Njelu Kasaka ajiunga na CHADEMA

Njelu Kasaka ajiunga na CHADEMA

Safari hii magamba hamtapona mtasambaratika na kutawanyika kwa njia saba, na ndipo andiko litatimia
 
Ukombozi umeshafika, watanzania kuweni tayari wa mabadiliko kwa mara ya kwanza tangu uhuru wa taifa.

Kwa hisani ya JF, wajue wabunge 55 wa kundi lililodai Tanganyika mwaka 1993.

Wabunge 55 waliofahamika kama G55, wakiongozwa na mtoa hoja, Njelu Kasaka, waliiunga mkono hoja hiyo. Baadaye wakaongezeka wengine kumi na kuifanya idadi yao kuwa 65 hadi kufikia Julai 22, 1994.

Wabunge wengine waliounga mkono na majimbo yao ya wakati huo yakiwa kwenye mabano ni;
Mateo Tluway Qaresi (Babati),
Jenerali Twaha Khalfani Ulimwengu (Taifa/Jumuiya ya Vijana),
Mbwete Polile Hombee (Mbeya Vijijini),
marehemu John Byeitima (Karagwe),
Chediel Yohane Mgonja (same),
Japhet Sichona (Mbozi),
Benedict Losurutia (Kiteto ),
Dk. Mganga Kipuyo (Arumeru Magharibi),
Stanley Kinuno (Nyang’hwale),
Dk. Aaron Chiduo (Gairo),
Edward Oyombe Ayila (Rorya)
Shashu Lugeye (Solwa).


Wengine walikuwa ni
John Mwanga (Moshi Mjini),
Dk. Deogratius Mwita (Serengeti),
Abel Mwanga (Musoma Mjini),
Juma Jamaldin Akukweti (Tunduru),
Patrick Silvanus Qorro (Karatu),
Steven Mwaduma (Iringa Mashariki),
Dk. Ndembwela Ngunangwa (Njombe Kusini),
Richard Koillah (Ngorongoro),
Ahmed A. Mpakani (Iringa Magharibi),
Paschal K. Mabiti (Mwanza),
Luteni Lepilal Ole Moloimet (Monduli),
Lumuli Alipipi Kasyupa (Kyela),
Profesa Aaron Masawe (Hai)
Arcado Ntagazwa (Kibondo).


Katika kundi hilo walikuwemo pia
Phineas Nnko (Arumeru Mashariki),
Paschal Degera (Kondoa Kusini),
Mussa Nkhangaa (Singida Mjini),
Halimenshi Kahema Mayonga (Kigoma Kaskazini),
Said Abdallah Nakuwa (Lindi Mjini), na
Mosi Tambwe (Taifa/Wanawake).

Nimesoma majina ya hawa waheshimiwa nikasikia mwili wote UKINISISIMKA!

Nameomba Mungu kabla sijafa nione Serikali ya Tanganyika.
 
Safari hii magamba hamtapona mtasambaratika na kutawanyika kwa njia saba, na ndipo andiko litatimia
 
Duh...kama wazee hawa wanakikimbia chama cha majambazi nashangaa vijana wenye nguvu zao wanasubiri nini.....

Njaa ndio zinawabakisha humo watakula waapi kuna wengine tunafanya kazi na kutoa jasho ili tupate mlo wa kesho lakini kuna wenzetu, majungu, fitna , uongo ndio shibe yao ya kila siku ukistaajabu ya MUSA utayaona ya Firaoni.
 
Huyo ni mpinzani toka kitambo hivyo amerudi nyumbani kwake. Hana madhara huyo ni kopo aende huko amsubiri chizi mwenye kopo amfuate.

Teh teh teee bakini na mafisadi yenu manake wengine wana hofu ya Mungu wasijekufa na dhambi ya dhulma bure .
 
Alishahama lini? Weka rekodi sawa tusikuone wa hovyo

Mkuu TAWA Ilikuwa ni mwaka 2000 baada ya kushindwa katika kura maoni za ubunge ndani ya CCM na alihamia CUF ambako haikumchukua muda mrefu akarejea CCM a.k.a UGAMBANI.
 
Last edited by a moderator:
Huyu mzee hana lolote ni msaka madaraka tu! Siyo kwamba aliwahi kuvua gamba halafu baadaye akarudi tena? Au nimesahau? Huyu anasaka kuteuliwa kugombea ubunge jimbo la Lupa, nawaomba UKAWA wamweke pembeni tuone uvumilivu wake? Sina imani naye huyu!!
 
Huyu Mzee anahangaika alihamia CUF kisha akarudi CCM tena amehama CCM kwenda. CHDEMA
 
Alishaona hapiti akaona bora ahamie CHADEMA ni sawa sawa leo hii Steven Gerald anavyohamia LA Galaxy kwa kukosa # kwenye team yake. CHADEMA Walivyo mazuzu wataona wamepatia hahaha kumbe huyo ni Gunia la Sukari baharini.
 
Wacha longolongo zako wewe mbona umeshondwa kupanga mipango mizuri na ukatoka na ushauri mzuri kwa lowasa hasipoteze ela zake kwenye kutangaza nia na badala yake azipeleke vituo vya afya kununulia dawa ili kuokoa maisha ya mama na watoto ?
Hio post mbona sijahawahi i post humu? Na kwakweli na shangaa kuona umeni quote humu wakati haina relevance yeyote na Topic wala kinachokua discussed humu. Imeingieje?
 
Back
Top Bottom