Njia rahisi ya kupata mtaji wa kuanzisha biashara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Njia rahisi ya kupata mtaji wa kuanzisha biashara

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by OGOPASANA, Dec 16, 2011.

 1. OGOPASANA

  OGOPASANA JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  Heshima kwenu wadau,
  Kibiashara kuna njia nyingi za kupata mtaji wa biashara hasa kwa zile zinazoanza ingawa nyingi kati ya hizo ni NGUMU sana, hivyo kupelekea watu wengi kuwa na mawazo mazuri ya kibiashara lakini hushindwa kuyafanikisha kutokana na mitaji.

  Kwa mtazamo wangu, naona kama ukitumia njia ya kuomba fedha kidogo kidogo kutoka kwa watu wengi walio karibu yako, wanaokuamini, kukuheshimu, kukufahamu na wenye uwezo kiasi itakuwa njia rahisi ukilinganisha na mikopo kutoka taasisi za kifedha ambapo utajikuta unafanya biashara kwa presha na hofu ya kurejesha deni. unaweza kufanya kama ifuatavyo kwa kuchukulia uhitaji wa mtaji wa Tsh 10,000,000:

  1 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 100,000 kutoka kwa watu 100 = Tsh 10,000,000
  2 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 200,000 kutoka kwa watu 50 = Tsh 10,000,000
  3 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 350,000 kutoka kwa watu 30 = Tsh 10,000,000
  4 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 500,000 kutoka kwa watu 20 = Tsh 10,000,000
  5 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 1,000,000 kutoka kwa watu 10 = Tsh 10,000,000

  NB: -
  Naamini tunafahamiana na watu wengi sana tangu mtoto unakua hadi hapo ulipo, kuanzia uliocheza nao, marafiki wa primary, sekondary, vyuo, kazini, majirani, ndugu, jamaa, marafiki, marafiki uliojuana nao kwenye mitandao kama JF, Facebook, Twitter nk..nina hakika hutakosa watu wasiopungua 100 wenye nia, uelewa na uwezo wa kukufanikishia hili.

  Uhitaji, madhumuni ya kuomba, muda wa kurejesha, malengo ya matumizi inategemea na makubaliano yako na unayemuomba, na si lazima hao watu utakao waomba wajue kusudio lako la njia hii ya kupata mtaji, pia usiombe kama msaada, omba kama mkopo ili baada ya muda mfupi kama miezi miwili ama mitatu uahidi kurejesha.

  Nina imani kiasi cha Tsh 10,000,000 ni mtaji tosha kwa biashara ndogo ndogo kwa kuanzia. Mfano: jiko la baa, kibanda cha chips, salon ya kiume, stationary, internet cafe, duka la jumla, duka la kawaida, genge, grecery, bajaji, duka la nguo hasa mitumba bomba nk.. ambapo itakuwa rahisi kwako kwa muda wa miezi mitatu kuweza kurejesha fedha ulizoomba.

  Nawasilisha.


  ....................................... For English Audience.....................................


  There are many ways to get a business capital especially for the beginners, though it is not easy, This is why many people have good business ideas but fail to achieve them because of lack of capital. From my perspective, borrowing money from few people around you, is a simple way compared to getting a loan from financial institutions where you will find yourself doing business with fear of debt.

  1 – Ask or Borrow 100,000 Tsh from 100 people = 10,000,000 Tsh
  2 - Ask or Borrow 200,000 Tsh from 50 people = 10,000,000 Tsh
  3 - Ask or Borrow 350,000 Tsh from 30 people = 10,000,000 Tsh
  4 - Ask or Borrow 500,000 Tsh from 20 people = 10,000,000 Tsh
  5 - Ask or Borrow 1,000,000 Tsh from 10 people = 10,000,000 Tsh

  Everyone knows a lot of people so i believe you will get at least 100 people who will be willing to help you out. Don't ask people for money as if you are asking for help but ask for money as you are asking for a loan so that after a few months you will return back the money.
   
 2. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Njia hiyo siyo rahisi kama unavyofikiri, kwa Africa tumrzungukwa na marafiki na ndugu wengi ambao ni tegemezi ( hawana tumaini hata kesho wataishije). Na hapa ndio microfinance zinapigia bao: wanakopesha hadi Tshs.20,000 hapo ndo utajua watu wapo kwenye chronic poverty!
   
 3. happiness win

  happiness win JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,478
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Asante kwa kunifungua akili. Sasa nawaza, huku mtaani kwetu kwa Mtogole, sijui nitaanzia kwa nani?
   
