Urithi wa Bendi ya Osibisa katika muziki wa Afrika

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,590
2,090
Nikipata nafasi ya kufika Jiji la London kuna vitu lazma nivifanye kwa ukamilifu, mosi nitakwenda kutazama mechi za timu za Tottenham Hotspur pamoja na Arsenal, na baada ya hapo nitafanya kupitapita mitaa kuuliza kuhusu bendi za muziki ambazo zimepata kuwa maarufu kwa kuzunguzma ukuu wa mwafrika, natambua kuwa wapo watakaoniambia kuwa bendi bora ni Assagai, Chris McGregor's Brotherhood of Breath, pamoja na Demon Fuzz. Ila kiukweli natamani nipate kuandika kuhusu bendi ya muziki ya Osibisa, wengine walipata kuiita jina la Osibisi na baadhi wanaifahamu kama Osi Bisa.​

071fda83da3e232ff6eb6bd7f322f1f2.jpg

Mwanzoni mwa miaka ya 1950 huko mitaa ya Ghana kulikuwa na mafundi na magwiji ya muziki, pale unakutana na mtaalamu wa kubembeleza kwa saxophone, Bwana Mkubwa Teddy Osei, pembeni kulikuwa mpiga ngoma maridadi kabsa, Bwana Amarfio, wapuliza filimbi wawili, Mamon Shareef, pamoja na Farhan Freere bila kumsahau na Soloman ambaye sauti yake ilitosha kabsa kuona mahaba katika ala ya muziki.
brotherhood_antibes_1975.jpg

Magwiji hawa walikutana na kuanzisha bendi ya The Star Gazers ila mwaka 1958 waliondoka na kuungana na Kaka wa Teddy Osei ambaye anaitwa Mac Tontoh ambaye huyu alikuwa akipuliza tarumbeta basi wakiwa watu sita wakaanzisha bendi ya Comets ambayo walisumbua sana Afrika ya Magharibi ka wimbo wao wa “(I Feel) Pata Pata”, wimbo ulipata umaarufu mkubwa sana kiasi kwamba ulimfanya Osei kwenda Londo kusomea taalua ya muziki mara baada ya kupata ufadhili wa masomo kutoka serikali ya Ghana mwaka 1962. Lakini mwaka 1964 Osei alianzisha bendi ya Cat's Paw, bendi ambayo ilikuwa ikipiga ala za muziki zikiwa na mchanganyiko wa rock pamoja na soul. Mwaka 1969, Osei aliwaalika maswahiba wake Amarfio pamoja na Tontoh kwenda London na hapo ndipo lilipozaliwa wazo la kuanzishwa kwa bendi ya Osibisa.
unnamed.jpg

Timu ilikuwa na magwiji watatu ambao wao tu ilitosha kuwapa burudani watu ila Osei aliona kuna hoja na msingi sana ya kuongeza wasanii wengi, basi wakamtafuta Richardson, mtaalamu wa kupiga gitaa na muimbaji wenye sauti tamu sana, walimtafuta na kumuingiza Lasisi Amao ambaye ni Mnaijeria, fundi sana katika kupiga saxophone, pia waliwaongeza Wendell, Roger Bedeau, Robert Bailey, Fred Coker pamoja na Mike Odumosu ambao hawa waili waliongezeka mwishoni kabsa.​

image.jpg

Bendi hii ya Osibisa ilifanya ziara nyingi za kimuziki ndani ya miaka ya 1970, walikwenda Tokyo Japani, kisha Sydney Australia, walifika mpaka New Delhi India kisha walirudi na nyumbani Afrika kulipa fadhira kwa Wanaijeria na Ghana. Katika kipindi hiki Bendi ya Osibisa iliwaongeza wasanii kama Paul Golly (mpiga gitaa) pamoja na Daku Adams "Potato" akiwa na menzake Kiki Gyan.

January 1976 wimbo wao wa Sunshine Day ulifika nafasi ya 17 kwenye chart ya Uingereza, na baadaye wimbo wa Dance the Body Music ulifika nambari 31 katika chart hiyo hiyo. Mwaka 1980 Osibisa walipata nafasi ya kutumbuiza kwenye sherehe za sikukuu ya Uhuru wa Zimbabwe, ilikuwa ni nafasi ya kipekee ya kuwaburudisha waafrika katika sherehe yao muhimu.
osibisabandyamahacopy1.jpg
Mabadiliko ya kimuziki yaliwafanya Osibisa waanze kupoteza mvuto taratibu huku kukiwepo na bendi zingine zikifanya vizuri, kitu ambacho kiliharibu zaidi umaarufu wao ni kufanya ziara nyingi za kimuziki pasipo kuwa na nafasi ya kutoa nyimbo zao na kusubiria mauzo. Wasanii wa Osibisa waliona ni vyema wakarejea Ghana na kufungua studio ya muziki pamoja na ukumbi ambao utakuwa ukitumika kwa ajili ya wasanii chipukizi.​

ctc_02_img0433.jpg

Kilichomkuta Defao, Extra Musica pamoja na Madilu System ndo kiliwakuta Osibisa, miaka ya 1990 kulitokea wimbi kubwa la wapiga dili ambao hawa walitumia nyimbo za Osibisa na kuzichoma kwenye CD pamoja na Mikanda ya VHS kisha waliuza kwa bei ndogo tena pasipo kuheshimu hakimiliki wala kutoa mirabaha ya aina yoyote kwa bendi husika ambao walikuwa ndo wamiliki, hali ilikuwa ngumu kiasi kwamba ilifika sehemu Osei, Amarfio pamoja na Tontoh walikimbia na kuiacha bendi ikiwa inapumulia mipira hiyo ni miaka ya 1980.
unnamed1.jpg

Mwisho mwa miaka ya 1990, Osei aliona sio mbaya ajaribu tena bahati zao, akarudisha wenzake huku pia nyimbo zako zikipata mirabaha kwa bendi huku hakimiliki ikizingatia wa ukubwa wake kutokana na umaarufu wa bendi ya Osibisa. Baadhi ya nyimbo zao zilifanyiwa remic na kuongezewa zaidi nyama ili watu waendelee kuburudika huku picha mjongeo za kwenye ziara zao zikiunganishwa katika nyimbo zao.
unnamed11.jpg

Abdul Loughty Lasisi Amao hakudumu sana kwani yeye alifariki maka 1988, wakati Mac Tontoh alifariki 2010, Tarehe 13 Disemba 2022 dunia ikampoteza Sol Amarfio ambaye alifariki akiwa a miaka 84, Juni 2023 tukampoteza Victor Mensah akiwa na miaka 66, na sasa tumebaki na Teddy Osei, Robert Bailey, Wendell Richardson. Ila mpaka sasa mchango wa Osibisa unaonekana kwa kiasi kikubwa kwani ilikuwa ni moja ya bendi za mwanzo kutoka Afrika kufanya ziara zenye mafanikio makubwa zaidi. Binafsi wimbo wa Sunshine Day ndo wimbo wangu maarufu zaidi.​

Everybody do what you're doing

Smile will bring a sunshine day

Everybody do what you're doing

Smile will bring a sunshine day

Sunshine Day!
O ṣeun fun ẹbun iyanu yii
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom