Rufiji dam
JF-Expert Member
- Feb 20, 2020
- 3,804
- 8,797
Mara nyingi kumekuwepo na malalamiko kuhusu suala la uwajibikaji katika Jeshi la Polisi. Kumekuwepo pia na visa na mikasa mingi ya uaminifu kati ya raia na Jeshi la Polisi.
Serikali ya Mama Samia ikaja na tume ya Haki Jinai ili kuangali jinsi ya upatikanaji wa haki, jeshi la polisi limeongoza kwa kutiliwa mashaka katika utendaji wake.
Sehemu za Vijini kumekuwepo na uonevu mkubwa. Wilaya Sikonge kuna huyu Askari anaitwa Chuwa, amekuwa na mienendo sio rafiki na amekuwa na tabia ya kubambikia watu kesi ili mradi aweze kupewa chochote, na amekuwa na tabia ya usumbufu sana. Ingelikuwa jambo la maana endapo RPC ama Takukuru mkoa wa Tabora kuja kujionea tabia za huyu Askari sijui kaja kuumiza raia aka kaja kufanyakazi kwa kufuata maadili na miiko ya kazi yake. Kitu ambacho hana maadili ya kazi. Wito kwa RPC huyu Chuwa tunaomba atolewe ama akumbushwe maadili yake ya kazi. Kafikia hatua sio njema maana analeta uchonganishi kati ya Raia na serikali.