Niwaombe Watanzania "yeyote anayepita jamii za kimataifa kutuombea njaa" tumuone ni mhaini

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Kwanza kabisa niseme wazi kuwa mimi binafsi sio kwamba naridhika na kila kitu kinavyotendeka katika nchi yangu hii lakini ustawi wa watanzania wote, ustawi wa nchi yangu ni bora kuliko matakwa yangu binafsi.

Nilivyokuwa mdogo niliwaza sana kufanya kazi katika taasisi kubwa za nchi hii kwa maana mafanikio tuliyaona kama yanatokana na kuajiriwa na taasisi kubwa, lakini nilivyokuwa mkubwa haikuwezekana kuweza kufanya kazi katika taasisi hizo. Nadhani kila mtanzania anaelewa kuwa kwa mazingira tuliyokuwa haikuwezekana kwa kila mtanzania kupata ajira TRA, Bandarini, Benki kuu n.k. Kwa busara zetu watanzania hatuwezi kuzusha uhasama miongoni mwetu kwa mambo kama haya ila tunaamini kadiri mda unavyosonga mambo mengi yanabarika.

kwa kifupi hakuna mtanzania yeyote ambaye anaweza kujiona kila sehemu katendewa kama alivyostahili.

Hoja yangu kubwa leo ni kwa Wanasiasa wetu.

kuna wanasiasa wanatuaminisha wanatendewa ndivyo sivyo hivyo wameamua kututafutia njaa kwa kujaribu kushawishi jumuiya za kimataifa zituwekee vikwazo n.k.

Daima mimi huwa naamini hakuna familia isiyokuwa na ugomvi au changamoto ndani, kuna familia baba ananyimwa unyumba, kuna familia kutukanana kila siku ndiyo mfumo wa maisha, kuna familia kuna baadhi ya watoto wanapendwa zaidi kuliko watoto wengine. Yote haya hayampi kibali mmoja wa wanafamilia hii kuombea njaa familia yao.

kwamba baba ukinyimwa unyumba ambao ni haki yako ya msingi na kila mmoja anaelewa haihalalishi wewe baba wa familia kwenda kuchukua shoka na kuchinja mke na watoto wa familia. baba kunyimwa unyumba haikupi kibali cha kuwalaza na kuwashindisha njaa watoto wa familia yako. Siku ukifanya hivyo watu watakushangaa na kukudharau wewe baba.

Kwamba mtoto, kama baba yako anampendelea sana ndugu yako katika kila kitu na ninyi wengine mnabezwa na kudharauliwa na kunyimwa mahitaji, je hilo linaweza kuhalalisha wewe mtoto kuendesha harakati za kuhakikisha nyumbani kwenu hampati chakula au mahitaji? huo ndiyo ujinga ambao shule zetu zilitakuwa kuuondoa kwamba hauwezi kufocus kwenye tatizo dogo na kutengeneza tatizo kubwa kama suluhu la kutatua tatizo dogo.

Wapo wanasiasa wanapita pita jumuiya za kimataifa kutafuta sapoti kwa watanzania kuwekewa vikwazo na kunyimwa misaada eti kisa wanaona wanatendewa ndivyo sivyo.

Sijui kama watanzania wanaelewa maana ya jambo hili wanalolifanya hawa wenzetu.

Jambo la kwanza tanzania kunyimwa misaada na kuwekewa vikwazo hakuwezi kuwaathiri viongozi walioko madarakani hata kidogo bali wananchi wa kawaida tulioko mitaani ndiyo tutaumia na hatua hii. Watanzania wenzangu hebu tuitazame Zimbabwe ilivyokuwa.

Wazimbabwe walikuwa na siasa za mvutano baina ya Robert Mugabe aliyekuwa raisi wa nchi hiyo na Morgani Tsvangirai aliyekuwa upinzani. Waliendesha mivutano na wapinzani wakafanya kampeni za kutokuwepo demokrasia na kadhalika na kuishawishi jumuiya ya kimataifa kuiwekea vikwazo nchi yao. Kwa kifupi vikwazo viliwekwa maana mkishaanza kupiga kelele kutafuta vikwazo huko nje watatafuta kila namna na kila sababu watawawekea vikwazo hata kama havihusiani na hoja za wapiga kelele. Leo Hii tumesahau yale yote na kila mtu anapiga kelele Zimbabwe iondolewe vikwazo baada ya kubaini mateso makubwa wanayopitia Wazimbabwe kutokana na vikwazo.

Hivi vikwazo vimebadili siasa za Zimbabwe? Siasa zimebaki vilevile watawala wameendelea kuwa watawala na watawaliwa wakaendelea kuwa wataliwa. Hivi kweli mtanzania anayepita huko kutuombea vikwazo anatutakia mema sisi watanzania wa kawaida? na je mtu kama huyo tunaweza kumuwaza hata kumpa uongozi wa kijiji kimoja tu?

