Niulize swali lolote kuhusu Pemba na Wapemba

Niulize swali lolote kuhusu Pemba na Wapemba

Pemba hiyo biashara haijawahi kuweko na haitotokea kuwepo hata siku moja. Ukija Pemba kama kivazi chako hakiko rasmi ukitembea huwezi kunyanyua uso ukaangalia watu. Na inabidi ubadilike tuu.
Sawa sheikh, mmeshajikosesha watalii wa ndani kwa kubana hiyo biashara.
 
Ingawa sio mpemba, ila swali limenigusa sababu umetaja mikoa ya pwani, tangu uzaliwe ni lini Pemba umesikia wanahitaji msaada eti wamezidi na njaa au shida yeyeto ya kimahitaji, pamoja kuwa na watoto wengi. Unataka kuniambia watu wa bara hawana nguvu ya kuzaa sababu kufanya kazi sana.
Nimefika Unguja na Pemba pia wavivu ni Waunguja ambao ukiona wachapakaz ujue asili Yao bara au ni wapemba waishio Unguja. Swali linafuata ni kwanini hamuwaozi binti zenu kwa watu wa bara? hasa nyinyi wenye asili ya kiarabu?
 
waogopa MAGOVI
Bora watu wa Unguja ni vigumu kuolewa na watu wa bara (mikoa ya ndani) ila Ukiwa mtu wa MRIMA unapewa mke bila kinyongo, ila wapemba hawana taabu, ni kukuamini tu. Kikawaida
Ha haa mkuu umenichekesha Sana.ila vyuoni mpo bright Sana tofauti Na waunguja lakini nasikia mnawabagua Sana wabara wakija kwenu
Ukifika sehem usijifanye matawi ya juu, nenda nao kama wenyewe wanavyotaka mpaka wakukubali. Hata nikenda mikoani husoma tabia za watu wa pale sio kujifanya Mimi natoka dsm kila kitu najua n.k ( ushamba tu huu). Kuwa mnyenyekevu uone kama utadharauliwa na kutwengwa. Maoni yangu
 
Nimefika Unguja na Pemba pia wavivu ni Waunguja ambao ukiona wachapakaz ujue asili Yao bara au ni wapemba waishio Unguja. Swali linafuata ni kwanini hamuwaozi binti zenu kwa watu wa bara? hasa nyinyi wenye asili ya kiarabu?
Hili swali lipo kiujumla sana, sasa wana sifa zao kama hujatimiza huwezi kupewa, siwalaumu ila kuna watu kibao wa bara (mikoani) na wa MRIMA (pwani/mwambao) wameoa na kuolewa huko Unguja /Pemba ....
 
Nimefika Unguja na Pemba pia wavivu ni Waunguja ambao ukiona wachapakaz ujue asili Yao bara au ni wapemba waishio Unguja. Swali linafuata ni kwanini hamuwaozi binti zenu kwa watu wa bara? hasa nyinyi wenye asili ya kiarabu?

watu wabara wengi tabia zao na tamaduni zao zinamashaka sana, lakini pia kumbuka wapo wabara kibao wameoa wapemba masikini kwa matajiri. wao wanachoangalia sana je tamaduni zao (dini hasa) itazingatiwa?? mwanawao atalelewa vyema au ndio kipigo kama punda??? wakiridhika na mambo yako na tabia zako hata ukitaja jahazi zima utapata. kazi kwako
 
Hii tabia ya kusema waswahili ni wavivu tushaizoea, lakini hasikii maeneo ya pwani kuwa na njaa tofauti na huko ndani " wanakofanya kazi kuliko matrekta" sisi tumekinaishwa tokea udogoni, kazi, ibada n.k
Sasa hao " wabara" wa kinguja walipatikana vp ? Mbona unajichanganya ? Pwani sio kama hatukubali " wabara" ila mkija mnataka tubadilike ili tufate mila zenu na khulka zenu, sasa hapo ndo mashaka yanapokuja.
 
