Mgibeon
JF-Expert Member
- Aug 7, 2011
- 11,141
- 20,787
ukoo wapiii mamaaaaaa!!! Uko wapi mamaeeee!!Bila kuuweka hapa wimbo wa NALIA LIA MAMA... UKO WAPI MAMAA...
uzi utakuwa feki
Afu kuna ile dereva wetu hodari (Ally Mwinyi eenh)
ukoo wapiii mamaaaaaa!!! Uko wapi mamaeeee!!Bila kuuweka hapa wimbo wa NALIA LIA MAMA... UKO WAPI MAMAA...
uzi utakuwa feki
Kumbe ulijuaaaaaa, unamimba yanguuu, ilikuaje tena kuniambia,ukaniambiaa imetokaaaa, mashetani yametoa mimbaa!Ashaaaa niambie ukweli kama hunitaki usinitapeli... ilikua balaaa
kondakta kaja juu akasema haiwezekani kupanda bure imeruhusiwa jeshi la polisi..
mnanda sema tu hawauelewi
Btw Asha imeimbwa na jack simela au
Hiyo stuli kiufundi inaitwa "Taiming",ni moja kati ya vyombo muhimu sana kwenye mziki huo.Jamaa waliendaga ulaya kufanya show, wazungu wanashangaa jamaa wanapanda na visturi na kinanda cha watoto, ila sound ilipoanza wanaona sturi inatumika kama ala! Mizuka ikapanda, jamaa anaimba "We Baba Dulaaaaaaaaaaa" wazungu wanaitikia "Eee Eee'...
Mnanda/mchiriku mtamu sana!
"Njaa haimpendezi MTU kama suti" Mzee nifanyie mpango wa huo wimbo mzeeNyimbo gani mwamba?
Hakuna kigezo rasmi cha kumpata super star namba moja bongo,sababu allmost masuperstar wekubwa wengi kila mtu alitamba zama zake,mfano kuanzia miaka ya mwishoshoni mwa themanini kuja tisini hakuna bendi iliyokuwa maarufu zaidi ya Hisani Gari kubwa kutoka Mwanyamala,baadae kidogo Tumaini Jabali(wasanii hao hao wa Hisani walikua wanachepuka kufyatua albamu ki maslai yao),mbeleni Fadhira nao walivuma wakati mwisho wakaja kukimbiza Jagwa hususani baada ya kuja baba J kutoka Chaukucha Family hiyo ni kwa upande wa Kinondoni(Mwananyama),njoo Temeke,wakati Uraibu wanatamba wengine walikua vidampa,lakini baadae Topaz wakatikisa,kisha Atomic Music na Kombora ikiwa balaa,mbele Kidogo New Kiwembe,Kijumuia na Seven Survivor ikawa patashika nguo kuchanika.nani Superstar wa mchiriku bongo
Uko wapi mama wa Hisani Gari kubwa mdau we nenda You tube,kule kuna mwanangu wa faida Mudy B.Mwanaharakati kaiweka utaiona tu.Humu binafsi nashindwa sababu ina mb nyingi!.ukoo wapiii mamaaaaaa!!! Uko wapi mamaeeee!!
Afu kuna ile dereva wetu hodari (Ally Mwinyi eenh)
wewe kweli ni shabiki wa mchirikuHakuna kigezo rasmi cha kumpata super star namba moja bongo,sababu allmost masuperstar wekubwa wengi kila mtu alitamba zama zake,mfano kuanzia miaka ya mwishoshoni mwa themanini kuja tisini hakuna bendi iliyokuwa maarufu zaidi ya Hisani Gari kubwa kutoka Mwanyamala,baadae kidogo Tumaini Jabali(wasanii hao hao wa Hisani walikua wanachepuka kufyatua albamu ki maslai yao),mbeleni Fadhira nao walivuma wakati mwisho wakaja kukimbiza Jagwa hususani baada ya kuja baba J kutoka Chaukucha Family hiyo ni kwa upande wa Kinondoni(Mwananyama),njoo Temeke,wakati Uraibu wanatamba wengine walikua vidampa,lakini baadae Topaz wakatikisa,kisha Atomic Music na Kombora ikiwa balaa,mbele Kidogo New Kiwembe,Kijumuia na Seven Survivor ikawa patashika nguo kuchanika.
Hivyo kila kitabu na zama zake!!!.