Sisi Tunatamani mtu ambaye anahitaji kuwa kiongozi wetu, ikitokea akaulizwa tuwatese watanzania tukufanye tajiri au kiongozi ? na yeye ajibu Kuwatesa watanzania kwa ajili ya mimi kuwa kiongozi au tajiri ni bora utajiri na uongozi niviache na watanzania waishi salama. Lakini hapo simaanishi kuwa ukiwa kiongozi basi wakitokea wahuni wakaaanza kuwatesa watu eti ili uachie madaraka na wao waongoze basi hapo nchi huwezi kuwaachia wahuni na huko ndiko kutetea watu wako.

Tuchukue mfano mwingine, tutazame libya jinsi watu walivyoamini Gadhafi alikuwa anawatawala kidekiteta na kutafuta msaada kumuondoa ghadafi, tutazame libya ya leo na libya ya Ghadafi. Tazama nchi zote ambazo watu wake wamekimbilia nje kutafuta msaada kwa "ujinga wa demokrasia" nchi zao wamezipeleka wapi?

Watanzania ni lazima tuelewe kuna mambo ambayo ni ya nyakati na kuondoka kwake, yanaondoka na nyakati.

Huko zamani tulikuwa na tawala za kifalme ambazo mfumo wake ulikuwa wa kibaguzi kabisa kwamba kuna familia moja ndiyo imechaguliwa sijui na nani ? na hiyo familia ndiyo ilitoa wafalme wa kutawala jamii zetu na kuna familia zilikuwa "branded" familia za mikosi. wazee wetu waliishi kwa amani kwa walikubaliana na mambo hayo ambayo yalikuwa ya nyakati hizo.

Hivi tujiulize kuna mtu gani angeweza kuleta mabadiriko ya kweli katika jamii za kifalme kama angewezakupambana kukataa utawala wa kifalme? kiukweli hakuna yeyote bali ni mtu kujiona hawezi kutawaliwa na mfalme na kutafuta yeye kujiweka kuwa mfalme na wengine kutawaliwa.

Lakini wahenga walisema " time heals" sasa Leo hii tawala hizi za kifalme ziko wapi? maana yangu ni kwamba yapo mambo ni ya nyakati na yataondoka na nyakati. hata hao hao wanaojifanya kupigana nayo ukweli ni kwamba wanatafuta kukalia nyadhifa za juu tu lakini wakifika huko na wao utawala wao utakuwa vilevile. kama uamini basi jaribu kufuatilia taasisi zinazopiga kelele juu ya demokrasia na uzitazame zenyewe zinaendeshaje demokrasia hiyo hiyo ndani ya tasisi zao?

ni mambo yaleyale ya kuwapa wake zao nafasi za viti maalumu, au watu kupita bila kupingwa kugombea katika majimbo au mwenyekiti hachalenjiwi.

Kuhusu uchaguzi mkuu mimi naamini vyama vya upinzani vimeshindwa kihalali kwa maana wananchi wameviadhibu kwa kuacha sera zinazochochea maendeleo ya wananchi na kubeba hoja za kupinga serikali kila inachokifanya.

Hebu tuvitazame vya vya upinzani miaka iliyopita vilikuwaje?

vyama hivi vilijenga hoja ambazo zilikuwa zikiwapendeza wananchi. walikuwa wakihoji iweje nchi yetu iwe na ndege moja na ka nchi kama rwanda kana ndege, uwekezaji katika miundo mbinu kama ya kuzalisha umeme walisema tanzania tangu ilipowekeza miaka ya 1970 basi, reli imekufa n.k

wananchi walivipenda na kuongeza ushawishi na uwakilishi.

leo hii watu wamebadilika wanapinga mambo yote ambayo waliyapigania mda mrefu na yakawapandisha chati, unategemea nini?

Sasa tutulie tujenge nchi yetu.

swala la kwamba mimi ninataka kuwa msanii lakini ma promota wana upendeleo wana wabeba badhi ya wasanii na kuwakataa wengine na hivyo unataka kutuharibia nchi kisa eti mapromota wamekubagua hilo haliwezekani.

swala la kwamba na wewe una vigezi na haki ya kuajiriwa BOT lakini eti wameajiriwa watu kwa upendeleo hivyo unataka kuvuruga maisha ya watanzania hilo halikubaliki

yapo mambo tunaweza kuyaona hayako sawa lakini ukitazama kile unachokitafuta nacho hakiko sawa hivyo tuvumiliane tujenge nchi yetu na yeyote anayewaza kubomoa nchi yetu kwa kigezo yeye kanyimwa kitu fulani huyo tumkatae sote.

mimi nilivyokuwa mdogo wazazi wangu walimpenda sana ndugu yetu ambaye alikuwa anasoma seminari na sisi kuonekana hatuna lolote. Ninachokuhahakishia Leo hii ninavyoongea ukubwani mambo yamebadirika na wazazi hawa hawataki hata kukumbuka kama kuliwahi kuwepo na mazingira hayo.

