa mtu mwenye asili ya ufugaji. Anavyoweza kufanya ufugaji bila ya kutumia pesa ila akili na uwezo.

Mfano: Umejiangalia ukagundua ujasiriamali wako ni kufuga kuku, hauna pesa ya banda wala ya kuhudumia hao kuku achilia mbali kuwanunua kuku wenyewe , kitu cha kufanya kama nilivyosema hapo juu andika vitu vinavyohitaji pesa

1. Banda 2. Matunzo 3. Kuwanunua kuku wenyewe n.k, ondoka nenda sehemu ambapo wanafuga kuku tengeneza

Tengeneza mazoea na mwenye banda, ongea nae kuhusu mpango wako wa kuwa mfugaji pia na mwambie tatizo lako ni mtaji lakini unataka uingie nae makubaliano halafu atakusaidia. Mwambie utamletea au utamuuzia aidha kuku au mayai trei au kiasi fulani cha kuku na ukifikisha wateja kiasi fulani atakupatia kuku na jogoo mmoja , nenda katafute soko na uza kama mlivyokubaliana na ukishafikisha utapewa hapo tayari mtakuwa mmeshazoeana utamuomba waendelee kukaa hapo kwake hadi utakapowatengenezea banda, akikubali subiri hadi kuku atakapototoa chukua yale mayai baadhi yaache mengine toa kwa kuuza kwa vile tayari unawateja unaweza kupeleka na kuuza ukapata kiasi fulani cha pesa hicho kiasi kitunze kama ni kidogo na anza kutengeneza banda dogo la muda subiri kuku wako atotoe tena fanya vivyo hivyo hadi utakaporidhika unaweza kuwahamisha watoe wapeleke kwenye banda lako na sasa utakuwa tayari unasoko na sehemu ya kuwatunzia matunzo yake pia yatatoka katika mayai na utakao amua kuwauza.

UKIWA UNAFANYA KITU KWA MOYO WOTE HUWEZI KUKOSA MBADALA WA CHANGAMOTO.

Fanyia kazi utambuzi wako na biashara ya moyo wako.UTAFANIKIWA tatizo kubwa kwa sasa ni uwezo wa kutambua ipi ndio njia sahihi ya moyo wako sababu wengi wanatamani vingi .
 
Basi si vibaya nami nitoe dukudukulangu.
Nikiwa katika harakati za research ya kufungu biashara nikawa napiga stori na ndugu mmoja akawa ananiambia kwamba
Hapo kariakoo sikuhizi hata wao wenyewe hawapatani kutokana na mfumo wa biashara unaoendeshwa kwa sasa(mtu anafungua biashara kutokana na mtu fulani ameifungua na amefanikiwa hiyohiyo) kitu ambacho kimekuwa kikiwa umiza wafanyabiashara wengi.mfano mtu huchukulia mzigo china wa bidhaa fulani.akikuelekeza inamaana mtaenda kuchukua mzigo wa aina moja na quality hiyohiyo kitu ambacho ukija huku bongo itakuchukua mda kuuza na hata mda mwingine kwake asiuze kabisa kwasababu saiz kutokana na serikali kubana makampuni ya crearing and forwarging kuanza kutumika moja tuu(la kigogo mmoja hapa bongo) wanachofanya wanaenda kule wanakash kidogo ili mzigo wake ukufika tuu utolewe haraka halafu mingine isubiri.
Sasa huo ni ushindani kwa wenye nazo sembuse mfuate mtu akupe mtaji(akukope).
Asili ya bongo ni michango hutolewa mtu akiwa amekufa lakini si yu hai(msibani).
 
Mjomba bora ukope mil 10 sehemu moja kuliko kwa sehemu 100! Hevu fikiria deni la mtu/taasisi moja linavozingua.
Sasa kwa design hiyo ya kwako ina maana timbwili la kudaiwa linakuwa kwa watu tofauti na kila mmoja na design yake ya kudai kama ambavyo mlikubaliana!