Mimi ni muislam zaidi ya wewe,ila uislam haubagui,mbora kwa Mwenyezi Mungu ni yule anayemcha Mungu,sio kwa rangi wala kabila,ila wapemba wao hujifanya ndio wanaojua dini kuliko mtu mwengine yeyote,utadhani sijui Mtume alishushwa Pemba,mm naona hata misikitini hua hawana imani na mtu yeyote asiye Mpemba!
Ni vzr zaidi ukaita jina "ALLAH" au jina lolote lililothibiti ktk dalili yaani ktk Quran na sunna za mtume swala llahu alaihi wasalam epuka tamko mungu kwani miungu ipo mingi sana wengine mpk miti wanaiita mungu na ikiwa umezoe kutamka mungu kwa kummaanisha ALLAH (tabaraka wataala) basi uwe unatamka au kuandika "MWENYEZIMUNGU WA HAKI"
wanazuoni wakiislamu wamekubaliana kuwa inafaa kumwita ALLAH kwa jina ambalo watu wasehemu husika wamelizoe ili wakuelewa unachomaanisha wkt unalingania dini mfano ukiita ALLAH kwa mmasai ambae si muislamu hatakuelewa hivyo unalaruhusiwa kuita hilo tamko kwa lugha husika na ukiongezea neno wa HAQ mfano ulitakiwa kusema Mungu wa Haq na sio mungu!!
natumai hutapaniki
 
Kwa dini ya Kiislamu mtoto huyo ni ruhsa kuoa kwahiyo na wapemba wanaoana kama kawaida.

Karibu sana
Hii inaweza kuwa sababu ya muislam wa ukoo wa mbali kukosa mke? Nalisema hili sababu ninaushuhuda muoaji alikuwa na vigezo muhimu ulivyotaja ila alikuwa ni m bara
 
Mimi nataka kuja pemba holiday, napenda vitu vifuatavyo, history site, chakula cha asili ya watu wa pemba, kuogelea. Je naweza nikakaa wiki hapo bila kupachoka, na hotel nzuri ni kiasi gani kwa siku, please let me know about it
 
Hivi Pemba kuna gereza? na kuna mahakama?
gereza lina wafungwa?

The Boss, Pemba Magereza yapo ila wafungwa ni wachache sana, wafungwa wa Pemba hasa ni wizi wa kuku,ndizi hawa ni wale wenye kundi la wavuta unga.
 
Mimi nataka kuja pemba holiday, napenda vitu vifuatavyo, history site, chakula cha asili ya watu wa pemba, kuogelea. Je naweza nikakaa wiki hapo bila kupachoka, na hotel nzuri ni kiasi gani kwa siku, please let me know about it

karibu sana. Katibu Tarafa, Pemba ina historical site za kuvutia sana, kama mkama ndume, Tumbe site, Kuna Mnarani, na kuhusu kuogelea zipo kama Vumawimbi,vitongoji na Wambaa, huwezi kuchoka kukaa wiki kwakua Pemba ina Miji 3 mikubwa na kila seheme zina hoteli nzuri na vyakula vizuri sana.
 
Je ni kweli kama ninavyo sikia kuwa kuna amani sana, unatembea bila hofu ya kuvamia na kunyanganywa ?
 
Je ni kweli kama ninavyo sikia kuwa kuna amani sana, unatembea bila hofu ya kuvamia na kunyanganywa ?

Ni kweli Hata kama unabeba hela kiasi chochote na zikawa zinaoneka hakuna tatizo, ukisahau pia sehemu unahifadhiwa au zinapelekwa msikitini.

Mimi binafsi ilinitokea kuiona Brifkesi nzima ya dola mpaka juu zilikua ni za wazungu fulani ambao walikua wanamiliki ile Boti ya Sepideh. kiukweli nilibaki kuzilinda tuu baadae wakarudi wenyewe kuzifata.
 
Back
Top Bottom