Nyakati zimeondoa hali iliyokuwepo na ninaamini chochote ambacho watanzania wanaona hakiko sawa, waendelee kuelimishana na mambo hayo yataondoka lakini watanzania tusitafute shida kwa watanzia wenzetu
 
Wezi wa kura za wananchi ndio wahaini. Wametumia jeshi na akina Mahera kupindua matakwa halali ya Watanzania wa Zanzibar na Tanganyika. Hao ndio wahaini.
Kwanza kabisa niseme wazi kuwa mimi binafsi sio kwamba naridhika na kila kitu kinavyotendeka katika nchi yangu hii lakini ustawi wa watanzania wote, ustawi wa nchi yangu ni bora kuliko matakwa yangu binafsi...
 
Kuhusu uchaguzi mkuu mimi naamini vyama vya upinzani vimeshindwa kihalali kwa maana wananchi wameviadhibu kwa kuacha sera zinazochochea maendeleo ya wananchi na kubeba hoja za kupinga serikali kila inachokifanya.
"Vyama vya upinzani vimeshindwa kihalali.."?? Hapa ndo umeharibu kabisa mantiki ya uzi wako.. ma-taga bhana!

Wananchi walio wengi wanabaguliwa wazi wazi na kikundi kidogo cha waovu, afu unasema watanzania wote tuungane dhidi ya michakato ya UKOMBOZi?!
 
Kwanza kabisa niseme wazi kuwa mimi binafsi sio kwamba naridhika na kila kitu kinavyotendeka katika nchi yangu hii lakini ustawi wa watanzania wote, ustawi wa nchi yangu ni bora kuliko matakwa yangu binafsi...
Hakuna mwanasiasa mwenye mapenzi na wananchi wala nchi yake. Wanasiasa wapo kwa ajili ya utawala na si vinginevyo. Wanasiasa wapo kwa ajili yao binafsi.

Nakubaliana wewe kwa kuliona hilo. Politicians are after Power and no otherwise.
 
Mhaini wa kwanza ni jiwe na genge lake ambaye ameifanya nchi kuwa mali yake binafisi. Hivi Magufuri ndio rais wa kwanza kuliongoza taifa hili? Je, kama sio wa kwanza kwanini hao mabeberu watuingilie wakati wa hawamu hii ya 5 na si hawamu zilizo pita?

Umetolea mfano wa Zimbabwe huo ni mfano harisi kabisa ya kwamba viongozi wa Africa sio watu wanao jali maisha ya raia wao bali masilahi yao tu.

Viongozi wa Zimbabwe wangekuwa wanawapenda raia wao wange tekeleza yale yanayo takiwa kufanyika ili iondole vikwazo.
Hebu angalia raia wa Zimbabwe wana teseka kwa sababu tu ya kulinda masilahi ya kikundi cha watu kama100 walioko madarakani.

Sasa hivi Zimbabwe hela yake imegeuka makaratasi haina thamani yeyote, madawa hakuna,chakula cha shida, maji ya shida umasikini ulio kithiri haya yote yame sababishwa na mtu mmoja aliye kuwa anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa kujivika ngozi ya uzarendo.

Hivi utajiitaje kiongozi mzalendo kwa taifa lako wakati taifa lako linaangamia kwa sababu tu ya kulinda chama chako?

Na Tanzania ina elekea kwenye njia ya Zimbabwe kwa sababu ya mtu mmoja anaye jiona anajua kila kitu.
 
Hapa ndo umeharibu kabisa mantiki ya uzi wako, ma-taga bhana!

Wananchi walio wengi wanabaguliwa wazi wazi na kikundi kidogo cha waovu, afu unasema watanzania wote tuungane dhidi ya michakato ya UKOMBOZi?!
Michakato ya ukpmbozi ??????

hizi nyimbo huwa tunasema wajinga ndiyo waliwao

hakuna mtawala anayeweza kutawala na watu wote, kila mmoja huiba nyimbo zake ili kupata madaraka na yeyote anayepata madaraka huchukua kikundi kidogo na kuwatawala walio wengi.

nimesema tazama vyama vya upinzani kimoja kimoja uniambie "reflection" ya ukombozi unaiona wapi katika yale wanayoyafanya ndani ya chama chao.

ni wangapi wamekimbia vyama vya upinzani kwa kudai kutendewa ndivyo sivyo? ipo mifano hai Ziko kabwe alitoka Chadema kwa sababu gani?

