BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,831
- 287,782
Itawezekanaje kubadilisha mmiliki wa kampuni inayohusika na kashfa kubwa ya BOT!? 
Wakati Kikwete anaendelea na usanii ushahidi unaharibiwa na baada ya miezi sita tutaambiwa na hao waliopewa uwezo wa kuchunguza kashfa hii "Uchunguzi wetu umegundua kwamba makampuni yote yaliyotuhumiwa na kashfa ya BoT walifuata njia halali kujipatia mikopo toka BoT na hivyo hawana kesi ya kujibu."
Njama za kuharibu ushahidi BoT zaanza
na Charles Mullinda
Tanzania Daima
KASHFA ya ubadhirifu wa fedha za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imezidi kuchukua sura mpya baada ya kuvuja kwa taarifa za kuwepo mkakati mahsusi unaoandaliwa na baadhi wa viongozi na wafanyabiashara ili kuharibu ushahidi wa kampuni zilizotajwa kuhusika na uchotaji wa fedha hizo, kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).
Taarifa zilizoifikia Tanzania Daima Jumapili, zinaeleza kuwa kumekuwepo jitihada za makusudi zinazofanywa na baadhi ya viongozi kwa msaada wa wafanyabiashara za kuwanusuru baadhi ya wahusika wakuu wa baadhi ya kampuni kwa nia ya kuwahakikishia usalama wanasiasa kadhaa wazito.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, mipango hiyo inayofanywa kwa siri kubwa ilikuwa ikilenga kumtwisha mzigo huo mfanyabiashara mwingine ambaye kimsingi hakuhusika kwa njia yoyote katika sakata hilo la EPA.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa mtu waliyetaka kumtwisha mzigo huo ni mfanyabiashara mmoja maarufu mwenye asili ya Kiasia.
Taarifa hizo zinaitaja wazi moja ya kampuni zilizowekwa katika mpango huo kuwa ni Kagoda Agriculture Limited, ambayo tangu kuibuliwa kwa kashfa hiyo imekuwa ikielezwa kuwa ilisajiliwa na mmoja wa makada maarufu wa CCM mwenye ushawishi mkubwa serikalini akitumia majina ya watu wenye mahusiano naye ya karibu.
Aidha taarifa zaidi zilidai kwamba katika moja ya vikao vya hivi karibuni vya viongozi wa juu, mpango wa kumbadili mmiliki wa kampuni hiyo ulijadiliwa kwa kina na kuamuliwa kwamba kampuni hiyo ikabidhiwe kwa mfanyabiashara huyo Muasia, ambaye amekwisha kupewa maelekezo ya kupambana na maswali ya wajumbe wa kamati iliyoteuliwa na Rais Kikwete kuchunguza tuhuma za ubadhirifu katika kashfa ya EPA.
Habari zaidi ambazo gazeti hili limezipata kutoka kwa watu walio karibu na mfanyabiashara huyo, zilieleza kuwa juhudi hizo zimegonga mwamba hadi hivi sasa.
Zilisema ingawa mfanyabiashara huyo hajakubaliana na ombi hilo, bado jitihada za kumshawishi akubali kuwa mmiliki mpya wa moja ya kampuni hizo zinaendelea kwa kile kilichoelezwa kuwa ni jitihada za mwisho za kuwanusuru viongozi wa ngazi ya juu wanaohusishwa katika kashfa hiyo.
Pamoja na Kagoda, zipo kampuni nyingine mbili zinazodaiwa kuwa katika mpango huo, ambazo pia mfanyabiashara huyo anaombwa kuwa mmiliki wake.
Wachambuzi na wafuatiliaji wa mambo hapa nchini, wamelieleza gazeti hili kuwa madai hayo hayapaswi kupuuzwa kutokana na hali ya usiri ambayo imekuwa ikionyeshwa katika kashfa hii.
Wamesema hata hatua ya Rais Kikwete kutamka kwamba baadhi ya watu wanapotosha na kueneza habari za uvumi kuhusu kashfa hiyo, inaonyesha dhahiri kulenga kupinga madai kwamba, fedha za EPA ziliingizwa katika kampeni za CCM zilizompa ushindi yeye mwenyewe na chama hicho mwaka 2005.
Wakati hali ikiwa tete, mtu pekee anayeonekana kuwa na turufu ya mwisho na mwenye siri kubwa ni aliyekuwa Gavana wa BOT, Daudi Ballali ambaye taarifa za hivi karibuni zinaonyesha kuwa afya yake imekuwa ikiimarika.
Habari ambazo Tanzania Daima inazo zinaonyesha kuwa, Dk. Ballali amekuwa akifanya mawasiliano ya mara kwa mara na viongozi kadhaa wastaafu pamoja na baadhi ya wanasiasa ambao wameonyesha nia ya kumsaidia kujinasua katika tuhuma zinazomkabili.