 4. OGOPASANA

  OGOPASANA JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  Ndugu Payuka najua waafrika wengi ni maskini wa hali na mali lakini si wote, si kweli kwamba watu wote unaofahamiana nao ni maskini wa kushindwa kukuazima mifano ya kiasi hicho nilichotaja, pia kumbuka kuwa wewe ukiwa huna wenzio wanao, so usiwakatishe wengine tamaa...fanya utafiti gharama zinazotumika katika sherehe na tafrija mbalimbali kuanzia uswahilini, katika familia zetu hadi serikalini, tembea kwenye kumbi na sehemu mbalimblai za starehe, angalia matumizi ya watu siku za weekend nk.. ni dhahiri utagundua kuwa kuna gap kubwa la wasio nacho na mafisadi (wabadhilifu wa mali), lakini kama tukiweza kusaidiana katika mambo ya msingi hasa yale yanayotuingizia kipato kuliko yanayotumia vipato vyetu nina imani tutafika mbali. Usipinge kitu ambacho wewe mwenyewe binafsi hujajaribu, na usisahawishi wengine kwa kuwakatisha tamaa kwa kuwa wewe umeshindwa.

  ' try and fail but never fail to try'
   
 5. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,167
  Likes Received: 1,894
  Trophy Points: 280
  Hii njia sidhani.. Itakuwa ni Ngumu kidogo.
   
 6. L

  LAT JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  ninafurahi sana kuona kwamba kila kukicha wana jf wanaumiza vichwa jinsi ya kupata mitaji na kukwamuka kibiashara

  big up and God bless
   
 7. OGOPASANA

  OGOPASANA JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  RGforever... umeshawahi kujalibu? kuna mtu ama watu unaowafahamu wameshajalibu njia hii?? unaweza kutusaidia njia nyingine rahisi zaidi ya hii??
   
 8. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wazo zuri lakini unapotegemea watu zaidi ya mmoja ujue kuwa muda watakaoweza kujikusanya na kukupatia huo mtaji utapishana kidogo na hapo malengo yasige kamilika kwa wakati mzuri. Na kama makubaliano ni kurejesha hilo deni kila mwezi usije jikuta unamkopa "Paul" kumlipa "Peter", bila hiyo hela kufanya mzunguko uliotarajiwa.

  Wazo hili la kujumuisha watu wengi linafaa kwenye biashara inayoendelea, ambayo ina uwazi wa kutosha kuweza kuwaonyesha hao unaowalenga kuwa biashara inalipa. Michango yao inakuwa kama msukumo wa kuendeleza hiyo biashara.

  Anzisha biashara, au pata capital ambayo asilimia 51 utakuwa nayo, mfano, katika mil10, uwe na mil5 laki moja. Ukope zinazobaki na hapo utakuwa na control ya hiyo biashara zaidi. Watakaochanga / kukopesha watakuwa junior members kwenye biashara.
   
 9. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #9
  Dec 16, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  wewe unacheza na mambo ya hela na marafiki.jichulie mfano wewe mwenyewe unamarafiki wangapi?na je ulisha wai kupatwa na matatizo ukaona mwitikio wao?naje unajua rafiki wa kweli utamjua vipi?ndugu unaleta utani...marafiki ndugu wa kibongo hawapendi maendeleo ya mtu,wanafulahia mtu awe na matatizo.sasa wambie marafiki wawili tu utajawasikia wanakupiga majungu ooo hata mimi kaniomba sijui anafikili si hatuna shida
   
 10. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #10
  Dec 16, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wazo lako ni zuri na linafanya kazi. hata mimi nilishawahi kuitumia hii model unayoipropose but si kwa watu wengi namna hiyo. Ili ikae vizuri, inabidi utengeneze repayment model itakayokidhi mahitaji ya hao watu waliokuazima hela (kitu ambacho ni kigumu). Kutokakana na ugumu huo unaweza kuta unafunga biashara kwa kushindwa kurejesha kutokana na pressure za hao watu.

  Ushauri wangu ni "Dream Big, Start Small". Jiaribu kuanza na network ya watu kama watatu tu ambao hawada uhitaji na hiyo hela kwa siku za usoni (I mean wawe well off kidogo) ili nawe uweze kupita kile kipindi cha payback period katika biashara yako, mbali na hapo itakuwa ngumu mno
   
 11. L

  LAT JF-Expert Member

  #11
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  a
  Thank you great thinker
   
 12. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #12
  Dec 16, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Inasemwa "MAISHA ni KOMBOLELA, BUTUA UWAOKOE WENZIO".
   
 13. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #13
  Dec 17, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Hiyo kitu ipo san kwa watani wangu wangoni wanaita MAJAMANDA! hahahaa, nendeni benki bana mkakope pesa ziko kibao.
   
