Njama za kuharibu ushahidi BoT zaanza

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Itawezekanaje kubadilisha mmiliki wa kampuni inayohusika na kashfa kubwa ya BOT!? :confused:

Wakati Kikwete anaendelea na usanii ushahidi unaharibiwa na baada ya miezi sita tutaambiwa na hao waliopewa uwezo wa kuchunguza kashfa hii "Uchunguzi wetu umegundua kwamba makampuni yote yaliyotuhumiwa na kashfa ya BoT walifuata njia halali kujipatia mikopo toka BoT na hivyo hawana kesi ya kujibu."


Njama za kuharibu ushahidi BoT zaanza

na Charles Mullinda
Tanzania Daima

KASHFA ya ubadhirifu wa fedha za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imezidi kuchukua sura mpya baada ya kuvuja kwa taarifa za kuwepo mkakati mahsusi unaoandaliwa na baadhi wa viongozi na wafanyabiashara ili kuharibu ushahidi wa kampuni zilizotajwa kuhusika na uchotaji wa fedha hizo, kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).
Taarifa zilizoifikia Tanzania Daima Jumapili, zinaeleza kuwa kumekuwepo jitihada za makusudi zinazofanywa na baadhi ya viongozi kwa msaada wa wafanyabiashara za kuwanusuru baadhi ya wahusika wakuu wa baadhi ya kampuni kwa nia ya kuwahakikishia usalama wanasiasa kadhaa wazito.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mipango hiyo inayofanywa kwa siri kubwa ilikuwa ikilenga kumtwisha mzigo huo mfanyabiashara mwingine ambaye kimsingi hakuhusika kwa njia yoyote katika sakata hilo la EPA.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa mtu waliyetaka kumtwisha mzigo huo ni mfanyabiashara mmoja maarufu mwenye asili ya Kiasia.

Taarifa hizo zinaitaja wazi moja ya kampuni zilizowekwa katika mpango huo kuwa ni Kagoda Agriculture Limited, ambayo tangu kuibuliwa kwa kashfa hiyo imekuwa ikielezwa kuwa ilisajiliwa na mmoja wa makada maarufu wa CCM mwenye ushawishi mkubwa serikalini akitumia majina ya watu wenye mahusiano naye ya karibu.

Aidha taarifa zaidi zilidai kwamba katika moja ya vikao vya hivi karibuni vya viongozi wa juu, mpango wa kumbadili mmiliki wa kampuni hiyo ulijadiliwa kwa kina na kuamuliwa kwamba kampuni hiyo ikabidhiwe kwa mfanyabiashara huyo Muasia, ambaye amekwisha kupewa maelekezo ya kupambana na maswali ya wajumbe wa kamati iliyoteuliwa na Rais Kikwete kuchunguza tuhuma za ubadhirifu katika kashfa ya EPA.

Habari zaidi ambazo gazeti hili limezipata kutoka kwa watu walio karibu na mfanyabiashara huyo, zilieleza kuwa juhudi hizo zimegonga mwamba hadi hivi sasa.

Zilisema ingawa mfanyabiashara huyo hajakubaliana na ombi hilo, bado jitihada za kumshawishi akubali kuwa mmiliki mpya wa moja ya kampuni hizo zinaendelea kwa kile kilichoelezwa kuwa ni jitihada za mwisho za kuwanusuru viongozi wa ngazi ya juu wanaohusishwa katika kashfa hiyo.

Pamoja na Kagoda, zipo kampuni nyingine mbili zinazodaiwa kuwa katika mpango huo, ambazo pia mfanyabiashara huyo anaombwa kuwa mmiliki wake.

Wachambuzi na wafuatiliaji wa mambo hapa nchini, wamelieleza gazeti hili kuwa madai hayo hayapaswi kupuuzwa kutokana na hali ya usiri ambayo imekuwa ikionyeshwa katika kashfa hii.