Tanzania Daima ilithibitishiwa na mwanasiasa mmoja mwenye ushawishi hapa nchini kuwa anaendelea kuwasiliana na Dk. Ballali, na kwamba amekuwa akimpa baadhi ya dondoo za siri alizonazo kuhusu kashfa hiyo ili aone kama anaweza kuzifanyia kazi.
"Ninawasiliana naye, najua atakuja ingawa hajaniambia ni lini, lakini hivi sasa yuko nyumbani kwake Marekani, nina uhakika huo. Na hata kuchelewa kwake kurejea inawezekana kunatokana na vitisho, wakubwa wengi sasa wanaogopa.
"Unajua hata ukiangalia jinsi alivyoondoka utaona kuwa hakuwa na nia ya kukaa huko muda mrefu, aliondoka Jumanne, akiwa ameahidi kurudi Jumapili ya wiki hiyo hiyo aliyoondoka, lakini alipofika hospitali huko Marekani aliambiwa hawezi kurudi, hali yake ni mbaya, akalazwa, akafanyiwa upasuaji.
"Hata hivyo, dalili zinaonyesha kuwa ugonjwa wake haukuwa wa kawaida, kuna dalili kabisa kwamba alipewa...!" alisema mwanasiasa huyo ambaye jina lake tunalihifadhi.
Mwanasiasa mwingine aliyezungumza na gazeti hili kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu sakata hilo, ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kabwe Zitto, ambaye alisema kuwa kwa namna yoyote kashfa ya ufisadi wa fedha za BoT, haiwezi kutenganishwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Alisema Mkapa hawezi kukwepa kuifahamu kashfa hii, kwa sababu wakati inatokea alikuwa rais na kwamba Gavana wa Benki Kuu humpa taarifa rais kuhusu mambo yanavyoendelea katika benki hiyo.
"Kabla Dk. Ballali hajaja, Mkapa ndiye mtu pekee anayeweza kutoa msaada katika jambo hili, maamuzi yote ya gavana ni lazima 'ambrief' rais, hivyo Mkapa anajua.
"Kweli BoT ni taasisi huru, maamuzi mengi ya gavana yanachukuliwa ndani ya BoT, lakini fedha za EPA zilikuwa za serikali, hivyo inawezekana kabisa ni Mkapa aliyemuita na kumtaka afanye jambo fulani.
"Zaidi ya hapo ni kwamba, hatujamsikia Dk. Ballali akitoa ushahidi wake, Ernst & Young katika ukaguzi wao hawakumuhoji, uteuzi wake umetenguliwa, kuna gavana mpya lakini hajamkabidhi ofisi, hapo unaweza kuona kuwa kama Dk. Ballali atafika na kusema, mambo yanaweza kubadilika," alisema Zitto.
Akizungumza kuhusu kauli ya Rais Kikwete kuwa Watanzania wasiamini uvumi kuhusu kashfa hiyo, Zitto alisema Watanzania wana kila sababu ya kuendelea kuamini uvumi mpaka hapo ukweli utakapofahamika.
Kuhusu CCM kukanusha kumegewa fedha zilizochotwa EPA na kuzitumia katika kampeni zake za uchaguzi wa mwaka 2005, alisema njia pekee ya kukisafisha chama dhidi ya kuhusika katika ufisadi huo ni kufanyika kwa uchunguzi wa fedha kilichotumia wakati wa kampeni hizo.
"CCM wanajitetea kutotumia fedha za EPA, huo ni utetezi ambao hauingii akilini, hakuna njia nyingine zaidi ya kufanyika kwa uchunguzi huru, ili ijulikane walipata wapi fedha za kufanyia kampeni za namna ile," alisisitiza Zitto.
Taarifa za awali ambazo gazeti hili lilizipata siku chache baada ya kutangazwa kwa kampuni hizo, zilieleza kuwa, baadhi ya viongozi serikalini, na wafanyabiashara wakubwa waliotajwa kuhusika katika kashfa hiyo, walikuwa katika hali ya wasiwasi na woga mkuu.
Hali hiyo ilidaiwa kusababishwa na kupatikana kwa taarifa kwamba Dk. Ballali alikuwa akifanya mawasiliano na wanasheria kwa ajili ya kujilinda kisheria, ikiwa ni pamoja na kutoa siri nzito za vigogo waliohusika katika uchotaji wa fedha hizo.
Joto la kashfa hiyo lilizidi kupanda, baada ya kuelezwa kuwa Dk. Ballali alikuwa katika maandalizi ya kurejea nyumbani akiwa na vielelezo muhimu vya kashfa hiyo, vikiwemo vya maandishi, ambavyo alipanga kuvitumia kwa ajili ya kujisafisha.
Siku chache zilizopita, ilidaiwa kuwa kurejea kwa Dk. Ballali hakuna uhakika wa moja kwa moja, kwa sababu uraia wake una utata.