Fanya haya kuifanya sound system yako idumu kwa muda mrefu

kelphin

JF-Expert Member
Dec 24, 2019
9,120
14,490
Habari ya wakati
Natumaini tuko salama

Fanya haya ili subwoofer yako na sound system yako idumu kwa muda mrefu
usichajie simu sehemu ya kuchomeka frash disk

Sababu hi imekua ndio sababu kuu ya kuuwa system ya frash ya watu wengi zaidi Ile haikutengenzwa kwajiri ya kuchajia bali kuchomeka frash peke. Na hi sio kwenye subwoofer pekee bali hata DVD players
usiongeze speaker nyingine zaidi ya zile zilizokuja na system yako

Mara zote redio inapotengenezwa hua inatengenezwa kusukuma speaker za kiwango husika
Unapoongeza za kwako bila ya kua na kipimo maalumu au kiwango cha ukinzani wa coil ya speaker yako (ohms) KUNAUWEZEKANO wa kusababisha uharibifu wa system yako.

Sikukatazi kufanya hivyo ila kwanza elewa kiwango cha ohms kinachotakiwa na system yako kisha elewa kiwango cha ohms cha speaker zako zote kabla ya kuziunganisha na sound system yako
usipende kuweka sauti kubwa sana kwa muda mrefu na mara kwa mara.

Hii inawahusu zaidi wenye subwoofer za mchina.

Hii itakusaidia kuifanya subwoofer yako iishi kwa muda mrefu zaidi.

Hii inawahusu wenzangu na mimi wa birthday na vipaimala.

Kwa faida yako tu ni kuwa.

Unapoongeza sauti kwenye redio yako tafsiri yake ni kua unaruhusu umeme mwingi kutoka kwenye amplify yako na kwenda kwenye speaker.

Hivyo ongezeko la joto hupanda zaidi kwenye baadhi ya components zinazounda circuit za subwoofer yako (components zinazounda circuit ni vitu vote kiujumla vinavyounda ramani, kadi, mashine ya system yako).

Hivyo unapoifungua kwa sauti kubwa kwa muda mrefu zaidi ni kua ile joto inakuwepo humo kwa muda mrefu.

Kumbuka kua subwoofer nyingi kama sio zote hazina mfumo mzuri wa kupooza (feni)

Kwa namna yoyote jitahidi mende, panya wasiingie ndani ya system yako
Sababu mkojo wao huweza kutengeneza short ya components.

Hii ni kwa wale wanaotumia home theater na subwoofer hizi za kisasa

Pia panya hula waya na speaker.

Hivyo unatakiwa kuzilinda kwa namna yoyote utakayoiweza

tumia voltages stabilizer kulinda vifaa vyako vya kielecronic.

Hii sio kwenye sound system pekee.

Bali vifaa vyako vyote vinatakiwa kulindwa na stabilizer.

Stabilizer za kisasa huweza kujizima zenyewe pindi umeme unapokua juu au chini ya kiwango.

Na zipo nyingine zinabalance bila ya kuleta hitilafu ya vifaa vyako

Kwa leo ni hayo tu

For additional
Ili kupata sound safi (bass nzuri) usiweke subwoofer yako juu ya meza au stool au sehemu itakayoitenga mbali na floor

Itakupa good sound ikiwa on floor

IMG_7987.jpg



K’phin.
 
Hii upande wa dc imepigwa naona huto tu dude tumepesuliwa. Naomba aina ya hyo diode na hyo nyingine ni replace
IMG_20220930_181049.jpg
 
Back
Top Bottom