Njia rahisi ya kupata mtaji wa kuanzisha biashara

Heshima kwenu wadau,
Kibiashara kuna njia nyingi za kupata mtaji wa biashara hasa kwa zile zinazoanza ingawa nyingi kati ya hizo ni NGUMU sana, hivyo kupelekea watu wengi kuwa na mawazo mazuri ya kibiashara lakini hushindwa kuyafanikisha kutokana na mitaji. Kwa mtazamo wangu, naona kama ukitumia njia ya kuomba fedha kidogo kidogo kutoka kwa watu wengi walio karibu yako, wanaokuamini, kukuheshimu, kukufahamu na wenye uwezo kiasi itakuwa njia rahisi ukilinganisha na mikopo kutoka taasisi za kifedha ambapo utajikuta unafanya biashara kwa presha na hofu ya kurejesha deni. unaweza kufanya kama ifuatavyo kwa kuchukulia uhitaji wa mtaji wa Tsh 10,000,000:

1 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 100,000 kutoka kwa watu 100 = Tsh 10,000,000
2 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 200,000 kutoka kwa watu 50 = Tsh 10,000,000
3 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 350,000 kutoka kwa watu 30 = Tsh 10,000,000
4 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 500,000 kutoka kwa watu 20 = Tsh 10,000,000
5 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 1,000,000 kutoka kwa watu 10 = Tsh 10,000,000

NB: - Naamini tunafahamiana na watu wengi sana tangu mtoto unakua hadi hapo ulipo, kuanzia uliocheza nao, marafiki wa primary, sekondary, vyuo, kazini, majirani, ndugu, jamaa, marafiki, marafiki uliojuana nao kwenye mitandao kama JF, Facebook, Twitter nk..nina hakika hutakosa watu wasiopungua 100 wenye nia, uelewa na uwezo wa kukufanikishia hili.
- Uhitaji, madhumuni ya kuomba, muda wa kurejesha, malengo ya matumizi inategemea na makubaliano yako na unayemuomba, na si lazima hao watu utakao waomba wajue kusudio lako la njia hii ya kupata mtaji, pia usiombe kama msaada, omba kama mkopo ili baada ya muda mfupi kama miezi miwili ama mitatu uahidi kurejesha.
- Nina imani kiasi cha Tsh 10,000,000 ni mtaji tosha kwa biashara ndogo ndogo kwa kuanzia. Mfano: jiko la baa, kibanda cha chips, salon ya kiume, stationary, internet cafe, duka la jumla, duka la kawaida, genge, grecery, bajaji, duka la nguo hasa mitumba bomba nk.. ambapo itakuwa rahisi kwako kwa muda wa miezi mitatu kuweza kurejesha fedha ulizoomba.

Nawasilisha.
Kufahamiana ni jambo moja na kuaminika ni jambo lingine. Na mambo yasipoenda vizuri? Naona umekurupuka na wazo lako
 
Habari za leo ndugu zangu,

Bila shaka mu bukheri wa afya na mpo katika mapambano ya kuhakikisha uchumi binafsi na uchumi wa nchi unakuwa na kuzifikia ndoto zenu. Nimekuwa nikikutana na maswali kadha wa kadha kuhusu mtaji ambapo wengi husema kwamba kila mtu ana mawazo na ndoto nzuri sana lakini tatizo kubwa likiwa ni mtaji. Leo nitajikita zaidi Kwenye kujibu hoja hizo kwa kutumia hoja zenye mashiko mahususi. Ni kweli isiyopingika kwamba wengi wanaoongea hivyo hawana mbinu yoyote ya kupata mtaji na mawazo yao yakagota ukutani na kuona kizingiti kikubwa mbele yao, yote ni kwasababu wengi huwaza kuwa matajiri sana kutoka sifuri mpaka kuwa milionea ndani ya muda mfupi yaani kwa kifupi hakuna anayetaka kujitoa jasho na kuumiza akili zaidi hivyo hutaka mpaka wapate mtaji ndipo wanaweza kutimiza azma yao ya kufanya biashara. Hapa chini nitaelezea kipengele kimoja baada ya kingine na namna ya kukabiliana na hali hiyo ili kuweza kupata mtaji.