Kwa kifupi utapata stres ambazo hutokaa uzisahau katika maisha yako!!

Hahaha kwanz umenfraaisha sana nakuunga mkono asilimia 100 yan kudaiwa na watu mia?na kila. Mtu ana stail yake ya kudai yan n majanga
 
Heshima kwenu wadau,
Kibiashara kuna njia nyingi za kupata mtaji wa biashara hasa kwa zile zinazoanza ingawa nyingi kati ya hizo ni NGUMU sana, hivyo kupelekea watu wengi kuwa na mawazo mazuri ya kibiashara lakini hushindwa kuyafanikisha kutokana na mitaji. Kwa mtazamo wangu, naona kama ukitumia njia ya kuomba fedha kidogo kidogo kutoka kwa watu wengi walio karibu yako, wanaokuamini, kukuheshimu, kukufahamu na wenye uwezo kiasi itakuwa njia rahisi ukilinganisha na mikopo kutoka taasisi za kifedha ambapo utajikuta unafanya biashara kwa presha na hofu ya kurejesha deni. unaweza kufanya kama ifuatavyo kwa kuchukulia uhitaji wa mtaji wa Tsh 10,000,000:

1 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 100,000 kutoka kwa watu 100 = Tsh 10,000,000
2 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 200,000 kutoka kwa watu 50 = Tsh 10,000,000
3 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 350,000 kutoka kwa watu 30 = Tsh 10,000,000
4 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 500,000 kutoka kwa watu 20 = Tsh 10,000,000
5 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 1,000,000 kutoka kwa watu 10 = Tsh 10,000,000

NB: - Naamini tunafahamiana na watu wengi sana tangu mtoto unakua hadi hapo ulipo, kuanzia uliocheza nao, marafiki wa primary, sekondary, vyuo, kazini, majirani, ndugu, jamaa, marafiki, marafiki uliojuana nao kwenye mitandao kama JF, Facebook, Twitter nk..nina hakika hutakosa watu wasiopungua 100 wenye nia, uelewa na uwezo wa kukufanikishia hili.
- Uhitaji, madhumuni ya kuomba, muda wa kurejesha, malengo ya matumizi inategemea na makubaliano yako na unayemuomba, na si lazima hao watu utakao waomba wajue kusudio lako la njia hii ya kupata mtaji, pia usiombe kama msaada, omba kama mkopo ili baada ya muda mfupi kama miezi miwili ama mitatu uahidi kurejesha.
- Nina imani kiasi cha Tsh 10,000,000 ni mtaji tosha kwa biashara ndogo ndogo kwa kuanzia. Mfano: jiko la baa, kibanda cha chips, salon ya kiume, stationary, internet cafe, duka la jumla, duka la kawaida, genge, grecery, bajaji, duka la nguo hasa mitumba bomba nk.. ambapo itakuwa rahisi kwako kwa muda wa miezi mitatu kuweza kurejesha fedha ulizoomba.

Nawasilisha.

Bajaji miezi mitatu bado hujarudisha hela mkuu
 
Hi k2 iliondoka na ujamaa,inawekezekana ila kwa asilimia ndogo sana pia inatokana na mazingira husika hasa kama una ndugu wengi ambao wapo vzr kdgo financially.kwa marafiki ni asilimia ndogo sana.
Hulka ya mwadamu wa sasa iliyo jengwa na sera za ubepari,kila mtu anataka awe juu ya mwenzake hasa kimaendeleo.in short ni ngumu binafsi nimisha ijaribu sitaki hata nikumbuke kilicho nitokea nilihc sina thamani rohoni na machoni mwao.
Huwa ninashangaa sana wale wanao sema cha msingi ni kuwa na wazo <idea>,mtaji si tatizo wanashinda kutambua mazngra ya kiafrika. hata uwe na mawazo/mipango kama trillion iiyo bora kama huna resource especialy (fund) ya ku implement ni sawa na bure
 
Mm natafuta sehemu watakayo kubali niweke dhamana vyeti vyangu vya taaluma toka stnd 7- cha chuo kikuu.wanikope 1M tu Nilirudishe aftr 4mths.
 
