Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Dec 24, 2019
9,127
14,497
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia.
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Na me naomba niulize jamani......home theatre yangu ya sony DZ650 inatoa sauti ndogo sana.....itakua imekufa nn??
Mkuu La Pronto, samahani kwa kuchelewa kutimiza ahadi yangu kama nilivyoahidi kukurejea ndani ya Siku tatu, kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu.
Hiyo HT yako ikiwaka inatoa sauti ndogo hata kama utafikisha max volume?
Je, kama ni ndiyo, inakubali kupunguza hiyo sauti ndogo hadi 0dB(silence)?
 
Nina Lg home theater system zile za watt 350. Ina speaker 5 na subwoofer. Shida ni kwamba ports 3 za kuunga speaker kwenye amplifier hazifanyi kazi. Speaker zote ni nzima ila shida kuna baadhi ya ports ukiplug hizi speaker 3 hazilii
 
Nina Lg home theater system zile za watt 350. Ina speaker 5 na subwoofer. Shida ni kwamba ports 3 za kuunga speaker kwenye amplifier hazifanyi kazi. Speaker zote ni nzima ila shida kuna baadhi ya ports ukiplug hizi speaker 3 hazilii
Mkuu BUSH BIN LADEN, japo sijajikita zaidi kwenye matumizi ya Consumer Electronics, bali R & D ya hiyo field upande wa digital technology, uzoefu wangu mdogo
upande wa matumizi ya HT unaniambia kwamba HT yako haina hitilafu ni settings tu.
Japo hiyo HT ni 5.1 capable, imesetiwa kwenye mfumo wa 2.1 ndo maana inapiga Spika mbili na subwoofer. Soma kwa umakini User Manual/guide jinsi ya ku-set between hizo modes tatizo litaisha.
Ukishindwa, weka hapa model number kwa msaada zaidi.
 
Mkuu Prince Mhando, hiyo Subwoofer yako unvyoiwasha inawaka sauti kubwa sana ghafla au inaanza sauti ndogo ndiyo inajipandisha? Je kwenye display inakuwa inaonyesha level ipi ya volume?
inaanzia 23 ivi na haipungui hadi mtu apunguze. inatulazimu ukiwasha uwe karibu nayo ili upunguze. na hata ukiizima na sauti ndogo ukiwaka lazima ianze na sauti kubwa.
 
inaanzia 1-60. hapo haruki namba hata moja hadi iyo 60
Japo sijui algorithm iliyotumika kuandika program ya hiyo subwoofer, tatizo litakuwa contents za EEPROM ambazo zinatumika kama default setting values za subwoofer yako zinakuwa zime-corrupt. Mfano, kama volume ilikuwa inaanzia 10, ikabadilika ikawa 23, ikatunzwa kwenye EEPROM, itaendelea hivyo hivyo hadi ku-copy content za EEPROM ya subwoofer toleo kama hilo na kuzi-program kwenye EEPROM ya subwoofer yako. Au ku-edit contents za hiyo EEPROM ya subwoofer yako.
Mara nyingi hii husababishwa na voltage surges au noise kwenye serial communication bus wakati bus ikiwa busy na EEPROM inapokuwa open kwa ajili ya memory write operation. Hizo strong surges zinaweza Sababishwa na vitu Kama radi etc.

Je, ukiwasha ukaacha kupunguza volume itabakia hapo hapo 23 au inaendelea kupanda? Kama no ndivyo, tatizo litakuwa Rotary Encorder ya subwoofer yako.
 
Japo sijui algorithm iliyotumika kuandika program ya hiyo subwoofer, tatizo litakuwa contents za EEPROM ambazo zinatumika kama default setting values za subwoofer yako zinakuwa zime-corrupt. Mfano, kama volume ilikuwa inaanzia 10, ikabadilika ikawa 23, ikatunzwa kwenye EEPROM, itaendelea hivyo hivyo hadi ku-copy content za EEPROM ya subwoofer toleo kama hilo na kuzi-program kwenye EEPROM ya subwoofer yako. Au ku-edit contents za hiyo EEPROM ya subwoofer yako.
Mara nyingi hii husababishwa na voltage surges au noise kwenye serial communication bus wakati bus ikiwa busy na EEPROM inapokuwa open kwa ajili ya memory write operation. Hizo strong surges zinaweza Sababishwa na vitu Kama radi etc.

Je, ukiwasha ukaacha kupunguza volume itabakia hapo hapo 23 au inaendelea kupanda? Kama no ndivyo, tatizo litakuwa Rotary Encorder ya subwoofer yako.
haijiongezi
 
View attachment 2423546huu mziki naukubari sana kinacho niuzi ni hayo mataa kwenye spika zake zote na. ukiiwasha inaanza na sauti kubwa sana. kingine ukiwasha bluetooth yake inasauti kali sana. ila kwa upande wa bass naona kama ina mziki mzuri kuliko seapiano. yenyewe ni 3.1View attachment 2423546a
kwenye remote kuna button imeandikwa LED hold hiyo then zitazima hizo taa.
 
Back
Top Bottom