Wamesema hata hatua ya Rais Kikwete kutamka kwamba baadhi ya watu wanapotosha na kueneza habari za uvumi kuhusu kashfa hiyo, inaonyesha dhahiri kulenga kupinga madai kwamba, fedha za EPA ziliingizwa katika kampeni za CCM zilizompa ushindi yeye mwenyewe na chama hicho mwaka 2005.

Wakati hali ikiwa tete, mtu pekee anayeonekana kuwa na turufu ya mwisho na mwenye siri kubwa ni aliyekuwa Gavana wa BOT, Daudi Ballali ambaye taarifa za hivi karibuni zinaonyesha kuwa afya yake imekuwa ikiimarika.

Habari ambazo Tanzania Daima inazo zinaonyesha kuwa, Dk. Ballali amekuwa akifanya mawasiliano ya mara kwa mara na viongozi kadhaa wastaafu pamoja na baadhi ya wanasiasa ambao wameonyesha nia ya kumsaidia kujinasua katika tuhuma zinazomkabili.

Tanzania Daima ilithibitishiwa na mwanasiasa mmoja mwenye ushawishi hapa nchini kuwa anaendelea kuwasiliana na Dk. Ballali, na kwamba amekuwa akimpa baadhi ya dondoo za siri alizonazo kuhusu kashfa hiyo ili aone kama anaweza kuzifanyia kazi.

"Ninawasiliana naye, najua atakuja ingawa hajaniambia ni lini, lakini hivi sasa yuko nyumbani kwake Marekani, nina uhakika huo. Na hata kuchelewa kwake kurejea inawezekana kunatokana na vitisho, wakubwa wengi sasa wanaogopa.

"Unajua hata ukiangalia jinsi alivyoondoka utaona kuwa hakuwa na nia ya kukaa huko muda mrefu, aliondoka Jumanne, akiwa ameahidi kurudi Jumapili ya wiki hiyo hiyo aliyoondoka, lakini alipofika hospitali huko Marekani aliambiwa hawezi kurudi, hali yake ni mbaya, akalazwa, akafanyiwa upasuaji.

"Hata hivyo, dalili zinaonyesha kuwa ugonjwa wake haukuwa wa kawaida, kuna dalili kabisa kwamba alipewa...!" alisema mwanasiasa huyo ambaye jina lake tunalihifadhi.

Mwanasiasa mwingine aliyezungumza na gazeti hili kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu sakata hilo, ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kabwe Zitto, ambaye alisema kuwa kwa namna yoyote kashfa ya ufisadi wa fedha za BoT, haiwezi kutenganishwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa.

Alisema Mkapa hawezi kukwepa kuifahamu kashfa hii, kwa sababu wakati inatokea alikuwa rais na kwamba Gavana wa Benki Kuu humpa taarifa rais kuhusu mambo yanavyoendelea katika benki hiyo.

"Kabla Dk. Ballali hajaja, Mkapa ndiye mtu pekee anayeweza kutoa msaada katika jambo hili, maamuzi yote ya gavana ni lazima 'ambrief' rais, hivyo Mkapa anajua.

"Kweli BoT ni taasisi huru, maamuzi mengi ya gavana yanachukuliwa ndani ya BoT, lakini fedha za EPA zilikuwa za serikali, hivyo inawezekana kabisa ni Mkapa aliyemuita na kumtaka afanye jambo fulani.

"Zaidi ya hapo ni kwamba, hatujamsikia Dk. Ballali akitoa ushahidi wake, Ernst & Young katika ukaguzi wao hawakumuhoji, uteuzi wake umetenguliwa, kuna gavana mpya lakini hajamkabidhi ofisi, hapo unaweza kuona kuwa kama Dk. Ballali atafika na kusema, mambo yanaweza kubadilika," alisema Zitto.

Akizungumza kuhusu kauli ya Rais Kikwete kuwa Watanzania wasiamini uvumi kuhusu kashfa hiyo, Zitto alisema Watanzania wana kila sababu ya kuendelea kuamini uvumi mpaka hapo ukweli utakapofahamika.

