EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
Mapema mwakani kura ya maoni inatarajiwa kupigwa nchini Sudan kuamua mustakbali wa eneo la kusini la nchi hiyo.
Wakati dunia nzima ikipigania kuwa wamoja na maeneo yenye kujaribu kujitenga kama huko Comoro nguvu zikitumika kupinga kujitenga,mambo ni tofauti huko Sudan.
Baadhi ya uongo wa mataifa ya magharibi kuhalalisha kujitenga eneo la kusini lenye utajiri mkubwa wa mafuta ni eti waarabu wanawabagua waafrika.
Hapo chini ni raisi wa Sudan general Omar Al bashir akionesha upanga wake kama silaha ya kupambana na wenye kuitakia mabaya Sudan,akiwa amezungukwa na wasaidizi na walinzi wake.
Kwanza kabisa unajichanganya sana kwenye hoja yako. Kwanza unaanza kwa kusema "Mapema mwakani kura ya maoni inatarajiwa kupigwa nchini Sudan kuamua mustakbali wa eneo la kusini la nchi hiyo." Then, unasema "Baadhi ya uongo wa mataifa ya magharibi kuhalalisha kujitenga eneo la kusini..." Kama kujitenga kumeshahalalishwa, hiyo kura ya maoni inayotarajiwa kupigwa nchini Sundan ni ya nini tena? Sina uhakika una elimu ya kiasi gani, but surely usirukie mambo usiyofahamu. Inaonyesha kabisa hufahamu kabisa historia mgogoro wa kusini mwa Sudan. Inaonekana hujui kabisa ni jinsi gani mataifa ya magharibi yameisadia Sudan kijeshi kuhusiana na huo mgogoro. Huu mgogoro haujaanza juzi na hautaisha kesho.
Huu mgogoro inabidi uangaliwe zaidi kihistoria na sio kidini. Ni vigumu sana kuijua historia ya kusini mwa sudan ukilinganisha na ile ya kaskazini. Wanahistoria wanasema inaonekana kama upande wa kusini ulikuwa na variety of semi-nomadic tribes. Kwenye karne ya 16 haya makabila, yaliyokuwa yanajulikana kama Funj yaliungana na Wanubia na kuanzisha Kingdom ya Sennar. Baada ya hapo masultani wa Funj waliconvert to islam na hapo ndio hii sehemu ya kusini ilipoanza kuwa entrenched. Wakati huo huo, Sultani wa Darfur alijitokeza upande wa mashariki mwa sudan, na kati yao Taqali alinzisha nchi ya Nuba Hills. Wakati huo, uchumi wa sudan ulikuwa feudalim ambapo watumwa wengi walikuwa wakiwasaidia Funj ruling class. Kwa hiyo biashara ya utumwa sudan haijanza leo.
Baada ya Berlin Conference (1882), Belgium ilichukua sehemu ya kusini mwa sudan na kuwa sehemu ya Belgian Congo. Waingereza walichukuwa kaskazini mwa sudan. Hata hivyo mwaka 1886, makubaliano kati ya Belgium na Uingereza yalifanya sehemu ya kusini ichukuliwe na Uingereza baada ya kifo cha King Léopold II in 1910.
Kuanzia hapo Waingereza walitawala kaskazini na kusini mwa Sudan tofauti na ninafikiri ndio hapo huu mgogoro wa sasa uliponzia. Upande wa kusini ulilinganishwa na sehemu nyingine za makoloni ya kiingereza kama ambayo yalikuwa Kenya, Tanganyika na Uganda wakati Upande wa kaskazini ulikuwa ulilinganishwa zaidi na nchi zinazoengea kiarabu kama Misri. Waarabu wa kaskazini walizuiwa kuchukua nafasi zozote za uongozi upande wa kusini uliokuwa dominated na wakatoliki. Pia Waingereza walikataza biashara kufanyanyika kati ya sehemu hizi mbili.
Hata hivyo Waingereza walishidwa kuhimili pressure toka upande wa kaskazini na mnamo mwaka 1946 ilibidi wakubali azimio la upande wa kaskazini on the condition kuwa wataform federal system of governance. Hata hivyo Lugha ya Kiarabu ilifanywa kama lugha ya utawala kusini na watu wa kaskazini walianza kuchukua nafasi mbalimbali za uongozi upande wa kusini. Watu wa kusini ambao walikuwa wamefundishwa zaidi lugha ya kiingereza hawakukubaliana na haya mabadiliko. Matokeo yake hawakuhusishwa kwenye serikali iliyoundwa na watu wa kaskazini. Baada ya uhuru, watu wa kaskazini walipewa mamlaka yote ya kumiliki na kutawala upande wa kusini. Hii ilisababisha mgogoro upande wa kusini.
Mwaka 1955 mgogoro ulikuwa mkubwa baada ya upande wa kaskazini kushindwa kutimiza makubaliano waliokubaliana na uongozi wa kikoloni kuwa wangeanzisha federal system. Miaka 17 iliyofuata ilikuwa ni vita tuu, na viongozi wa upande wa kusini wakaanza kudai regional autonomy au kujitenga kabisa.
