Niulize swali lolote kuhusu Pemba na Wapemba

Niulize swali lolote kuhusu Pemba na Wapemba

Hizbu ni akina nani?

Naweza pata Binti wa kipemba mwenye asili ya kiarabu?
 
View attachment 366523 View attachment 366523
Nimeamua kuja hapa rasmi kuizungumzia hali ya Kisiwa cha Pemba kimazingira, Uchumi,Afya,elimu, utamaduni na watu wake. Nimezaliwa Pemba eneo moja la kaskazini mwa kisiwa hiki chenye urefu wa wastani wa kilomita 95, Ni kisiwa chenye amani iliyorithiwa na sio ya woga. Watu wake ni wakarimu sana, lakini sio watu wanaopenda kuendeleza elimu kama msingi wa maisha yao. Hususani ni kipindi hicho ambacho tulikua tukisoma sisi sasa hivi ni tofauti kidogo zaidi kwa watoto wa kiume. Kwa upande wa watoto wa kike wazee hawaweki kipaumbele cha elimu.

Pemba imejigawa Miji mikuu 3, mizuri sana yenye huduma zote za jamii inayojitosheleza. Miji hii imejigawa na nikutoka kilomita 18 hadi mji mwingine. kwakua Miji hii imejigawa unaweza ukifika ukasema Pemba hakuna Maendeleo lakin Maendeleo yapo sababu kuu ya kutoyaona maendeleo hayo ni kila Mji na watu wake na Mambo yakeView attachment 366635 .View attachment 366631 View attachment 366632View attachment 366634 Bahari ya Pemba ni Blue yenye beach nzuri sana, ikiwa ina navisiwa vidogo vidogo ndani yake.

Idadi ya Watu wa Pemba kwenye sensa ya mwaka 2012 ni 406,808 ingawa wengi kipindi kile hawakujiandikisha.


Nimejifunza mengi sana katika maisha yangu ninayoishi pemba, kwakua nakielewa kisiwa hiki utandu na ukoko vizuri sana kuanzia ncha ya kusini mwa kisiwa mpaka kaskazini mwa kisiwa. Nimevutiwa kuweka bayana hapa kuhusu Hali yote ya pemba kwa sababu:

Nimepata changamoto nyingi niliposafiri sehemu tofauti watu wengi wana shauku ya kuijua Pemba na wapemba wakoje, wengi wanawaona wapemba kama hawasomeki au hawaeleweki, wengi wanawaona wapemba wana msimamo si watu wa kuyumba, wachawi ni watu wa kujituma.Wabaguzi hawapendi kujichanganya na wengine.

Nina majibu ya kutosha kuhusu hayo hapo kwa ufupi, ninapenda ukiwa na chochote ambacho umewahi kusikia kuhusu Pemba au kukukutokea niulize, nitajibu majibu yasiyopendelea upande wa kwetu au kujinasibu kwa majibu ya kejeli kwa wengine. nimeishi na watu tofauti nimesoma mazingira na tabia za watu wengi sana.View attachment 366637 View attachment 366639
Nikusaidie yafuatayo kuhusu wapemba:-

1. Wapenda sana uarabu, yuko tayari kufanya chochote aitwe Mwaarab! na ukitaka kumfurahisha mpemba basi wewe muite Mwaaarab, hapo utaona meno yake yote.

2. Hawapendi kuchanganyana na watu wengine wa makabila mengine, hua wanapenda wanapokua wao wawe ni wao tu, na wako tayari kwa hila zozote wakuhamishe kama utawakaribia,angalia, walivyo wengi, Kwarara,Mtoni Kidatu,

3.Wana choyo cha maendeleo na wana juhudi sana ya kazi.

4.Kila kwenye biashara ya mpemba shiriki ni lazima na lazima aweke jini dukani.

5.Ni wabaguzi wa hali ya juu, hata kama ukienda kwenye duka lake kama sio mpemba lazima atapandisha bei.
 
Dada Faiza Karibu sana tena sana kwa mara nyingi zaidi, wengi wanaisema Pemba na Wapemba tofauti kabisa na hasa wanaoisema ni wale waliokua hawaijui Pemba na Hawajui Wapemba wenyewe.

Karibu sana mara nyingine ukifika Pemba nipo Mji mmoja unaitwa Wete, Kwa Pemba mimi ni Maarufu kuliko Maalim SEIF.

Karibu sana.
Akija mlete hadi mchanga mdogo, pale ndo kwetu... Siku moja moja naeza kua masota kwa anti
 
Me muislamu na nisha Date na bint wa Kipemba akaniambia hutanioa kwetu hawatak mtu wa Bara
Kwa hiyo unahukumu jamii nzima ya wapemba kwa maneno ya huyo binti mmoja tuu?

Hakuna kabila bara ambazo hazitaki kuolewa na kabila fulani? Humu humu JF kuna watu hua wanadai hawataki kuolewa na Wakurya,hao utawahukumu vipi?
 