Kuhusu CCM kukanusha kumegewa fedha zilizochotwa EPA na kuzitumia katika kampeni zake za uchaguzi wa mwaka 2005, alisema njia pekee ya kukisafisha chama dhidi ya kuhusika katika ufisadi huo ni kufanyika kwa uchunguzi wa fedha kilichotumia wakati wa kampeni hizo.

"CCM wanajitetea kutotumia fedha za EPA, huo ni utetezi ambao hauingii akilini, hakuna njia nyingine zaidi ya kufanyika kwa uchunguzi huru, ili ijulikane walipata wapi fedha za kufanyia kampeni za namna ile," alisisitiza Zitto.

Taarifa za awali ambazo gazeti hili lilizipata siku chache baada ya kutangazwa kwa kampuni hizo, zilieleza kuwa, baadhi ya viongozi serikalini, na wafanyabiashara wakubwa waliotajwa kuhusika katika kashfa hiyo, walikuwa katika hali ya wasiwasi na woga mkuu.

Hali hiyo ilidaiwa kusababishwa na kupatikana kwa taarifa kwamba Dk. Ballali alikuwa akifanya mawasiliano na wanasheria kwa ajili ya kujilinda kisheria, ikiwa ni pamoja na kutoa siri nzito za vigogo waliohusika katika uchotaji wa fedha hizo.

Joto la kashfa hiyo lilizidi kupanda, baada ya kuelezwa kuwa Dk. Ballali alikuwa katika maandalizi ya kurejea nyumbani akiwa na vielelezo muhimu vya kashfa hiyo, vikiwemo vya maandishi, ambavyo alipanga kuvitumia kwa ajili ya kujisafisha.

Siku chache zilizopita, ilidaiwa kuwa kurejea kwa Dk. Ballali hakuna uhakika wa moja kwa moja, kwa sababu uraia wake una utata.




 
Kipimo cha Utanzania wa JK ni hizi kashfa ,yeye anapiga danadana na watu wanafanya mambo ya kuimaliza yeye anasemaje ?Mwaka huu ni mzito sana lakini CCM inakaribia mwisho wake .
 
Hilo gazeti la Daima linachanganya habari za kweli na za uongo,za kufikilika na majungu,wana ushahidi gani kuwa kuna watu wamepanga kuhalibu ushahidi,au nia ni kuuza tu magazeti yao,wanaposikia wenzao wanafanya habari za uchunguzi uko ulaya hawamaanishi na majungu na kujitungia habari zisizo na ushahidi
 
Hilo gazeti la Daima linachanganya habari za kweli na za uongo,za kufikilika na majungu,wana ushahidi gani kuwa kuna watu wamepanga kuhalibu ushahidi,au nia ni kuuza tu magazeti yao,wanaposikia wenzao wanafanya habari za uchunguzi uko ulaya hawamaanishi na majungu na kujitungia habari zisizo na ushahidi

Mamilioni ya Watanzania wanafuatilia na wanataka kujua kulikoni kuhusiana na kashfa ya BoT. SIRI KALI haisadii pale ambapo inaficha ripoti kuhusina na ukaguzi uliofanywa na kampanu ya Ernst & Young. Makampuni yote yaliyohusika na kashfa ya BoT yamewekkwa wazi kwenye ripoti hiyo. SIRI KALI kama ingekuwa makini basi ingetoa ripoti hiyo hadharani na kuwataja hadharani wamiliki wote wa makampuni hayo, lakini kwa sababu zisizojulikana hawaoni umuhimu wa kufanya hivyo ili iwaendelee kuwalinda mafisadi wanaohusika. Kwa hiyo magazeti yana haki ya kuandika habari zozote wanazozipata, SIRI KALI kama inaona ni uzushi basi ituambie ukweli kuhusiana na kashfa hiyo ya BoT.
 
Hilo gazeti la Daima linachanganya habari za kweli na za uongo,za kufikilika na majungu,wana ushahidi gani kuwa kuna watu wamepanga kuhalibu ushahidi,au nia ni kuuza tu magazeti yao,wanaposikia wenzao wanafanya habari za uchunguzi uko ulaya hawamaanishi na majungu na kujitungia habari zisizo na ushahidi

Wewe naye vipi tena? Ni mmoja wao?
 
Hilo gazeti la Daima linachanganya habari za kweli na za uongo,za kufikilika na majungu,wana ushahidi gani kuwa kuna watu wamepanga kuhalibu ushahidi,au nia ni kuuza tu magazeti yao,wanaposikia wenzao wanafanya habari za uchunguzi uko ulaya hawamaanishi na majungu na kujitungia habari zisizo na ushahidi

Pamoja na kwamba wewe ni mmojawao hao wala nchi, tungependa raisi aseme huo ukweli wa uvumi ambao anasema kwamba tusiuamini. Ni uvumi gani huo ambao hataki kutaja ukweli wake? Sie tutaendelea kuamini uvumi hadi ukweli ujulikane. Hotuba yake ya juzi imejaa porojo tu, sijaona la maana ambalo tunaweza kulifanyia kazi kuhusu ufisadi!
 
Hilo gazeti la Daima linachanganya habari za kweli na za uongo,za kufikilika na majungu,wana ushahidi gani kuwa kuna watu wamepanga kuhalibu ushahidi,au nia ni kuuza tu magazeti yao,wanaposikia wenzao wanafanya habari za uchunguzi uko ulaya hawamaanishi na majungu na kujitungia habari zisizo na ushahidi


Subiri kidogo, yatakuwa yaleyale ya Mhindi wa Radar aliyedaka Mabilioni ya walalahoi wa Tz. Baada ya uchunguzi kukamilika na Nyaraka kubadilishwa. Kesi hewa itafunguliwa kwa Watuhumiwa ambao watakuwa wamekwishaikimbia nchi. UKIONA SIRIKALI INASUASUA KUHUSU KUWEKA WAZI REPORT UJUE IPO KWENYE CATCH-22.
 
Kumbuka uvumi ni moja ya source za habari nyingi na ambazo hatimae kuwatia watu hatiani.
Cha msingi Balali arudi then atumbie kinaga Ubaga kulikoni fedha zote izo kutumbuliwa?
 
Guys hii issue imekwisha ni ajabu kwamba hamlioni hilo ndugu zangu.Hizo kampuni zote zilizotajwa kuhusika mostly ni za kwao so kitakachotokea zote baada ya hiyo miezi sita zote zitasafishwa kwamba taratibu zote zilifuatwa.

Angekuwa serious Kikwete hakukuwa na haja ya kuunda tume kuchunguza kilichochunguzwa tayari ilikuwa ni kuchukuwa hatua straight forward.Hapo tumeliwa kwa mara nyingine ndugu zangu maumivu matupu.

Idimi Kikwete is never serious and will never be serious. Me nadhani kosa kubwa ni lile walilofanya watz 80% ya wale waliopiga kura. Kibaya zaidi ni kwamba adhabu ya kosa hilo si kwetu tu ni mpaka wajuu wa vining'ina vyetu. Maana kama wameuza hata Serengeti sijui tubaki na nini maskini. Pole sana TZ nakusikitikia kutokujuwa kuchaguwa kumekumaliza.
 
Hilo gazeti la Daima linachanganya habari za kweli na za uongo,za kufikilika na majungu,wana ushahidi gani kuwa kuna watu wamepanga kuhalibu ushahidi,au nia ni kuuza tu magazeti yao,wanaposikia wenzao wanafanya habari za uchunguzi uko ulaya hawamaanishi na majungu na kujitungia habari zisizo na ushahidi

Una hakika gani kuwa gazeti hilo linachanganya habari za ukweli na uongo? Kashfa imeshatokea, kuna haja ya kuijadili kashfa hiyo na kuangalia kila pembe, habari ziwe za kweli au uongo, kwa kufanya hivyo ukweli utajidhihirisha!
 
