Njelu Kasaka ajiunga na CHADEMA

Haya ndio ya kukumbuka shuka wakati kumekucha, huyu Mzee angehama wakati ule wa G55 ningemkubali sana, lakini alipohongwa Unaibu Waziri akaufyata nikajua ni wale wale!
 
Mzee Njelu Kasaka amegeuka msaka tonge tu, hana lolote.

Mwanzo alitoka CCM akaenda CUF, akarudi tena CCM, sasa ameenda Chadema!

Chadema mpokeeni lkn wekeni akilini kuwa Mzee Kasaka anasaka Ubunge tu, sio kingine.

Vv
 
Kwanza alivyopigika kuanzia kisiasa na kila kitu hata huo uongozi hafai kabisa kwani akiwa mbunge wa chunya alifanya nini.
 
Huyu mzee ni bonge la Jembe, ni mmoja kati ya watu wa ccm niliokuwa nikiwakubali sana.

Ni mzee anayejitambua sana, hairuhusu akili yake ikatumika kwa maslahi ya watu wengine. Jamaa anajitambua sana. Ni mmoja kati ya wabunge waliounda kundi la G55 akiwemo Tuntememeke Sanga. Nilikiwa nikisoma sana Makala zake kwenye Gazeti la Raia Mwema na kwa kweli zilikuwa zinavutia sana.

Kila anayejitambua anaondoka ccm yanabaki majingajinga tu..!!!

BACK TANGANYIKA
 
Mzee Njelu Kasaka amegeuka msaka tonge tu, hana lolote.

Mwanzo alitoka CCM akaenda CUF, akarudi tena CCM, sasa ameenda Chadema!

Chadema mpokeeni lkn wekeni akilini kuwa Mzee Kasaka anasaka Ubunge tu, sio kingine.

Vv

What about Steven Wassira? alitoka CCM akaenda Chama kingine na akarudi. Yeye je?
 
Huyo ameanza kupigania tanganyika muda mrefu. ni mpambanaji na mzalendo wa kweli.
 

ni kweli mkuu chadema wamepata mtu makini. ni sawa na yule arcado ntagazwa yuko vizuri sana yule mzee. nawashauri cdm hawa wanaohamia cdm na waliwahi kuwa mawaziri wawatumie vizur ili kupata siri na madhaifu mengi yanayofanyika kwenye idara za serikali.
 
Yule ambaye aluhamia CUF msimu wa uchaguzi uliopita akikua ni nani?
 
No mwaka 2005 kasaka alishindwa ktk kura za maoni na mwambalaswa hivyo akahamia cuf lakin 2006 ktk mkutano wa ccm ulioongozwa nakikwete njelu alirud tena ccm 2010 njelu aligombea tena akashindwa ktk kura za maon akaendelea kuwamwanaccm muaminfu na mwaka huu kahama unajua kwann? huyu anaulilia ubunge san alioushika tangu mwaka 1990-2005 mwaka huu kweny ccm ameon hanauwezekan wakupita ndo mana kahamia cdm iliagombee ko sifa yake kubwa nikuw kila uchaguz unapofik na akion hakun uwezekan wakupitishw na ccm huama chama mwaka 2006alipokuw anarud ccm alitubu ktk mkutano ule kuwa yy ni mwanampotevu ko asamehewe ni baada ya cuf kushindw kumsimamisha kuw mgombea wao wa ubunge wasifu wa njeru aliwai kuwa mkuu wa mkoa tabora pia aliwai kuw naibu wazir wa afya
 

Njelu namshauri asigombee kwani hatopata historia Yake inamhukumu na kama UKAWA mtamsimamisha huyo Mzee juone jimbo hamtalipata kamww
 
Teeeeh ,teeeeh,jitekenye mwenyewe na kujichekesha watu wanasonga kuelekea magogoni,mtajijua mwaka huu wategemezi wa lumumba.

Ndoto za mchana nazo ni ndoto pia.
 
Huyo mzee anatabia ya kuhamahama vyama. Kwa hiyo angaliwe kwa makini sana.

Hili ndio neno la muhimu. Asije akawa na life span km ya mbu akiwa chadema.
CDM NI MPANGO WA MUNGU
 
Huyo ni kacherooo aliyekomaa..mngejua msingekuja kushabikia hapa kama watoto...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…