Njia rahisi ya kumaliza panya

Jamani hiyo dawa sidhani kama itafanya kazi kwa panya waliopo nyumbani kwangu.
Nimeshawapa kila aina ya sumu lakini hawafi.
imefikia kipindi wananacheza hadi miguuni kwa wageni wangu tena bila uoga.
Wale panya ni kama watu aisee. sometimes huwa wanatembea kwa miguu miwili kama binadamu yaani.
 
sure! ila paka nae ana kero zake kama we si mtu wa mambo ya pet

hapo kwenye red naamini sio paka jimmy wa JF!!! tehe tehe tehe!!

kama unaogopa saga vidonge vya dawa ya binadamu phenobarbitone vingivingi tu, maana dawa hii binadamu akinywa humletea usingizi sasa kwa panya yaweza kuwa kwake a letghal dose au kumlevya na kuwa zezeta, asubuhi utawakuta wamelewa au wamekufa kabisa
 
Mimi nawashauri badala ya sumu aliyoitaja changanya na dawa ya binadamu ya mifupa (indocid) sina uhakika kama ndio inavyoandikwa ila ndio inavyotamkwa. Nawashauri hili hasa wenye watoto, huwezi kujua siku ya bahati mbaya. Kwa kuhepusha hilo bora kutumia dawa ya binadamu kwani madhara yake hayatakuwa makubwa kama mtoto kwa bahati mbaya akilamba. Matokeo ni mazuri kama kutumia sumu tu, ila hawatakauka, hivyo ukiwaacha mpaka wafe watakunukia ndani. Ili wasinuke ndani ukishaweka usiku asubuhi ujaribu kuwasaka utakuta hawawezi kutembea, basi unawachukua na kuwaulia nje na ukipenda unaweza kuwa rafiki wa kunguru.
Mkuu, nauunga mkono,miguu n.k. Hiyo dawa ni KIBOKO kwa panya. Niliwahi kuitumia. Panya waliisha wote hata aliyekuwa anaogopesha paka. Angalizo unapowawekea kwenye mabaki ya chakula, hakikisha hawatapata access ya kunywa maji.
 
Pamoja na yote hayo pia mjaribu kupunguza makorokoro nadani ya nyumba. kama una ngu usizozivaa gawia wanaohitaji. Vyombo usivyotumia gawia wanaohitaji nk. mazingira ya ovyo ovyo huchangia mazalio ya panya. samahani kwa yeyote nitakaye mkwaza kwa maoni yangu
 
Nna panya ameshindikana ni mpevu kwelix2 ana kg kama 1 hivi,nimeweka dawa kali lakini wapi! Ila ntajaribu mkuu dawa yako ila ikishindikana naenda kuchukua mzigo gongo la mboto si yapo yamezagaa tuu waungwana?

kaka huyo panya kweli yafaa umtengue kwa bomu la tani 100.tofauti na hapo itafikia siku atakuwa hakuogopi hata wewe. Kama kunguru wa dar ambao hawaogopi watu kiasi cha kunyakua hata kofia kichwani pa mtu.
 
dawa ya kuua mende nunua vidonge vya ngao (vile vinavyotumika kwenye vyandarua). Uweke kwenye maji kama maelekezo yaliyopo, halafu hayo maji unyunyuzie kwenye sakafu au maeneo mende wanapopita ni vizuri ufanye usiku wakati unaenda kulala na madirisha ufungue ili upate hewa safi, pia mikono yako uvae gloves ipo kwenye pakiti utayonunua, kesho yake asubuh mama apige deki kama kawaida. Mende wataokatiza hapo lazima wafe hata wiki ikipita watakuwa wanakufa
...Wakuu yaelekea haya matatizo ya hawa wadudu ni kero sana. Mimi nasumbuliwa na mchwa nyumbani kwangu nimeshafanya fumigation 4 times lakini baada ya miezi michache wanarudi. Nilimchukua jamaa mmoja yuko makumbusho pale ni msukuma anadai ni mtaalamu wa kutoa mchwa ana dawa za kisukuma imeshindikana. Kwa kweli wananiharibia nyumba kwa kasi ya kutisha...Msaada please!!
 
<br />

duuh mkuu hii imeniacha hoi! Mchwa analetwa na nini tena kwenye nyumba hizo?
 
...Dah! hata mimi sijui jamaa yangu. ingekuwa ni mende ningesema wanavutiwa na uchafu sasa hawa mchwa sina maelezo kama unafahamu mbinu ya ukweli kuwaangamiza sema nidese chap chap kwa kweli hali ni mbaya.
 
dawa ya kuua mende nunua vidonge vya ngao (vile vinavyotumika kwenye vyandarua). Uweke kwenye maji kama maelekezo yaliyopo, halafu hayo maji unyunyuzie kwenye sakafu au maeneo mende wanapopita ni vizuri ufanye usiku wakati unaenda kulala na madirisha ufungue ili upate hewa safi, pia mikono yako uvae gloves ipo kwenye pakiti utayonunua, kesho yake asubuh mama apige deki kama kawaida. Mende wataokatiza hapo lazima wafe hata wiki ikipita watakuwa wanakufa

Mimi nilishawahi kutumia Ngao lkn ya maji. Ni siku nyingi, sijui km ya siku hizi ni strong km ya wkt ule. Nililoweka mchele, nikaukausha, nikautwanga, kisha nikachanganya na Ngao ya maji kwa mategemeo kwamba mende wangekula huo mchanganyiko. Cha ajabu, mende walianza kupukutika kabla ya hata kuusogelea mchanganyiko!! Tena walijitoa wenyewe kutoka ktk maficho yao! Hili lilinishangaza sana!! Atakayejaribu akumbuke kufunika vyombo vyenye maji na chakula.
 
Kuna wachina wamemuuzia waifu lipira linamiguu kama ng'e wakasema ulipake mchuzi panya aking'ata ananata lakini wapi!... ila inaonekana panya wanaliogopa hilo pira maana sijawaona tangu linunuliwe K'Koo sh 500 tu.

hahahaha hahahaha unajua mi nilivo yaona yale mapira yamezagaa kariakoo wala sikujua kazi yake hasa, sasa siku moja ma hasband kaja nalo nlicheka sana ila huwezi amin as u said panya walipotea kabisa mi nahisi wanaliogopa
 
Kuna wachina wamemuuzia waifu lipira linamiguu kama ng'e wakasema ulipake mchuzi panya aking'ata ananata lakini wapi!... ila inaonekana panya wanaliogopa hilo pira maana sijawaona tangu linunuliwe K'Koo sh 500 tu.

Bado yapo haya?
 
dawa ya kuua mende nunua vidonge vya ngao (vile vinavyotumika kwenye vyandarua). Uweke kwenye maji kama maelekezo yaliyopo, halafu hayo maji unyunyuzie kwenye sakafu au maeneo mende wanapopita ni vizuri ufanye usiku wakati unaenda kulala na madirisha ufungue ili upate hewa safi, pia mikono yako uvae gloves ipo kwenye pakiti utayonunua, kesho yake asubuh mama apige deki kama kawaida. Mende wataokatiza hapo lazima wafe hata wiki ikipita watakuwa wanakufa
Mkuu hiyo Ngao naitafuta ile mbaya ntaipata wapi kwa urahisi?
 
Back
Top Bottom