1) WEKA AKIBA HELA YAKO MWENYEWE
Bila kubisha si kwamba watu hawapati hela, vijana wanaweza kujiingiza kwenye biashara au vibarua na kujipatia shilingi mbili tatu ila tatizo kubwa huibuka kwamba hela wanayoipata huiona ndogo sana hivyo kuamua kuitumia tu na hatimaye kuishia kulaumu kwamba mtaji hawana na hawawezi kujiendeleza pasipo kuwa na mtaji wa maana. Njia moja kubwa ya kupata mtaji ni kuweka hela yako mwenyewe akiba ambapo hakikisha unabana matumizi vilivyo na kuweza kuweka angalau 50% ya hela unayoipata mahala ambapo huigusi kisha ndani ya mwaka mmoja utajikuta una hela nzuri tu. Mfano mdogo tu iwapo utaweka akiba shilingi 2000 kwa kila siku ndani ya mwaka mmoja tu wa siku 365 itakuwa ni shilingi laki saba na elfu thelathini (730,000) je mpaka hapo hujapata kianzio cha biashara yako au tatizo huna wazo zuri la biashara ndio maana.

2) ANZA KWA BIASHARA YENYE MTAJI MDOGO
Kiuhalisia watu hudhani kwamba biashara ni lazima uanzie mtaji wa mamilioni ndio uweze kutajirika lakini leo nataka nikupinge kwa hoja. Miaka kadhaa iliyopita nilifanya utafiti mdogo tu na kutambua mtaani kwetu kuna bar nyingi na pia wavuta sigara ni wengi wahiyo nilichokifanya ni kwamba nilienda bar kadhaa na kuongea na meneja wahusika na wamiliki ili waniruhusu kuweka biashara yangu ya sigara katika bar zao. Ombi langu lilikubaliwa na nilichokifanya nilichukua elfu sabini (70,000) nikaingia duka la jumla nikanunua bunda moja moja la sigara ambapo bunda la embassy lenye pakti 10 nikanunua kwa 25,000 kisha bunda la SM kwa 22,500 na bunda la Sports kwa 22,500. Baada ya hapo nikasambaza bunda sita yaani bunda mbili mbili kwa kila sigara kwa bar tano tofauti, kwa hesabu za haraka haraka nilikuwa napata faida ya shilingi elfu 15 kila siku na kwa siku 30 nikawa nina laki nne na nusu je mpaka hapo hujaona nilianza kuwaza kwa mtaji mdogo kisha nikajikuta naingiza hela nyingi kwa kila mwezi? Tatizo letu tunataka mpaka tuwe na mtaji wa milioni kadhaa ndio biashara ifanyike, waza kwa kuanzia chini kisha upasnde taratibu mpaka kufikia pale unapotarajia kufika.

3) JENGA MAZOEA YA KUJITOLEA
Watanzania sisi ni wavivu sana na ndio huishia vijiweni nkumwaga lawama kwa sekta mbalimbali za nchi hii, ulikwishawahi kujiuliza kwamba umefanya nini kwenye jamii yako angalau watu wakakujua? Hebu nikudadafulie kidogo mtaani kwetu kuna kaka mmoja tumezoea kumuita mandevu kutokana na ndevu zake kuwa kama za waarabu. Alianza kuzoa takataka mtaani kwetu ila hapo alishapata vibali husika kutoka kwa mwenyekiti wa mtaa na mtendaji wa kata, akawa anazunguka na toroli lake kuchukua uchafu kila nyumba kisha anawalipisha hela kadhaa kwaajili ya huduma hiyo. Huu ni mwaka wa tatu tangu nimeanza kumuona akizoa takataka na sasa hivi ana maduka yake yapo kimara na ubungo pia ameongeza idadi ya vijana sasa wapo wanne. Kuna mashirika mengi tu Tanzana yetu fanya kujitolea kuweza kupata mbinu mbalimbali na kuongeza uwezo wa kufikiri, unadhani kwa kukaa mtaani ukilalamika unamkomoa nani kama sio wewe mwenyewe? Wawekezaji wengi hupenda kuwekeza kwa mtu ambaye tayari ameshafanya kitu katika jamii, yaani kama ni biashara basi uwe umeianzisha na inaonekana ndio maana hata benki hawawezi kukupa mkopo kama huna biashara na ifikishe miezi sita ndio huamini umekomaa na unaelewa upepo wa biashara ndipo hukupa mtaji, hawawezi kukupa mtaji au mkopo na wakati kutwa upo mtaani unamwaga lawama tu

4) NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI
Hapa ni kuhusu kupata mtaji wa kufanya biashara yako ambapo wengi hushindwa kuwaconvince watu wao wa karibu ili waweze kuwapatia mitaji ya biashara zao. Iwapo huwezi kuwaconvince hao watu wa karibu wakupatie mtaji unadhani utaweza kumconvince mtu wa mbali akupatie mtaji? Nikupe mfano labda wewe ni mwanafunzi wa chuo na unawaza kufanya aina fulani ya biashara ambayo mtaji unaweza kuwa milioni moja au mbili, jenga mazoea na wanachuo wenzako. Mtu kukupa milioni moja ni jambo ambalo haliwezekani kamwe bali kukupa elfu moja inawezekana kabisa, mfano chuo chenu kina wanafunzi elfu mbili jitahidi kufanya kitu kitaalamu ambapo orodhesha majina yao na kozi wanazosoma na pembeni weka kiasi. Mfate mmoja mmoja akusaidie elfu moja moja bila shaka hawezi kukataa kutoa elfu moja, mpaka hapo watu elfu mbili kwa elfu moja moja huoni tayari una milioni mbili? Kama upo mtaani orodhesha majina ya wakazi wa mtaani kwako ambao unaona kabisa kukusaidia elfu moja inawezekana. Wafate kisha kila ukipewa unaiweka mahala mpaka hapo hujapata mtaji wa kuanzia biashara yako? Je tatizo ni huna mtaji au huna mbinu ya maana ya kukusongesha mbele? Kila kitu kinawezekana tatizo sisi tumelaza ubongo na kuishia kuona matatizo tu Zipo njia nyingi sana za kupata mtaji acha kumwaga lawama badala yake utumie muda huo kuwaza kwa kina na kuvumbua mbinu ambazo zitakukwamua kimaisha, epuka sana kuanza kwa kuwaza kuwa na mtaji mkubwa ambao ni ngumu kupata badala yake anza kwa biashara yenye mtaji mdogo na kupanda taratibu mpaka kufikia juu. Kumbuka hata roma haikujengwa kwa siku moja vivyo hivyo hakuna mafanikio yanayokuja kwa usiku mmoja ni lazima uhangaike na kuumiza akili yako zaidi. Asanteni sana kwa kusoma makala hii bila shaka imekupa mwanga wa kipi unachopaswa kukifanya kuweza kupiga hatua ya juu zaidi ya hiyo uliyopo hapo.

Imeandaliwa na
Mtenga Gerald
Mkurugenzi Mtendaji wa
TAECO LTD
taecoltd@yahoo.com, taecoltd@gmail.com, gmtenga@gmail.com www.taecoltd.webs.com
0713332606
Iko poa sana mkuu hii
 
mawazo yako bhna hao watu mia wa kukopa sh laki moja moja unawatoa wap em jarbu ww tuone
 
Tajiri mkubwa na mashuhuri duniani, Bwana Warren Buffet aliwahi kusisitiza kuwa, kama unataka kujenga mtaji kutoka kwenye akiba yako binafsi ni sharti ujitahidi kuacha tabia ya “kuweka akiba baada ya kutumia na badala yake utumie kile kinachobaki baada ya kutenga pesa ya akiba”. Katika maisha ya umilikaji pesa duniani, kuna makundi ya ina mbili.

Kundi la Kwanza ni la wale wanaoweka akiba ya kile kinachobaki baada ya wao kutumia na kundi la pili ni wale wanaoweka akiba kabla ya kutumia. Kwa mfumo wetu wa mapato na matumizi ya pesa, tunaona kuwa kundi la waweka akiba baada ya kutumia ni wengi sana na ndilo kundi la watu ambao ni walalamikaji juu ya ukosefu wa mitaji ya kufanyia biashara au shughuli nyingine za kiuchumi.

Katika ulimwengu wa biashara, mtaji ndilo suruhisho la uwekezaji wowote wenye tija. Hatahivyo, mtaji umekuwa ni adimu kuupata na umekuwa ni kikwazo namba moja cha watu wengi kushindwa kuwekeza na hatimaye kuwa wajasiriamali. Ili kuweza kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa mitaji, watu wengi wamezidi kuhamasishwa kujiweea akiba binafsi kidogo kidogo kutoka kwenye mapato wanayopata.

Lakini pamoja na kwamba njia hii ya akiba binafsi ni rahisi na ya uhakika, bado suala la kuweka akiba limekuwa gumu kutekelezeka. Sababu kubwa ya kushindwa kujiwekea akiba ni kwamba watu wengi tumejenga utamaduni wa “kutumia kwanza na akiba baadae”.

Ukweli ni kwamba, pindi tunapopata pesa, kitu cha kwanza kufanya ni kutumia kwanza kwa lengo la kumaliza eti shida zilizopo. Hapa kipaumbele kinakuwa ni kumaliza shida na siyo kuweka “akiba”. Uzoefu umeonyesha kuwa, ukipata pesa na ukaanza kutumia kabla ya kutenga akiba, inakuwa siyo rahisi kubakiza pesa yoyote kwasababu shida ni nyingi na mahitaji ya wakati huo ni mengi, ukilinganisha na kiasi cha pesa unachokuwa umepata.

Ukipata pesa na ukatumia kabla ya kutenga akiba, basi ujue umelipa watu wengine kwanza kabla ya kujilipa wewe. Utamaduni wa kulipa watu wengine kwanza pindi tupatapo pesa umezidi kukua siku hadi siku na tumeendela kuulithisha kwa watoto wetu. Pesa yoyote unayojilipa kwanza ndiyo hiyo hugeuka kuwa “akiba”. Tunahitaji kujenga utamaduni wa kujilipa kwanza kabla ya kufikiria kununua kitu chochote kile pindi tunapoingiza pesa mifukoni mwetu.[HASHTAG]#Kiranja[/HASHTAG]

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Wageni karibuni wote
Humundani kuna fursa moja ambayo ita wainua watu wengi.

Jiunge na ajira hii ya mtandaoni kwa manufa yako mwenyewe

1.ajira hi aitaji kipato wala elimu INA itaji muda na kifurushi cha intanet

2.malipo yake yana fanyika SAA yoyote ndani siku za kazi pale uta kapo hitaji ulipwe

3.ukijiunga ili uweze kupatiwa pesa zako itakubidi ufikishe dola 150$ kwamara yakwanza hi wana ifanya ili kujua kama upo serious kufanya kazi nao.ila ukisha to a kwa Mara ya kwanza baada yahapo itakua unalipwa kila unapo fikisha 5$ nakuendelea

3.na malipo yana fanyika kwenye account ya benki yoyote APA nchini kwetu

Ku pata dola 150$ ni rahisi itakuchukua SAA moja nanusu kwa kufanya kazi bila kusimama bila kusimama

Kazi yenyewe niku angalia ma tangazo yanayo wekwa kwenye tovuti apo chini ili kujiunga

Boyeza linki
Viewing payed advertising sites rpmoney.club - Welcome!
Unaweza ukawa shilikisha na wenzako

 
Kwanza naomba nitangulize salaam kwenu natumaini mu wazima wa afya...

Twende kwenye hoja.. Nimejaribu kutafakari,kuwaza na kuwazua mtu ukitaka kufanikiwa kimaisha ni lazima ujiajiri lasivyo utaishia kua masikini kama wastaafu wengine..

Kwanini nimesema hivyo Now days makampuni mengi yanatafuta sana ma cheap labor,yani wakuajiri na wakulipe ujira mdogo kulingana na hali ya uchumi ulivyo sasa..

Mfano vijana wengi tukiajiriwa tunaliwapwa sio zaidi ya 500,000 yani kwenye hiyo hyo laki tano.. Inatakiwa ule, usafiri, pango la nyumba, umeme,maji,uvae,bado kama ndugu na jamaa usaidie kidogo kama mnavyo jua familia za kiafrica.. Huwezi iacha familia yako na ndugu baadhi..

Ukija kufanya hesabu hapo huwezi save zaidi ya 50,000 kwa mwenzi inamaana hadi ufikishe 1,000,000 sio chini ya miaka miwili..Sana mimi kama kijana napenda sana kufanya biashara lakini tatizo lipo hapa..

Wapi nitapata mtaji ata kwa kukopa...naamini katika kulima na biashara sio kuajiriwa ni kupotezeana mda na kutufanya tuzidi kua masikini..

Wakuu kwa anayefahamu namna ya kupata mkopo nafuu kwa sisi vijana tusio na asset yeyote ile kama ardhi ama nyumba.. Naomba nisaidiwe hapa najua wajuvi wa mambo mpo mtatoa msaaada wenu..

Na mtaji ninao utaka ni wa (5,000,000) million tano
 
Kuna jamaa alinipaga mbinu japo sijawahi ifanya hila nahisi ina msaada anaitwa ONTARIO ni member wa humu jf.

Yeye jamaa anadai kuna kitu kinaitwa FOREX yaani foreighn exchange kikimaanisha kubadilisha pesa kimtandao

Yaani wewe unatafuta mentor ambaye atakusaidia kufanya hiyo miamala nisawa unavyofanya biashara ya kuuza dollar kama unaelewa hicho kitu.

Mtafute huyo jamaa kwa msaada zaidi hutakuja kulialia tena huku utakuwa unatunyasia maji tu huko barabarani.
 
Back
Top Bottom