Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Dec 24, 2019
9,197
14,684
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia.
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Mfumo wa kuoperate. Bahati mbaya sikujua anafanyaje lakini utakuta kama ulikuwa ukipunguza sauti inaonesha namba, hiyo inakoma. Huwezi kupata ile menu ya bass, treble n.k

Mkuu mfumo wa operations ni tofauti na amplifier
Yaani namaanisha hivi operation haiwezi kusababusha amplify izingie ndio maana napata tabu kuelezea na kukuelewa
Ila ingekua subwoofer za digital kuzifuma kwa analogy inawezekana kuzibadilishia
Au mfumo wa kuitumia kuset mziki kutoka digital kwenda analog inawezekana
 
Anasuka kwa mfumo wa class AB. ambao unaweza hata kusuka kwa kutumia transistor kutoka kwenye mfumo wa IC kikubwa ni filter ya bass. (Kikubwa subwoofer zote ni dual power) hivyo hakuna kinachoharibika.

Sio zote mkuu
Seapiano hizi za sasa nyingi ni single ila high currents
 
Unaweza kueleza hapa kidogo inakuwaje?
Katika usukaji wa amplifier anasuka kama amplifier ya kawaida, kinachobadilika ni kwamba subwoofer nyingi zinatumia ic TDA sasa yeye anasuka kwa mfumo wa transistor, kwenye input yake anaitengenezea crossover kwa kutumia IC kama TL072/4558 au kwa ajili ya kuchange signal kutoka za kawaida na kuwa bass (60-150hz).
 
Samahani kwa usumbufu, nina suboowfer ya Ailiang 5.1 za (zamani) nilichange mp3(analog) yake to digital . Tatizo: Imekuwa 2.1.Swali: Huu mfumo huwa unachagua signal? Kwa maana signals za tweeter huwezi kuziweka zote?
Ziada: Circuit zake zote mbili (power na audio) zinaweza kupatikana au kuwa modified?
20100430190947-Ailiang-5-1-Home-Theater-System-FM-9200H-USBFM-9200H-.320_320.jpg
 
Subwoofer yangu ilikua nzima inafanya kazi ghafla imezima na haiwaki tena! Nimejaribu kuifungua nimekuta capacitor zimevimba na zimevuja nimereplace nyingine lakini bado haiwaki ina kata fuse! Tatizo linaweza kua ni nini!
 
Samahani kwa usumbufu, nina suboowfer ya Ailiang 5.1 za (zamani) nilichange mp3(analog) yake to digital . Tatizo: Imekuwa 2.1.Swali: Huu mfumo huwa unachagua signal? Kwa maana signals za tweeter huwezi kuziweka zote?
Ziada: Circuit zake zote mbili (power na audio) zinaweza kupatikana au kuwa modified?View attachment 1748024

Bila samahani, kwanza nikupongeze kwa kumiliki dundo kari sana
Litunze utaishi nalo miaka mingi sana
Mkuu hiyo mp3 sidhan kama nmekuelewa vizuri
Nahisi nimekuelewa vibaya naomba unieleweshe hapo
Mp3 uneweka hivi vyakisasa vyenye ki remote?
Kama nlicho ki post hapo juu au la?
Kuhusu circuit hiyo redio ndani inatumia linear power supply ambayo ina transfom pembeni kwahyo power circuit ipo hpo hapo na ya amplify ipo hapo hapo hazijatenganishwa
Ku modify yani kama ukitaka kuifanyaje mkuu?
 
Subwoofer yangu ilikua nzima inafanya kazi ghafla imezima na haiwaki tena! Nimejaribu kuifungua nimekuta capacitor zimevimba na zimevuja nimereplace nyingine lakini bado haiwaki ina kata fuse! Tatizo linaweza kua ni nini!

Pole sana mkuu ni subwoofer ya aina gani mkuu
Naomba npigie picha mbele na nyuma
Kisha nikupe majibu
 
Bila samahani, kwanza nikupongeze kwa kumiliki dundo kari sana
Litunze utaishi nalo miaka mingi sana
Mkuu hiyo mp3 sidhan kama nmekuelewa vizuri

Nahisi nimekuelewa vibaya naomba unieleweshe hapo
Mp3 uneweka hivi vyakisasa vyenye ki remote?
Kama nlicho ki post hapo juu au la?
Kuhusu circuit hiyo redio ndani inatumia linear power supply ambayo ina transfom pembeni kwahyo power circuit ipo hpo hapo na ya amplify ipo hapo hapo hazijatenganishwa
Ku modify yani kama ukitaka kuifanyaje mkuu?
Kuhusu mp3: Mp3 yake ni ya zamani (analog) kwa maana haina Bluetooth. Niliweka mpya za kisasa zenye mfumo huo. Baada ya hapo mfumo ukawa 2.1.
Kuhusu circuit : Nataka kujua kama zinaweza kupatikana kama zikiharibika.
Kuhusu modificaton: Kama hazipatikani hakuna uwezekano wa kuzirekebisha?
 
Fuse ipo nyuma ya transfomaView attachment 1748457

Nimeshakuelewa mkuu
Je ukichomoa hizo waya za blue zinazienda kwenye circuit bado fuse inakata? Jibu nadhan hapana
Hi inamaana kua hizo njia mbele zina short yaan zinakutana
Sasa chakufanya niambie inatumia ic gan ya power
2030 au 7379 ili tuone inakuaje
Lakini pia kuna 7805 inakuwepo hapo nyuma kwajiri yakuwasha hiyo radio uko mbele
Je ipo?
 
Back
Top Bottom