Bussiness Man
JF-Expert Member
- Mar 9, 2016
- 213
- 244
Nimeamua kuja hapa rasmi kuizungumzia hali ya Kisiwa cha Pemba kimazingira,
Uchumi,Afya,elimu, utamaduni na watu wake.
Nimezaliwa Pemba eneo moja la kaskazini mwa kisiwa hiki chenye urefu wa wastani wa kilomita 95, Ni kisiwa chenye amani iliyorithiwa na sio ya woga.
Watu wake ni wakarimu sana, lakini sio watu wanaopenda kuendeleza elimu kama msingi wa maisha yao. Hususani ni kipindi hicho ambacho tulikua tukisoma sisi sasa hivi ni tofauti kidogo zaidi kwa watoto wa kiume. Kwa upande wa watoto wa kike wazee hawaweki kipaumbele cha elimu.
Pemba imejigawa Miji mikuu 3, mizuri sana yenye huduma zote za jamii inayojitosheleza. Miji hii imejigawa na nikutoka kilomita 18 hadi mji mwingine. kwakua Miji hii imejigawa unaweza ukifika ukasema Pemba hakuna Maendeleo lakin Maendeleo yapo sababu kuu ya kutoyaona maendeleo hayo ni kila Mji na watu wake na Mambo yake . Bahari ya Pemba ni Blue yenye beach nzuri sana, ikiwa ina navisiwa vidogo vidogo ndani yake.
Idadi ya Watu wa Pemba kwenye sensa ya mwaka 2012 ni 406,808 ingawa wengi kipindi kile hawakujiandikisha.
Nimejifunza mengi sana katika maisha yangu ninayoishi pemba, kwakua nakielewa kisiwa hiki utandu na ukoko vizuri sana kuanzia ncha ya kusini mwa kisiwa mpaka kaskazini mwa kisiwa. Nimevutiwa kuweka bayana hapa kuhusu Hali yote ya pemba kwa sababu:
Nimepata changamoto nyingi niliposafiri sehemu tofauti watu wengi wana shauku ya kuijua Pemba na wapemba wakoje, wengi wanawaona wapemba kama hawasomeki au hawaeleweki, wengi wanawaona wapemba wana msimamo si watu wa kuyumba, wachawi ni watu wa kujituma.Wabaguzi hawapendi kujichanganya na wengine.
Nina majibu ya kutosha kuhusu hayo hapo kwa ufupi, ninapenda ukiwa na chochote ambacho umewahi kusikia kuhusu Pemba au kukukutokea niulize, nitajibu majibu yasiyopendelea upande wa kwetu au kujinasibu kwa majibu ya kejeli kwa wengine. nimeishi na watu tofauti nimesoma mazingira na tabia za watu wengi sana.