Heshima kwenu wadau,
Kibiashara kuna njia nyingi za kupata mtaji wa biashara hasa kwa zile zinazoanza ingawa nyingi kati ya hizo ni NGUMU sana, hivyo kupelekea watu wengi kuwa na mawazo mazuri ya kibiashara lakini hushindwa kuyafanikisha kutokana na mitaji. Kwa mtazamo wangu, naona kama ukitumia njia ya kuomba fedha kidogo kidogo kutoka kwa watu wengi walio karibu yako, wanaokuamini, kukuheshimu, kukufahamu na wenye uwezo kiasi itakuwa njia rahisi ukilinganisha na mikopo kutoka taasisi za kifedha ambapo utajikuta unafanya biashara kwa presha na hofu ya kurejesha deni. unaweza kufanya kama ifuatavyo kwa kuchukulia uhitaji wa mtaji wa Tsh 10,000,000:

1 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 100,000 kutoka kwa watu 100 = Tsh 10,000,000
2 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 200,000 kutoka kwa watu 50 = Tsh 10,000,000
3 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 350,000 kutoka kwa watu 30 = Tsh 10,000,000
4 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 500,000 kutoka kwa watu 20 = Tsh 10,000,000
5 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 1,000,000 kutoka kwa watu 10 = Tsh 10,000,000

NB: - Naamini tunafahamiana na watu wengi sana tangu mtoto unakua hadi hapo ulipo, kuanzia uliocheza nao, marafiki wa primary, sekondary, vyuo, kazini, majirani, ndugu, jamaa, marafiki, marafiki uliojuana nao kwenye mitandao kama JF, Facebook, Twitter nk..nina hakika hutakosa watu wasiopungua 100 wenye nia, uelewa na uwezo wa kukufanikishia hili.
- Uhitaji, madhumuni ya kuomba, muda wa kurejesha, malengo ya matumizi inategemea na makubaliano yako na unayemuomba, na si lazima hao watu utakao waomba wajue kusudio lako la njia hii ya kupata mtaji, pia usiombe kama msaada, omba kama mkopo ili baada ya muda mfupi kama miezi miwili ama mitatu uahidi kurejesha.
- Nina imani kiasi cha Tsh 10,000,000 ni mtaji tosha kwa biashara ndogo ndogo kwa kuanzia. Mfano: jiko la baa, kibanda cha chips, salon ya kiume, stationary, internet cafe, duka la jumla, duka la kawaida, genge, grecery, bajaji, duka la nguo hasa mitumba bomba nk.. ambapo itakuwa rahisi kwako kwa muda wa miezi mitatu kuweza kurejesha fedha ulizoomba.

Nawasilisha.

Kwenye finance tunasema lazma debt equity ratio iwe less than 50%, ikiwa ina maana mkopo unauchukua lazima uwe pungufu ya thaman ya asset ulizonazo ili biashara yako isipoenda afu waliokukopesha wakikudai uwe na uwezo wa kuwalipa sasa kwa mfano mambo yasipooenda vizuri unafkiri utalipaje deni la watu? Ndugu kwenye swala la pesa watu hawana cha urafiki unaeza ukageukwa mda wowote, hii njia uliopendekeza ni risky sana, afu kingine kabla ujakopa hakikisha nawewe unakiasi chochote umuonyeshe huyo unayemkopa uko serious kwani huwa wanapenda mwenye kitu kuliko asiyenacho kabisa.
 
