Niulize chochote kuhusu Wilaya ya Sikonge Tabora

Iwensanto

JF-Expert Member
Mar 7, 2019
1,173
1,092
Wilaya ya Sikonge ipo Kusini ya Mkoa wa Tabora, Wilaya hii inapakana na Wilaya ya Uyui Kaskazini na upande wa Mashariki inapatikana na Mkoa wa Singida.

Kusini inapakana na Mkoa wa Mbeya Kusini Magharibi inapatikana na Mkoa wa Katavi na upande wa Magharibi inapatikana na Wilaya ya Urambo.

Wenyeji wa Wilaya hii ni wanyamwezi huku shughuli zao zikiwa ni kilimo ufugaji na uwindaji.

Mazao yao makuu yakiwa ni Mahindi, Maharagwe, Karanga, Mhogo na Mpunga. Huku zao kubwa la biashara likiwa ni Tumbaku.

Wilaya hii inajishughulisha pia katika ufugaji wa nyuki na inasemekana kuwa asali ya Tabora ndiyo asali iliyobora kuliko maeneo mengine yote katika nchi yetu.
 
Back
Top Bottom