 14. libent

  libent JF-Expert Member

  #14
  Dec 17, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 385
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Tena siku hizi hakuna upendo kabisa yaani mpaka mtu akupe laki moja ni inshu
   
 15. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #15
  Dec 17, 2011
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hili swala ni very practicle. Cha kuongeze ni kwamba mkakati wenyewe wa kuraise hiyo milion 10 inabidi uupe muda kama miezi 15 hivi.
  Vilevile ni vyema ukawa unaomba support badala ya kukopa kwa sababu huwezi kuwa na uhakika lini utapata full capital ya kuanzisha biashara. Kama idea ni nzuri watu watakuchangia tu. Na usiweke kiwango rasmi cha mtu kuchangia, take michango from as many people as possible.
  Halafu maisha yako unayoishi kila siku yaonekane kweli ni mtu unayetafuta pesa kwa ajili ya shughuli fulani Watu hawawezi kukuchangia kama wanaona wewe unaendelea na starehe zako kama kawaida.
   
 16. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #16
  Dec 17, 2011
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kwa kuongezea tu, hii njia siyo RAHISI ila ni POSSIBLE.
   
 17. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #17
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wahindi ndio wanaweza kuendesha utaratibu huo na ndio unaowatajirisha, waswahili bana ahadi zitakuwa kibao na hakuna kinachoingia kwenye account yako.
   
 18. Habdavi

  Habdavi JF-Expert Member

  #18
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 393
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45

  Tukiweza kupunguza michango ya harusi na kitchen party inawezekana kabisa. Nilisoma makala moja inayosema, michango ya harusi kwa mwaka ni zaidi ya Tsh 4 billion kwa mwaka.
   
 19. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #19
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Ogopasana naomba unikopeshe milioni moja.
   
 20. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #20
  Dec 18, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,118
  Trophy Points: 280
  Wakuu hii kitu si kwamba haiwezekani, inawezekana sana ila kwa c c watanzania kuna tatizo moja kubwa sana na ambalo itachukua muda mrfu kulibadilisha,

  - KENYA HII KITU INAFANYA KAZI, NA HATA NCHI ZINGINE KAMA ZA WAZUNGU, TATIZO LETU NI
  1. Unafiki ni mkubwa sana
  2. Wivu
  3. Kuto aminiana


  - Ni zungumzie la WIVU, chukulia mfano wa Ada za shule, Kenya wanaweza kusomesha watoto wengi hata nje ya nchi kwa kupitia Harambee, na ukisiliza Radio KBC ya kenya matangazo mengi ni ya Harambee ya kuchangia mtoto wa fulani anaenda kusoma nchi za nje, WAKENYA KWENYE SWALA LA KUCHANGIA NDUGU AKASOME HAWANA WIVU KABISA

  - Njoo kwa Sisi Watanzania, Ndugu, Marafiki, Majirani na kazalika hawako tiyali kumchangia mtu kitu ambacho wanafahamu kitakuwa na Faida kubwa sana kwa mchangiwa,

  - Harusi huwa zinachangia Pesa nyingi sana Si kwamba wanapenda sana anae changiwa No bali wanafahamu hizi Pesa wanazo changa hata kama mchangaji hatahuzuria harusi zitaliwa tu, Wanachanga kwa sababu wanajua hazitakufaidisha wewe maishani zaidi ya kukufaidisha siku moja tu ya Harusi

  - WAKUU FAHAMUNI HILO, KWAMBA HARUSI ZINACHANGIWA KWA SABABU WANAJUA MWISHO WA SIKU HIZO PESA ZITALIWA/ZITATUMIKA SIKU YA HARUSI

  - JARIBU KUWAAMBIA WAKUCHANGIE MTOTO AKASOME, HAMNA ATAKAE CHANGA KWA SABABU WANAHUA MTOTO AKISOMA TAFAIDIKA YEYE NA ATAKUJA KUWAZIDI KIMAISHA,

  - KWENYE BIASHARA NDO KABISA, WANAJUA UTAWAZIDI, NDUGU KWA NDUGU HUWA HAWATAKI KUONA NDUGU MWENZAO ANAKUA JUU KULIKO WAO, WANATAKA MUWE LEVO MOJA NA IKIBIDI WAKUZIDI WAO NA SI WEWE UWAPIKU.

  WAKUU WIVU NA UNAFIKI NDO KIKWAZO KWA HILI

  KIFANYIKE NINI?

  1. My be Wakati wa mtu kutaka kuoa hapo ndo mtu awe anatumia mwanya huo kutafuta mtaji wa biashara mfano ukichangiwa milioni 15, unafanya harusi ya milioni 5, milioni 10 zinakuwa mtaji, ingawa watalaumu sana kwamba hawakushiba lakini wewe utakuwa umefanya jambo la maana sana.

  TOFAUTI NA HAPO NDUGU HAWAKO TIYALI KWA SABABU UTAFAIDIKA NA UTAWAZIDI
   
Loading...