Njia mpya ya kulipia NHC Bills bado tatizo

ngonyango

JF-Expert Member
Aug 7, 2017
1,883
1,599
NHC kwenye Bill payment system yenu boresheni yafuatayo;
1.Mngeweka kwenye website yenu njia mpya ya kulipia hizo bills zenu kupitia control numbers... wengine tupo maporini lakini ni wapangaji wenu...naangalia hapa kwenye website yenu hata helpdesk page haifunguki nimeshindwa kupata msaada ingawa nataka kulipa...sawa hata ukinipa control number ,nikitaka kulipa kupitia MPesa napitia menu option gani,baada ya kuchagua 'Lipa kwa Mpesa?' 3,4 au 5?
2.Halafu hizo control numbers lazima tuzipate kwenye hizo bills zenu za makaratasi mpaka milele? kwa nini msifanye kama DAWASA ambao wanatutumia sms kila mwezi inayoonyesha akaunti namba,kiasi unachodaiwa ,kwa kipindi gani... na control numbers zetu ambazo hazibadiliki?mbona mnafanya kiujima sana?Mbaya zaidi naona zinabadilika kila mwezi au itakuwa moja?
Nawasilisha , jiwe gizani
 
Back
Top Bottom