Pia ikumbukwe kuwa moja ya sababu zilizosababisha vita kuu ya pili ya dunia ni natural resources za Sudan hasa zilizoko upande wa kusini. Pia kusini ndiko kuliko na tributaries nyingi za mto Nile na heavier precipitation. Upande wa kusini pia una access kubwa ya maji na ina rutuba zaidi. Upande wa kaskazini umepakana zaidi na jangwa. Hata hivyo, upande wa kaskazini ndio unaomiliki natural resources zote za kusini. Nia ya upande wa kaskazini ni kuendelea kumiliki vyanzo hivi vya uchumi wakati nia ya upande wa kusini ni kuwa na mkono kwenye hizi natural resources. Hili pia zimechangia sana kuzuka kwa hii vita. Kinachonishangaza ni kwamba pia kuna vita kati ya Nuer and Dinka ambao wote wanatoka upande wa kusini.
Mwaka 1983, rais Nimeiry alitaka kuibadilisha Sudan iwe nchi ya Kiislamu na kuigawa nchi kwenye sehemu tatu ambazo zingeongozwa na Sheria za Kiislamu. Hii ilikuwa issue sana hata miongoni mwa vikundi vya kiislamu. Kama mnakumbuka hii ndio iliyofanya Ansnar awekwe kwenye house of arrest. Mwaka 1984, Nimeiry alidecrare state of emergency kuhakikisha kuwa sheria za kiislamu zinatumika zaidi. Haki zote za kikatiba zilikuwa-suspended na sheria za kiislamu zilianza kutumika zaidi. Hii yenyewe iliongeza chachu kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe ukizingatia upande wa kusini walikuwa ni wakatoliki.
Jeshi la Sudan People's Liberation Army (SPLA) lilianzishwa mwaka 1983 na watu wa kusini kupambana na serikali ya kaskazini. Nia yao ilikuwa ni kuanzishwa kwa nchi mpya kusini mwa Sudan na kiongozi wa jeshi hili alikuwa John Garang. Nasikia alisoma Tanzania. Mwaka 1984, Nimeiry alitangaza kuisha kwa hali ya hatari. Pia aliwahakikia wasio kuwa waislamu kuwa haki zao zitaheshimiwa japokuwa watu wa kusini hawakumwamini.
Pia cold war imechangia sana kwenye hii vita. Baada ya huru jeshi la sudan liliendelea kufundishwa na kupata zana za kijeshi to Uingereza. Hata hivyo, Ungereza, Marekani na Ujerumani Mashariki, walikata mawasiliano mwaka 1967 baada ya ile vita kali ya siku sita huko sudan. Kati ya mwaka 1968 hadi 1972 Urusi na nchi nyingine za COMECON waliuza silaha nyingi sana Sudan. Pia walitoa training na supports za kijeshi. Urusi iliendelea kuisaidia Sudan Kijeshi mpaka mwaka 1977, pale Sudan ilipofuta mkataba baada ya Urusi kuunga mkono issues za Marxist nchini Ethiopia. Kuanzia hapo China ndio ilikuwa supplier mkubwa wa slaa Sudan, ikisaidiwa na Misri. Hata hivyo katikati ya miaka ya 1970, Marekani ilianza tena kusambaza slaa Sudan ili ku-counteract kitendo cha Urusi kuunga mkono Ethiopia na Libya kwenye issues za Marxist. Hata hiyo, Marekani walikatisha uuzaji wa silaha sudan mwaka 1987 baada ya kuanza kwa vita ya pili Sudan. Ninachojaribu kuonyesha hapa nk kwamba, wakati mtoa hoja anadhani kuwa nchi za magharibi zinafagilia zaidi upande wa kusini ujitenge, pia zimesaidia sana upande wa kaskazini kijeshi. Silaha walizouza Sudan ndio zilizotumika kwa mauaji yaliofanyika huko sudan ya kusini.
Wafuatiliaji wa mambo wanaestimate that kati ya watu 200,000 toka sudan ya kusini wanawake kwa watoto wamechukuliwa kama watumwa na watu wa kaskazini. Watumwa hawa walikuwa wanapatikana kwa kuraid miji na vijiji. Karibia watu 4,000,0000 wameyakimbia makazi yao. Karibia watu 5,000,000 wameikimbia sudan kutokana na vita. Vita imesababisha watu washindwe kulima au kufanya biashara. Vita imesababisha njaa na utapiamlo mkubwa. Watu wa kusini wanaitwa "lost generation". Hawana elimu, ajira na afya bora ukilinganisha na watu wa kaskazini.
Kweli kuna umuhimu wa Waafrika kuungana kama kweli tunataka kupambana na nchi za magharibi. Lakini hatuwezi kulazimisha muungano kama watu wenyewe wanaona hauna manufaa kwao. Na hapa siongelei udini. Kwa mfano, sioni umuhimu wa kulazimisha Chechnya ambao wengi wao ni waislau iwe ndani Russia, kama Wachechnya wenyewe hawataki. Kama njia pekee ya kumaliza vita ya sudan ni sehemu hizo mbili kujitenga na kuwa nchi mbili then let it be so. Let the people exercise their right to self determination - their inherent right to choose how they want to be governed.
Leo, kama watu wa Zanzibar wakiamua kutaka kujitenga sidhani kama itakuwa busara kwa watu wa bara kuwarushia makombora eti kwa nia kudumisha muungano. Let people choose if they want to unite, but do not impose such unification on them especially if they think that they won't benefit from it. Kitu kinachonikera ni double standards zinazotumiwa na nchi za magharibi. Kama kweli wanaona kuna haki ya watu wa kusini mwa sudani kujitenga, vipi watu wa Western Sahara?