Wale wapemba weupe kama waarabu wanapatikana sehemu gani? Hapo pemba nataka nije kuowa huko nasikia bila milioni hupati mke na vip tabia zao wanawake wa kipemba? Majbu plz
 
Mimi niseme majungu yananguvu siku zote kuliko ukweli, Ukweli hakuna Wapemba wachafu, Lakini pia hawapendi kuvaa suti, ili umuone Mpemba amekuwa smart mpaka avae kimini? Swala la kunguni lilikuwepo miaka hiyo ambayo umaskini ulikuwa juu tofauti na sio sasahivi na jamii nyingine walikuwa wanalala na ngombe na mbuzi kwenye mabanda kama wanyama.
Unaposema miaka hio sijui unamaanisha mwaka gani,hii habari ya kunguni si habari ya muda mrefu,any way inawezekana hii inauma kidogo lakini ndio ukweli huo,halafu kuhusu ubaguzi naona hujalisemea lolote.Na ndio ndio maana licha yakua zanzibar inawakazi tofauti kama wapemba,waunguja na wengine lakini wanaowika ni wapemba tu kila pahala ho wengine hawasikiki hapa utagundua kwamba wapemba ni wabaguzi ukilinganisha na hao wengine.
Hata hii habari ya kelele kwenye muungano bado utaona msingi wake mkuu ni ubaguzi na hasa ubaguzi wa kidini.
 
Mambo yafuatayo yanawafanya wapemba kuonekana wanapenda siasa.

Kuonekana wachawi.

Wanazaa sana.

Wabaguzi.

Wachafu.

Hawajengi kwao.

Hizi ni propaganda za kupindukia.Ni wapemba asilimia kubwa ndio wana mashirikiano na pande zote Tanzania.
Wapemba wameshika Dini na uchawi kwa kiwango kinachotajwa si kweli.
Miundo mbinu ilicheleweshwa sana,Kiasi mpaka miaka hii ya 2000s walitumia generators na barabara mbovu na finyu.Wanabaguliwa pakubwa kwenye kazi kiasi cha kua wajiri wa taasisi za serikali hukimbilia zaidi cheti cha kuzaliwa hata kabla kukagua certificates za masomo.Suala la uchafu si kweli mana maambukizi ya kipindu pindu yapo chini.Kuhusu kuzaa sana ,Tanzania nzima ilikua ina tatizo hili kabla(ndio mana kukawa na taasisi nyingi zinazo endesha mpango wa uzazi wa mpango )mbona haziku dominant Pemba tu?.
Wameonekana ni wapinzani wakubwa ni kwa sababu tu hii ndio njia halali ya kutumia demokrasia kudai mabadiliko ya kiuchumi na kueleza mawazo mbadala.
Suala la kuzaa sana pemba naweza kusema kuwa ni starehe zetu kwa wake zetu, kwa maana ya kwamba pemba hakuna starehe kama baa na maskan, hata kama zipo wakati huu, basi wapemba wanapenda sana family zao, mke watoto, na kutokana na umasikini wa wapemba, watoto ndio utajiri mkubwa, pemba shughuli nyingi za kutafuta zinamaliza saa 4 yaani saa kumi, na hii ni kutokana na geography ya pemba na population, ukifika muda huo kila mtu hurudi kwake au aliko toka.

Raha ya pemba saa kumi na nusu ushapata chajio, unavaa serun yako umeridhika alhamdullah, unasubiri bibie afukize udi
 
Kwa nin wapemba wanaipenda sana cuf?


Wapemba wanaipenda CUF kwa kufikiria tuu kuwa siku moja inaweza ikawatoa walipo na kuwafikisha sehemu wanayotaka. Mawazo haya yapo sana vichwani mwa Wapemba karibu wote na ni shida sana kuwabadilisha kama Serikali inavotaka.
 
Kwa nini hakuna shule ya pemba kwenye kumi za mwisho, wakati unguja zipo saba? Matokeo fm6
 
Kwa nini Nungwi manahodha wanapaogopa

Mkuu Nungwi ni kiunganishi cha mzunguko mkubwa wa bahari ya Tanga,Pemba na Unguja hapa maji yanazunguka hayaeleweki. Kiukweli panatisha na sio kwa manahodha tuu hata abiria. Tuombe Mungu sana awe anatuvuusha salama kwenye mkondo huu na hasa katika kipindi hiki.

Serikali ingeweka bandari nungwi kuwa kiunganishi cha Unguja na Pemba iwe rahisi kufika kwakua sehemu hii kama itakuwa na bandari ni Dakika 40 tuu itakua safari ya Unguja na Pemba Imekamilika.
 
uvivu ndio unachangia sana watu kuzaa ovyo hususani mikoa ya pwani uzaliana sana na ndio mikoa inayoongoza kwa uvivu..naomba unijibu ili swali mtu mwenye upungufu wa nguvu za kiume ana uwezo kurutubisha yai?

Yaani kuzaa kwako weye waona Ni uvivu? Nadhani mvivu ni wewe usiyetaka watoto
 
Back
Top Bottom