Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,262
- 9,714
Ndugu zangu Watanzania,
Hapo usiku wa jana katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani Rais wetu na jemedari wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge alishiriki katika the citizen Rising woman.ambapo aliweza kuzungumza mambo mbalimbali na mengi sana.
Lakini pamoja na mambo mengi kugusiwa kuna eneo moja lililoteka hisia za wengi sana, ambalo lilikuwa ni juu ya R nne alizokuja nazo baada ya kushika madaraka ya Urais.anasema mara baada ya kushika madaraka ya Urais alisikia watu wakimwambia Mama mama unganisha Taifa.anasema kauli hizo zilimfanya ajiulize na kujipa jibu kuwa Taifa halipo pamoja na kuna mgawanyiko ndani ya Taifa.
Hivyo baada ya hapo akaamua kuja na R hizo nne za kuvumiliana,kustahimiliana, kufanya mabadiliko pamoja na kujenga upya Taifa letu.anasema kuwa akaanza kuzungumza na watu mbalimbali,taasisi ,makundi pamoja na vyama vya siasa.akaendelea kueleza kuwa adhima ikiwa ni kulileta pamoja Taifa na kujenga umoja wa kitaifa .
kwa kuhakikisha kuwa tunasameheana tulipokoseana,tunavumiliana,tunafanya mabadiliko ya mambo yanayotoa uhuru kwa watu kuzungumza na kueleza hisia zao pamoja na kujenga upya Taifa katika namna ambayo kila mtu atajiona anayo nafasi katika ujenzi wa Taifa letu pamoja na kutoa mawazo yake .yaani kila mtu anashiriikishwa na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa na siyo yeye kama yeye Rais kujifungia ndani na kufanya maamuzi peke yake juu ya Taifa letu..
Ndugu zangu Watanzania katika hili Rais Samia ameweka alama ya kudumu iliyoandikwa na kuchorwa kwa wino wa dhahabu katika mioyo ya watanzania.ambapo atakumbukwa vizazi na vizazi kwa namna alivyo liunganisha Taifa na kujenga umoja wa kitaifa.vifua vya watanzania vimejaa furaha,amani,uhuru na vimefunguka kama geti lililofunguliwa.hali hii imechochea ushirikiano na mshikamano miongoni mwa Watanzania pamoja na kupalilia mbegu ya upendo na kutamalaki kwa amani na utulivu hapa Nchini.
Hakuna manung'uniko ya watu kuonewa , kudhulumiwa,kunyanyaswa na kukandamizwa.na inapotokea mtu kafanyiwa hivyo na ikajulikana kwa mamlaka hatua kali na za haraka zimekuwa zikichukuliwa kwa watu waliofanya uonevu au uovu huo.hii imejenga imani kubwa sana kwa watanzania kwa serikali yao na kuiamini sana na kuendelea kuiunga mkono muda wote.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.