Dah bro, una KINA cha kutosha kwenye huu Mziki!Hakuna kigezo rasmi cha kumpata super star namba moja bongo,sababu allmost masuperstar wekubwa wengi kila mtu alitamba zama zake,mfano kuanzia miaka ya mwishoshoni mwa themanini kuja tisini hakuna bendi iliyokuwa maarufu zaidi ya Hisani Gari kubwa kutoka Mwanyamala,baadae kidogo Tumaini Jabali(wasanii hao hao wa Hisani walikua wanachepuka kufyatua albamu ki maslai yao),mbeleni Fadhira nao walivuma wakati mwisho wakaja kukimbiza Jagwa hususani baada ya kuja baba J kutoka Chaukucha Family hiyo ni kwa upande wa Kinondoni(Mwananyama),njoo Temeke,wakati Uraibu wanatamba wengine walikua vidampa,lakini baadae Topaz wakatikisa,kisha Atomic Music na Kombora ikiwa balaa,mbele Kidogo New Kiwembe,Kijumuia na Seven Survivor ikawa patashika nguo kuchanika.
Hivyo kila kitabu na zama zake!!!.
Ukiangalia Kwa vigezo vingi Juma Mpogo aliwazidi wenzake hasa kwenye utunziUsemacho ni kweli,lakini kwa vile halikuwahi kufanyika pambano la kitaifa la mziki wa mnanda basi itoshe kusema mnanda hauna bingwa!.
Kwanini?,kwanza kwenye mziki wa mnanda kuna kitu kikuu kinaitwa #Tune(mapigo au miondoko),kuna mziki wa Kinondoni,bendi kama Hisan Gari kubwa,Tumaini Jabali,Fadhira,Jagwa,Chaukucha,na hata Wanyamwezi familly,wao wana mapigo yao na mashabiki wao kindakindaki.
Na kuna mziki wa Temeke,bendi kama Seven Survivor,Atomic,Topaz,Kombora,Buti Kubwa,Miami Yankees,Kijumuia New kiwembe na hata Uraibu.Hivyo basi kila mpenzi wa muziki huu ana mapenzi binafsi kutoka kwenye band husika.
Hivyo hatuwezi kuitimisha kwamba fulani alikua bora kuliko mwengine ilihali halikuwahi kufanyika shindano na kila mmoja ana band yake
Atomic advantage je wapo?Topaz (Rasmi Topaz Advantage)band hii ilipotea kitambo sana,kwani baada ya manguli wa bendi hiyo kuanzia Omary Omary ambae alitoka na kwenda kuanzisha bendi yake mpya Atomic Advantage
Long time kitambo Born Town,wapi Surelele,wapi Manila,wapi Boys Brazil,wapi Ajax Mzamba,wapi Manova,Wapi Underdox,Wapi Puma,wapi Jogoo Fresh,wapi Target,wapi TP of Soccer,Kiembe Samaki,wapi ABC,wapi GustaTemeke Mikoroshini mtaa wa Sandali kwa wabishi
Ngoja niutoe kwenye External nitaupandisha hapa."Njaa haimpendezi MTU kama suti" Mzee nifanyie mpango wa huo wimbo mzee
Hata ubunifu na sauti ya kipekee piaUkiangalia Kwa vigezo vingi Juma Mpogo aliwazidi wenzake hasa kwenye utunzi
Ni kweli usemacho lakini kwa mustakabali mzima wa mziki wa mchiriku huwezi kutamka hivyo,ingawa mimi mwenyewe ni mpenzi wa Juma Mpogo na bendi yake ya Seven,na niko njiani kuandaa documentary yao chini ya kiongozi aliebaki #Nasosoro Mwipi(capten Chollo boy)lakini kamwe siwezi kutamka kwamba Mpogo alikua Alpha na Omega!!.Ukiangalia Kwa vigezo vingi Juma Mpogo aliwazidi wenzake hasa kwenye utunzi
Mkama Shapu huyu alikua ni askari polisi aliewahi kufanya kazi mitaa ya Temeke na baadae kituo cha Msimbazi kama sikosei,huyu alikua ni mdau mkubwa wa mziki wa mchiriku kwa wakati huo na bendi ya mwanzo maarufu kuipa saport ni bendi ya Night Star iliyokuwa chini ya Haidari Kesi.Mkama Shapu mdau mkubwa wa mchuliku.. Kile kikundi chake cha Mchiliku kilitwaje?
Hisani ngoma ilikiwa na mwimbaji wake wa kike, Aligongwa na gari asubuhi mitaa ya Faya, Kutokana na ile ajali wakatunga nyimbo uke mwimbo nimeusahau jina.. Unaitwaje? Kama uko nao tuwekee hapa...
Hussein Mwinyi sasa Rais Zanzibar alikuwa mdau mkubwa wa Hisani ngoma (Mchiliku) unakumbuka aliwahi kutungiwa nyimbo? Mbali na ule ya aliyotungiwa Baba yake Mzee Mwinyi kipindi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...
Mkuu huu mziki ni full masela.. Old is Nile..