Kama taratibu zitafuatwa ni kweli hakutakuwa na mtoto wa maskini ambae atakosa elimu ya juu. Walengwa katika hili wanakosa nafasi hiyo kutokana na baadhi ya watu kujivisha nafasi hiyo ili kupata njia mtelemko ya kupata elimu hiyo ya juu.Huyu huyu aliwahi kutwambia kwamba' "Hakuna mtoto wa maskini Tanzania atakayekosa elimu ya juu" na ukweli kuhusu yanayojiri pale UDSM unapingana na kauli yake hiyo. Hivyo hili pia inaweza kabisa kuwa ni kujiosha tu machoni mwa Watanzania.
swali zuri sana hili.yale yale ya graduates wa SUA badala ya kwenda kuhimiza kilimo bora na chenye tija vijijini wanajazana benki kuwa ma loan office na ma teller...halafu unazindua mkakati wa KILIMO KWANZA.....!!!! najutaaa kuwa mtanzaniaWhy tuwe na njaa? Sielewi kabisa...
Mwanatanu..unajua kuna wakati nafikiri Mungu akiingalia Tanzania anatikisa kichwa kwa masikitiko na kuuliwa "niwape nini watu hawa"?
akiba ya chakula tanzania ipo tena kubwa sana, jamani hadi muambiwe kila kitu ?
chakula kipo, na kama hakipo, basi mnafaa kulaumiwa nyinyi mnaolalamika ! Hamtaki kwenda kwenye mashamba kazi kwenye intaneti 24/7, mara ya mwisho Mnyika alikataa kata kata ushauri wangu wa kwenda shambani instead akaenda kwa wamachinga.
Kila mmoja humu anaweza kulima hekari 20 kutokana na uwepo wako humu ( kuna baadhi wanalala humu humu) hao nadhani wanaweza kuzalisha zaidi ! kama akina mwafrika wa kike !
mkuu sijaelewa sehemu hiyo niliyopigia mstari naomba muongozo
Hata hivyo njaa ambayo naweza kuiangalia toka mbali na inayosogelea kama simba anyatiaye haitokani na mambo hayo bali makubwa mawili.
a. Kupanda kwa bei ya chakula duniani.
Habari za leo ni kuwa bei ya chakula duniani imepanda kwa haraka kuliko wakati wowote ule na hivyo kusababisha ugumu wa kupatikana kwa chakula. Yaliyotokea Haiti na Misri siku chache zilizopita ni dalili ya ubaya wa hali hiyo. Kwa wale walioko Dar au maeneo yenye masoko ya kudumu na kwenye mialo mbalimbali kanda ya ziwa wanaweza kutusaidia kutuambia kama kumeanza kutokea mabadiliko yanayoonekana ya bei ya chakula siku hizi chache zilizopita.
b. Mvua ya masika.
Hata hivyo naamini kwa upande wa Tanzania kitakachosababisha njaa sana ni hii mvua ambayo imeharibu mashamba na mazao ya watu kiasi kwamba baadhi ya maeneo ambayo kwa kawaida yana chakula cha kutosha yanaweza kujikuta yanahamia mwaka huu. Kama mpunga wa Kyela utakuwa umeathirika kama Dr. Mwakyembe alivyosema kwenye mahojiano yake nami kuna uwezekano kuwa Mwaka huu bei ya Mchele nayo itapanda na hivyo kufanya nafaka hiyo ianze kuwa adimu na kupatikana kwa wachache.
Kwa vile tunajua haya yote na ziada; tufanye nini ili tujiandae na njaa ijayo?
Kama tuna serikali kubwa namna hii, yenye waziri, naibu waziri, katibu mkuu, mkurugenzi wa wizara na maofisa kibao wa wizara husika wanafanya nini? Kweli hawa ni mzigo kwa walipa kodi.
Bajameni habari ndo hiyo na lisemwalo lipo ka halipo basi li njiani. Zaidi wana JF erimisheni umma kuweka akiba kwa wakati mgumu usemwao. Mie sishangi kwa hili yawezekana unabii unatimia. Tusiwe ngedere aliye juu ya mti ikishangilia kuungua kwa msitu akali yumo humo. Zaidi ni kuwashawishi washauri na wataalamu kusimama katika nafasi zao ili kulinusuru Taifa letu ktk balaa hili. Maana kama tunaweza kuwashawishi watu fufani kugombea nyadhifa mbalimbali na ikawa si zaidi kwa hili??????
Mkuu;
Niliangalia hicho kipindi maalumu, I felt like crying . . . .
Nikaumia zaidi na kujilaumu kwamba wakati mimi nakula na kusaza, kuna watu wanakufa. I wish they were close nisaidie ninapoweza.
naibu Waziri wa kilimo anulizwa, anadai chakula kipo inatakiwa wakifuate katika maghala na kuwa labda hawana fedha za usafiri . . . . Grrrrrrrr I was shocked to hear that.
Then sijui chakula cha msaada ni kilo 10+ kg kwa kaya. I wonder kitawachukua muda gani kabla ya kwisha.
Tanzania hii yenye neema watu wanakula mizizi kweli . . . something is wrong in this country.
The question is: What is wrong and what can be done to bring positive changes?