Sina maana ya kutetea watawala kuwa kila wanachokifanya ni sahihi ila watanzania tusiwe wajinga kwa wanasiasa kuharibu maisha yetu wakijifanya wanatafuta haki.

Yeyote anayeenda kushawishi tunyimwe msaada kisa eti anadai katendewa ndivyo sivyo kwenye siasa ni sawa na baba anayewanyima watoto wake chakula kisa eti mama kamnyima unyumba na huyo ni adui wa taifa letu.

kama taifa ni lazima tupambane na ujinga huu wa mtu kudanganya watu natafuta haki wakati anachokifanya ni kutaka kuvuruga maisha ya watu.

Zamani nikiwa mdogo nilikuwa naifutilia nchi ya burundi.

hawa jamaa tangu nikiwa mdogo ni vita ya wenyewe kwa wenyewe, kila raisi anayeingia madarakani basi hutokea waasi wa kupigania haki. mpaka Leo hii nchi haijatulia, maisha ya watu yamerudi nyumba kwa ujinga wa watu wachache kudhani wanatafuta haki.

Kamwe hatuwezi kuruhusu ujinga kwa bendera ya kutafuta haki na kamwe wewe mtanzania popote ulipo usije kuingia kwenye mkumbo usioujua.

Nguvu ya kufanya maamuzi au mabadiriko ya nchi hii unayo wewe mtanzania na utayatumia pale tu unapoona au inapobidi.

kama mtanzania alipiga kura yake na ikaibiwa yeye ataona na sio mtu ambaye ni mpigiwa kura ndiye anawaambia wapiga kura nimeibiwa kura.

Narudia sisemi kuwa nafurahia mambo yote wanayofanya watawala lakini busara inanituma kurithika na hiki kidogo ninachokipata kuliko kurubuniwa na wajanja wachache kutumia shida zangu kuvuruga nchi yetu.

Ninaamini mkombozi wa kweli atakuja kwa njia ya kujenga nasio kuharibu na mtu yeyote anayejaribu kuharibu hana sifa ya kuwa kiongozi.
 
View attachment 1631830
Hivi hii picha siwezi kuuza kwenye political magazines huko “majuu ” 😄😄😄😂😂😂
Swali lako linaonyesha kabisa kuna watanzania wanatengeneza matukio ya kupatia pesa huko majuu.

hivi kweli kwenye kuhesabu kura wanafungua bahasha kutoa kura zilizoko ndani na kuzihesabu? haya ni mambo yanatengenezwa na baadhi ya watanzania kutafutia pesa huko majuu lakini siamini kuwa kuna mtu anaiba kura kwa kuweka kura nyingi kwenye mabahasha.

Ni lazima tuwabaini watanzania wote wenye akili za mitungi, kuharibu jina la nchi yetu ili wao wapate utajiri
 
Mjaini wa kwanza ni yule anayeiba kura na kuwanyima wananchi haki yao ya kichagua viongozi. Maana yake wameacha viongozi wanatakiwa na wananchi na kujipachika wao.

Ni bora vikwazo ili watunyooshe sababu hata sisi wananchi tumeona wizi uliofanyika hatujachukuwa hatuo. Bora watunyooshe na vikwazo hao wanatutendea haki sawasawa na matendo yetu ya wizi
 
Kwanza kabisa niseme wazi kuwa mimi binafsi sio kwamba naridhika na kila kitu kinavyotendeka katika nchi yangu hii lakini ustawi wa watanzania wote, ustawi wa nchi yangu ni bora kuliko matakwa yangu binafsi...

Kwahiyo wewe unataka watanzania wasiwe hata na haki ya kuchagua viongozi wao kikundi ka watu wajitengenezee kura pembeni na kujitangaza washindi halafu sisi tuogope vikwazo ili tuyawalowe. Mbona vikwazo walipowekewa afrika kusini hakuna aliyesema vinaumiza waafrika wote tuliunga mkono na mwishowe Kaburu akaondoka.

Hata hivi vikwazo vitasaidia madikteta waondoke hasa baada ya wananchi kuelewa kiwa wanazidi kuwa masikini sababu ya dikteta aliyeko madarakani itabidi afu,ushwe mara moja. Mimi kama mtanzania kwa lile vurugu la uchaguzi vikwazo watuwekee tena hadi tuwe tunashindwa hata kulipa mishahara maana wafanya kazi wenyewe ndo hao walioshiriki kuiba kura bora wafanya kazi bila mshahara ndipo wajuwe ubaye wa dhuluma.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom