Niulize chochote kuhusu Wilaya ya Sikonge Tabora

Wilaya ya Sikonge kwa muda mrefu haikuwa na barabara ya kukatisha kuingia na kutoka kwenye mikoa mingine - kifupi Wilaya ilikuwa kama kisiwa hivi. Kwa sasa ndiyo kuna barabara inajengwa toka Tabora mjini kupitia Sikonge hadi Katavi.

Barabara hii sasa ndiyo itahuisha biashara kati ya wilaya ya Sikonge na Katavi hadi Kigoma.

Ardhi ipo ya kumwaga, lakini kilimo chochote kinahitaji Mbolea, Mzunguko wa pesa hakuna - maisha ni magumu mno hasa wa vijana na kina mama.

Chakula kikuu ni Ugali wa Mahindi - Mboga ni Mlenda, Swalu, nsansa, kisanvu ma msusa - Mboga zote hizi zikiungwa kwa tui la karanga!! Uhodari wa wanawake wa Kinyawezi ni ile sifa yao katika mapishi - ni hatari.
mkuu, hizo mboga umenikumbusha home kabisa... Hivi Ntini bado zipo? Wale wadudu ni watamu balaa

TABORA HOME SWEET HOME
 
Kwa sasa hivi miundo mbinu iko vizuri
Ni mkongwe kwa sababu ya uwepo wa Mission ya Moravian lakini ulikuwa isolated kwa kukosa muunganiko na makao makuu.

Miji mingi ilikuwa inakua kwa kusuasua sana wayaback lakini kuanzia 2005 to 2015 kulikuwa na ukuaji wa haraka sana wa urban na peri urban areas.

Sasa Sikonge haina kivutio chochote kwa watu zaidi ya kilimo ambayo haiwezi kuwa ideal place kwa sababu ya ubovu wa miundombinu na huduma za jamii
 
Hata mimi nilioa tabora wanapenda sana ushirikina,kila kitu kinachotokea lazima amuulize mganga jinsi ya kufanya,kiufupi maisha ya wanyamwezi na wazaramo hayatofautiani
Aaah weee usitudanganye..nina mtoto huko tutuo na hao waarabu wenu, sikonge nina jamaa yangu huko kwao mambo aliyonieleza ya huko hapa wala usiwatetee mkuu.
 
Wilaya ya Sikonge kwa muda mrefu haikuwa na barabara ya kukatisha kuingia na kutoka kwenye mikoa mingine - kifupi Wilaya ilikuwa kama kisiwa hivi. Kwa sasa ndiyo kuna barabara inajengwa toka Tabora mjini kupitia Sikonge hadi Katavi.

Barabara hii sasa ndiyo itahuisha biashara kati ya wilaya ya Sikonge na Katavi hadi Kigoma.

Ardhi ipo ya kumwaga, lakini kilimo chochote kinahitaji Mbolea, Mzunguko wa pesa hakuna - maisha ni magumu mno hasa wa vijana na kina mama.

Chakula kikuu ni Ugali wa Mahindi - Mboga ni Mlenda, Swalu, nsansa, kisanvu ma msusa - Mboga zote hizi zikiungwa kwa tui la karanga!! Uhodari wa wanawake wa Kinyawezi ni ile sifa yao katika mapishi - ni hatari.

Kwa hizo mboga zao kuu aisee!
 
Back
Top Bottom