Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
10,515
Reaction score
17,439
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Nenda pale ubungo stand kwa mgaya kariibu mic hotel kachegue toleo linalokufaa,sikio lako ndio litaamua uchukue toleo lipi
Kuna hizi skywood soundbar wanadai Zina hit deep (bass) ni kweli mkuu umefanikiwa kuzisikiliza au ni promo tu

Wanazinadi kwambaZina mziki mzito mno
 
Signal inaenda kwa pt moja kwa moja au
Ni ngumu kupitisha signal moja kwa moja kwenye PT2313 kwa kuwa hakutakuwa na I2C commands za kuendesha hiyo PT2313 kutoka kwenye MCU, ambazo zitafanya signal za sauti ziwe selected kwenye source channel, pia ku-set attenuators za output channels, treble, gain etc.

Hivyo PT2313 haitafanya kazi. Inabidi signal za sauti ziende kwenye Sallen-Key filters za Sub na Hi, ziwe voltage pre-amplified kwenye opamp, baadae current-buffered kwenye opamp,ndipo ziende kwenye power amplifier ya class D(TPA3116D2 kwa Low frequencies, na TPA3118,TPA3128 kwa High frequencies) etc.
 
Hichi kitu hakuna, impedance haibadiliki hizo Ni myth kubadilika ujue coil ishaenda na maji
Kwa mtazamo wa juu juu usio wa kitaalamu zaidi, uko sahihi. Ila kwa mtazamo wa kitaalamu zaidi, mkuu nerilan yuko sahihi. Speaker impedance inabadilika kulingana na input frequencies zinazoingia kwenye driver(speaker), kinatokea kitu kinaitwa coil inductive reactance. Ambacho hakibadiliki ni speaker voice coil resistance, japo pia huathiriwa na joto. Hiyo voice coil resistance na voice coil inductive reactance kwa pamoja ndizo zinatengeneza hiyo impedance unayodai haibadiliki.
 
Hivi hawa pia si ndo watengenezaji wa seapiano
Kodtec(Konzo Digital Technology) ni kampuni ya Mtanzania aitwaye Japhet Patrick Konzo, ambayo bidhaa zake hutengenezwa China, under Kodtec-branded ODM business model.

Nashindwa kujua kampuni ya Kodtec inakwama wapi, maana subwoofer zake zinakubalika sana sokoni. Labda kulingana na ubora wake costs of production iko juu sana kiasi kwamba hapati faida?
 
Mkuu knachokufa kwny hz sub za kisasa na haktengenezeki na ndcho knacho control kila ktu kwny sub ikiwemo hiyo display kpo kdude cheusi hv cha pembe 4 skumbuki vema jna lake hcho ndcho kmelaza ma sub mengi ya ksasa kwa mafundi hakna repair kbs so usjaribu danganya watu hp ni display
Uko sahihi mkuu. Hiyo inayokufa inaitwa microcontroller, ambayo inahusika na settings za muziki na display operation kwa pamoja. Mafundi wengi huita display tu.

Kwa sasa zile zinazotumia PT2313 zinatengenezeka.
 
Habari wakuu.

Kama kuna mtu ana bookshelves speakers nzuri na anauza naomba anitumie model na pictures please. Ikiwezekana na bei pia.
 
Kodtec(Konzo Digital Technology) ni kampuni ya Mtanzania aitwaye Japhet Patrick Konzo, ambayo bidhaa zake hutengenezwa China, under Kodtec-branded ODM business model.

Nashindwa kujua kampuni ya Kodtec inakwama wapi, maana subwoofer zake zinakubalika sana sokoni. Labda kulingana na ubora wake costs of production iko juu sana kiasi kwamba hapati faida?
Huyo jamaa ni Mkinga aliyeoa mchina, jamaa kwenye home music kama subwoofer anakwama kwenye usambazaji na bei, hata kwenye professiona audio kama mixer,booster, speaker,mic amejaribu lakini soko haliendi vizuri,vijana wanauza bithaa zake wanataja bei za kiuwenda wazimu
 
Habari wakuu.

Kama kuna mtu ana bookshelves speakers nzuri na anauza naomba anitumie model na pictures please. Ikiwezekana na bei pia.
+255 748 040 464 mcheki huyo yuko ilala au search kule inst na fb anatumia jina used kama mpya, ila bei zake zimechangamka sana
 
Huyo jamaa ni Mkinga aliyeoa mchina, jamaa kwenye home music kama subwoofer anakwama kwenye usambazaji na bei, hata kwenye professiona audio kama mixer,booster, speaker,mic amejaribu lakini soko haliendi vizuri,vijana wanauza bithaa zake wanataja bei za kiuwenda wazimu
Mkuu, unashauri nini afanye ili kuweka mambo sawa, biashara yake isonge mbele?
Maana hali kama hii inavunja moyo kwa mtu mwenye wazo la kuwekeza katika soko la teknolojia nchini mwetu.
 
Mkuu, unashauri nini afanye ili kuweka mambo sawa, biashara yake isonge mbele?
Maana hali kama hii inavunja moyo kwa mtu mwenye wazo la kuwekeza katika soko la teknolojia nchini mwetu.
Kosa la kwanza alilolifanya ni kupitoea sokoni kwa muda mrefu kisha kurudi tena kodteck na seapiano ni subwoofer za mwanzoni kabisa, ukiachana na wengine kama wale akina mingo,X5,,sayona. Kosa la pili baada ya kurudi sokoni bithaa zake akauza mwenywe zaidi kkupitia maduka yake aliyofungua mikoani kote, vijana wake wakawa wanauza kwa kuwatajia wateja bei ya juu, mfaano mic ya codteck dukan kwake vijana walikuwa wanaweza kukutajia bei ef80,ila ukienda duka la kawaida mic yao hiyo hiyo unauziwa bei ya elf60 mpaka 55, tatu kutokufanya distribution ya kutosha kwa agents au watu wa kati kama vile akina aborder, yeye alikunbatia mali wakati wenzao wanatoa mzigo hata kwa mali kauli kwa superdealers. Tatu kufanya biashara huku yeye makazi yakiwa china.wenzie wanafanya wakiwa hukuhuku
Kwa sasa naona kahamia zaidi kwenye home ampliences japo pia hafanyi vizuri
 
Back
Top Bottom