Tupo tunasubiri majibu,kama wanataka kuona watz tumekata tamaa basi tusipewe majibu ya kina kwenye hili sakata. Uchaguzi si 2010,wataona kitakachowapata
 
CCM na viongozi wake wa juu wanajua kwamba Tanzania ni mali yao wao na wala si mali ya Watanzania wote.
Kuhusu hii kashfa ya BOT CCM watafanya kila wawezalo kupiga danadana kesi na mwisho wake tutaishia maumivu.
Kwa binadamu mwenye akili timamu haingii akilini kabisa kitendo cha kuunda tume kuchunguza ripoti iliyofanyiwa uchunguzi na wataalamu husika. Ernest and Young ni very reputable firm kwenye mambo ya Finance. Wamefanya kazi yao ya uchunguzi na kutupa ripoti inayoonesha kabisa wezi ni hawa hapa (Kwa kutupa majina na kampuni husika). Ilikuwa ni kazi ya kuwakamata wahusika na kuwaweka ndani na wala hakuna haja ya kuunda tume.
Serikali ya CCM inataka kutafuta njia ya kufuta kesi hii kama si kuwaruhusu wahusika kukimbia nchi kama muhusika katika kesi ya Rada basi wanataka kuzua kioja kingine ili attention ya Watanzania ihamie huko na kusahau hili jambo.
Watanzania inaonekana tuna ubongo ulioganda na waoga kama mifisi. Kwa jambo kama hili ingekuwa ni vyema kuandaa maandamano ya kuishinikiza serikali kuwakamata wahusika wa kashfa hili na kuwaweka ndani mara moja na bila kuwasahau wahusika wa Richmond, Buzwagi nk.

Tukiendela kukubali usenge huu basi hawa mafisadi yataendelea kufanya ufisadi wao na bado yatarudi tena kwa wananchi kuomba kupigiwa kura wakati wa uchaguzi kwa kumwaga mapesa yao ya wizi.
Sina nia ya kuitakia maafa Tanzania kama ya Kenya lakini inapobidi kupigania ama kusimama kwa haki yako huna budi kufanya hivyo. (STAND UP FOR YOUR RIGHTS - BOB MARLEY), and SOMETIMES YOU HAVE TO FIGHT TO BE A MAN - KENNY ROGERS.
Tumeanza na hii ya kuwazomea viongozi wapuuzi, tusiishie hapo bali tuwapige na mawe na kuwafukuza kwani hakuna cha maana wanachofanya bali ni kutumaliza.

Angalia wenzetu wa Chad hawajataka kukubali upuuzi hivyo wanaionesha serikali yao wazi kwamba HAWATAKI UPUZI. Sisi tunadanganywa kwamba ni kisima cha amani duniani.
 
Hilo gazeti la Daima linachanganya habari za kweli na za uongo,za kufikilika na majungu,wana ushahidi gani kuwa kuna watu wamepanga kuhalibu ushahidi,au nia ni kuuza tu magazeti yao,wanaposikia wenzao wanafanya habari za uchunguzi uko ulaya hawamaanishi na majungu na kujitungia habari zisizo na ushahidi

Angalao unakuja pole pole!! Haya basi tufafanulie hizo za kweli!!1 Inawezekana wewe ndiye uliyekwenda CRDB kutaka kubadili zile akaunti zenu bila kujua zamaaani vijana wa kazi walikwisha kupita na wameondoka nazo, utahaha huku ukilia na kusaga meno, mulidhani Watanzania walio wengi watawaangalia mukifanya madudu na kuwachekea. Kila kitu kimekwisha kuchukuliwa. Hizo ni jitihada za kitoto, JK anazo doc zote labda yeye ndiye awasamehe na huyo bosi wenu ambaye nasikia amekwisha kukimbilia nje baada ya kuona Dodoma pako MOTO
 
Habari yote tisa, kumi Zitto anazidi kunipa nguvu za ajabu yaani kama kuna watu wachache kama huyu nadhani Udanganyika utakwisha....na nuru ya Tanzania mpya kuwaka.
 
Back
Top Bottom