Ami,
Kuna vijarida vyenu vilivyojaa udini kama Annur, na radio zenu za kidini Radio Heri nadhani wasomaji wake akili zao zimetayarishwa kupenda mada kama zako. Sio hapa please.
Fahamu kuwa Sudan ni nchi iko vitani tangu mwaka 1983. Sababu ya vita ni kuwa watu wa Sudan Kusini ambao si waarabu na ambao hawahitaji kuwa waarabu au Waislamu wanalazimishwa na serikali ya kiislamu ya Sudan kubeba Uarabu na Uislamu. Watu karibu million 4 wamekufa kwa vita hiyo na walio wengi kati ya hao ni wa Kusini ndio waliokufa.
Fahamu pia kuwa kuna watu wapatao million 4 wa Sudan ya Kusini wamekimbia makazi yao kwa hofu ya majeshi ya Serikali, na pia raia 500,000 wa Sudani Kusini ni wakimbizi nje ya Sudan.
Sudan ina mchanganyiko mkubwa wa makabila na tamaduni. Wasudan hao ni waumini wa dini mbalimbali pia. Ni wazi Waislamu ndio wengi asilimia 65, wakifuatiwa na wakristu asilimia 15 na wanaofuata dini za jadi ni takriban 20%. Kitamaduni 52% wanafuata utamaduni wa kiafrika, japo wengine ni Waislamu (kama Darfur), wengine ni Wakristo wa Kusini na Wafuatao dini za jadi. Wanaofuata utamaduni wa Kiarabu moja kwa moja ni kama asilimia 39, na waliobaki wanachanganya.
Makabila yaliyopo Sudan kama nilivyosema ni mchanganyiko mkubwa sana. Kaskazini kuna makabila ya waafrika (weusi) ambao ni waislamu: Wanubi na Wabeja; na magharibi wako Wafur (Watu wa Darfur) ambao nao ni Waislamu pia. Hawa wa Darfur pamoja na kwamba ni Waislamu wanabaguliwa na Waislamu wanaojipa Uarabu pia. Kusini walio wengi ni Wakristu na wanaofuata dini za jadi. Wako Wadinka ambao ni 10% ya Wasudan wote, na kwa Kusini ni 40% ya WaSudan wa Kusini, wapo pia wanuer, Wachollo, Wamurle, Wamandari na Wabaka; pamoja na makabila mengi madogo madogo.
Ni kweli Sudan Kusini kuna mafuta ambayo yanaiingizia Serikali $2 millioni kwa siku, lakini $1million kwa siku zinatumika kwa jeshi tu.
Kwa maoni yangu, Serikali yoyote ambayo haiwezi kukubali tofauti za watu na kujaribu kuwaunganisha kwa kuwafanya waarabu na waislamu kama huko Sudan haitafanikiwa kumaliza umwagaji wa damu. Na kama hawawezi kupokea hizo tofauti, basi mawazo ya kujigawa lazima yawepo, na ni kwa kunusuru maisha ya watu, ambayo yana thamani sana bila kujali rangi wala dini zao.