Mimi nazani njia rahisi na kama unalengo itisha kikao cha harusi apo watatoa tena akikisha vikao vya muda mrefu
 
wewe unacheza na mambo ya hela na marafiki.jichulie mfano wewe mwenyewe unamarafiki wangapi?na je ulisha wai kupatwa na matatizo ukaona mwitikio wao?naje unajua rafiki wa kweli utamjua vipi?ndugu unaleta utani...marafiki ndugu wa kibongo hawapendi maendeleo ya mtu,wanafulahia mtu awe na matatizo.sasa wambie marafiki wawili tu utajawasikia wanakupiga majungu ooo hata mimi kaniomba sijui anafikili si hatuna shida

watu wanapenda kuona mtu anapigika...kabla sijapata kazi wala mtaji wowote niliwahi jaribu hii, majibu niyokutana nayo ni ya kukatisha tamaa...
cha msingi ni kukomaa kivyako tu au kutafuta patnership!!
 
Heshima kwenu wadau,
Kibiashara kuna njia nyingi za kupata mtaji wa biashara hasa kwa zile zinazoanza ingawa nyingi kati ya hizo ni NGUMU sana, hivyo kupelekea watu wengi kuwa na mawazo mazuri ya kibiashara lakini hushindwa kuyafanikisha kutokana na mitaji. Kwa mtazamo wangu, naona kama ukitumia njia ya kuomba fedha kidogo kidogo kutoka kwa watu wengi walio karibu yako, wanaokuamini, kukuheshimu, kukufahamu na wenye uwezo kiasi itakuwa njia rahisi ukilinganisha na mikopo kutoka taasisi za kifedha ambapo utajikuta unafanya biashara kwa presha na hofu ya kurejesha deni. unaweza kufanya kama ifuatavyo kwa kuchukulia uhitaji wa mtaji wa Tsh 10,000,000:

1 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 100,000 kutoka kwa watu 100 = Tsh 10,000,000
2 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 200,000 kutoka kwa watu 50 = Tsh 10,000,000
3 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 350,000 kutoka kwa watu 30 = Tsh 10,000,000
4 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 500,000 kutoka kwa watu 20 = Tsh 10,000,000
5 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 1,000,000 kutoka kwa watu 10 = Tsh 10,000,000

NB: - Naamini tunafahamiana na watu wengi sana tangu mtoto unakua hadi hapo ulipo, kuanzia uliocheza nao, marafiki wa primary, sekondary, vyuo, kazini, majirani, ndugu, jamaa, marafiki, marafiki uliojuana nao kwenye mitandao kama JF, Facebook, Twitter nk..nina hakika hutakosa watu wasiopungua 100 wenye nia, uelewa na uwezo wa kukufanikishia hili.
- Uhitaji, madhumuni ya kuomba, muda wa kurejesha, malengo ya matumizi inategemea na makubaliano yako na unayemuomba, na si lazima hao watu utakao waomba wajue kusudio lako la njia hii ya kupata mtaji, pia usiombe kama msaada, omba kama mkopo ili baada ya muda mfupi kama miezi miwili ama mitatu uahidi kurejesha.
- Nina imani kiasi cha Tsh 10,000,000 ni mtaji tosha kwa biashara ndogo ndogo kwa kuanzia. Mfano: jiko la baa, kibanda cha chips, salon ya kiume, stationary, internet cafe, duka la jumla, duka la kawaida, genge, grecery, bajaji, duka la nguo hasa mitumba bomba nk.. ambapo itakuwa rahisi kwako kwa muda wa miezi mitatu kuweza kurejesha fedha ulizoomba.

Nawasilisha.

naomba nikopeshe Laki tatu....!
 
Ur very bright never seen u b4 aisee
 
Ni NGUMU SAANA ila INAWEZEKANA SAANA. Yote hayo yanategemea umejiweka vipi(unajua unachokitaka?, utafanyaje kukipata? Na utahendo vip yote yatokanayo na utakacho?) Mimi nilitumia hiyo namna na nilifanikiwa kwa zaidi ya asalimia 55.
 
Vizr sn.Umejarbu kuonesha upande wa2 wa Shilingi Thank you bro.Kwa wale watakaoweza itawasaidia kwa watakaoshindwa wajarbu njia nyingine.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom