micro endoscope
Member
- Apr 30, 2020
- 60
- 95
Unaweza ukampata sema akiingia ndani mkaishi pamoja akaanza kubadilika pole pole, hasa kimaadili, muonekanao was kimwili nk.
Jitahidi tu kumuomba mungu akupe mke mwema mengine ni ya kupita tu, na wala hizo sifa ambazo umezitaja so za maana sana.
NB:
WATAKUJA WENYEWE KUELEZA.
TUWAACHIE WANAWAKE UWANJA WAO NAO WAJITETEE KAMA KWELI SIFA HIZO WANAZO?
Sent using Jamii Forums mobile app
Jitahidi tu kumuomba mungu akupe mke mwema mengine ni ya kupita tu, na wala hizo sifa ambazo umezitaja so za maana sana.
NB:
WATAKUJA WENYEWE KUELEZA.
TUWAACHIE WANAWAKE UWANJA WAO NAO WAJITETEE KAMA KWELI SIFA HIZO WANAZO?
Habari wakuu,
Ni jumamosi tulivu bila taarifa mpya ya Visa vya Corona. Tunazidi kuondoa hofu ya ugonjwa huu hata barakoa hatubadilishi tena.
Niende moja kwa moja kwenye Swali, Hivi ni njia gani nyepesi ya kupata mke mwema? Yaani yule mke wa sogea tukae ambaye anaamini mume ana nafasi kubwa sana kuliko wazazi kwenye ndoa.
Mke mnyenyekevu na mchamungu, asiyeyumbishwa na wachungaji wajasiriamali, asiyejipendekeza kwa mabosi zake, yaani mke asiye na tamaa.
Wapi wanapatikana kwa urahisi?
Mke asiyejua club, hajawahi kudanga, haigizi maisha
Mke mwenye bidii ya kazi na roho nyeupe, amejaa upendo kwa watu wote.
Mke mkarimu, hajui tusi wala kilevi, ana sura ya kike na mwili wa kike, mke kijana hajatumia Ujana vibaya wala hajafika 30
Mke anayekula kwa kiasi na mazoezi kidogo, hana mafuta ya hovyo wala manyama uzembe
Mke anayejua maisha ni kutafuta, tunaanzia popote
Mke ambaye dunia haijamuacha nyuma anajua ongoing issues ña ana degree ya kweli sio chura pekee
Wapi anapatikana kwa urahisi?
Kama yupo mwambie vijana tunamtafuta, kama Kuna sehemu wanapatikana mtuambie tukawachukue.
Nawasilisha swali langu, samahani kwa uandishi mbaya ni madhara ya kusoma sayansi nchini
Sent using Jamii Forums mobile app