Njelu Kasaka ajiunga na CHADEMA

Njelu Kasaka ajiunga na CHADEMA

Dona Kantri

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2012
Posts
346
Reaction score
115
Ni Njelu Kasaka mbunge wa zamani wa jimbo la Lupa wilayani Chunya mkoa wa Mbeya, leo ametangaza kukihama chama cha Mapinduzi na kujiunga na CHADEMA.

Akiongea na wananchi wa chunya leo, mwenyekiti wa chadema mkoa wa mbeya amethibitisha hayo.

"Chunya leo tumekuja kufanya kazi kuu mbili kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na kumpokea rasmi mzee wetu Njelu Kasaka"

Katika mkutano huo wa hadhara pia Katibu mtendaji wa TLP alijiunga na chadema na kukili kuwa TLP imebaki Vunjo tu ambako nako itapotea baada ya miezi mitatu...!

Mkutano umefanyika Chunya mjini umeongozwa na mwenyekiti wa mkoa na mzee wa upako!
 
Very gud! Gud job. Njelu kasaka very nyce.
 
Duh,kazi ipo mwaka huu,Ccm watabaki mafisadi na wasiojitambua.Nasikia hata mzee Warioba yuko njiani kuingia kwenye uzima huo
 
Huyo ni mpinzani toka kitambo hivyo amerudi nyumbani kwake. Hana madhara huyo ni kopo aende huko amsubiri chizi mwenye kopo amfuate.
 
Wengi wa waliotia nia wakikatwa majina yao watatimkia UKAWA ... soon CCM itaporomoka kama ambavyo vyama vingine vya Ukombozi vilivyoporomoka na kupotea ...
 
waziri wa mkapa au waziri kipindi cha awamu ya mkapa mbona hujui kuandika hata kichwa cha habari mleta uzi
 
Back
Top Bottom