Kabende Msakila
JF-Expert Member
- Oct 7, 2020
- 1,398
- 1,264
Nimekuelewa kiasi ingawa bado nahitaji kufahamu:-Shida ninayoiiona kwa wanasiasa wengi ni kutumia wananchi kama chambo ya kupata kile wanachokitafuta wao na sio kwa maslahi ya wananchi.
Sasa mimi nasema nataka kuwa mwenyekiti wa chadema, au nataka kuwa kiongozi Mkuu wa ACT wazalendo
Je unadhani nitafanikiwa kumngoa mbowe Chadema? au nitafanikiwa kumung'oa zito ACT? Ninaamini vyama hivi si mali zao ila kwa hulka zilezile wanazoziona upande mwingine na kupiga kelele na wao wanazo.
kila uchaguzi ukifanyika kwenye vyama vyao leo wataendelea kubaki madarakani na kwao huo sio udikiteta bali uchaguzi ukifanyika serikalini na watu fulani wakabaki madarakani basi wanapiga kelele.
Hoja yangu ni kama hatutakuwa na double standard tutaona kuna hulka za kijamii ambazo ndizo zinapigiwa kelele.
Mimi sina Tatizo na mbowe kuendelea kuongoza chadema, au zito kuendelea kuongoza ACT au JPM kuwa raisi wa Tanzania ninachokisema
Watanzania tusikubali wahuni wavuruge nchi yetu kisa eti mbowe kashinda kuwa mwenyeti wa chadema tena na wao wanaamini mbowe anatumia ujanja kuendelea kukalia kiti hicho cha uenyekiti.
Watanzania tusikubali wahuni kuvuruga ama uchumi wetu au amani yetu kwa kisingizio eti Zito anaendelea kukalia kiti cha kiongozi mkuu wa act wazalendo na wao kuamini zito kukalia sio demokrasia.
Watanzania tusikubali wahuni kutuvuruga kwa kisingizio cha JPM anaendelea kuongoza nchi hii kwa wao kuamini sio demokrasia.
(i). Ni kweli kwamba ktk uchaguzi uliopita walikuwemo wahuni wachache ktk kundi la upinzani? (Viashiria vya uhuni wao ni vipi?
(ii). Nchi marafiki kutupa misaada inaweza kuwa hiari yao - lkn je sababu zinazotajwa kutumiwa kutunyima misaada ni sababu zenye uzito au ni nyepesi i.e wanazungumzia uminywaji wa demokrasia - vipigo - na vifo kwa baadhi ya maeneo; je hizi sababu hazina ukweli na uzito?
Machache tu mkuu