Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Kichuguu nina ist ya wife ukiwasha AC baada ya muda mrefu na kwenye speed ndogo mfano foleni huwa gari inajizima, ukiiwasha inawaka kawaida tuu. Tatizo ili kama hujawasha AC huwa halitokei na hata kama ukiwasha ukiwa kwenye speed huwezi ona ili tatizo
 
Nilishawahi kujibu swali kama hilo hapa
 
Vipi oil namba 50 kwa gari ndogo (Rav4 kilitime)
 
Mkuu habari na hongera kwa kazi nzuri.

Nina shida na engine ya IZZ. Muungurumo wake umekuwa juu na pia kunakuwa na mlio wa kkkkkkk.

Fuel consuption imeongezeka tofauti na kawaida. Nimebadili plug lakini shida haijaisha bado.

Pia kunakuwa na vibration sana.
Ni mambo gani natakiwa kufanya na tatizo linaweza kuwa ni nini?
 

Inawezekana tatizo lako ni dogo sana; je umeshabadili air filter au air cleaner? Baada ya hapo ndipo yanapofuata matatizo mengine madogomdogo pia kama vile air flow sensor kuwa chafu au baadhi ya injector kuwa zimeanza kuziba. Kuna mafuta ya kuzibulia injector, na vile vile kusaifishia air flow sensor, lakini tatizo lako kubwa linaweza kuwa ni air filter tu.
 
Mpwaa HONGERA sanaa sana aise
 
Soma kwanza kitabu cha gari yako, kuna injini nyingi zinataka 5W-30 na 5W-20. Hata hivyo kwa Dar es Salaam ambayo ni sehemu yenye joto sana, unaweza kutumia 10W-30 au 10W-20.
Na pia, matumizi ya oil yanategemea sana matumizi ya gari lenyewe. Maana low viscocity oils zinataka kubadilishwa baada ya kilometa chache zaidi ya high viscocity oils. Kwa hivyo ni chaguo la mtumiaji zaidi ingawa watengeneza magari wenyewe wana mapendekezo yao.
 


Ninakushukru sana mkuu kwa maelekezo mrua.
Nilishabadili air cleaner tu.
Kuna fundi nilimshirikisha akanambia huenda ikawa ni fuel pump, nozzle, mounting na oxygen sensor.

Na gari ina km 200.000 kwa sasa, unashauri nibadilishe kitu gani ili liendelee kubaki kwenye hali yake?

Pia naomba kujua ni mafuta gani ya kuzibulia injector na wapi naweza yapata? Na kuna wakati ac inachelewa kufanya kazi hasa ninapokuwa nimepaki kwenye jua kwa muda mrefu.

Ngoja nifanyie kazi ushauri ulonipa kisha nilete mrejesho.
 
Hongera!

Ingiwa nimechelewa kusoma thread mapema.

Nitarudi nikikwama na hawa watu wetu wa mitaani!

 
Hii air cleaner uliyoweka ni original? Swali linaanzia hapo? Maana watumiaji wa magari wengi hawapendi vitu original na ambavyo vitasaidia kumaliza tatizo la gari badala yake wanaweka vitu kwa kupenda urahisi
 
Nishawahi kukatazwa na dealer wa Toyota kutumia injector cleaner,yeye alisema once ukianza basi inatakiwa utumie kila unapojaza mafuta hasa kwa kuwa filling station nyingi kwa bongo zinauza mafuta machafu (ambapo sikumuelewa kwa kweli)
1. Je, kuna ukweli katika hilo?
2. Nikiweka mafuta kwenye vituo vya kawaida gari haina mis,lakini nikiweka kwenye vituo vya TOTAL then nikarudi kwa vingine mis hutokea na sometimes gari kuzima na kusumbua kuwaka,Je,ni formula ya mafuta kutofautiana au kuna sensor kwenye gari haipo sawa?.
Shukrani.
 
NOAH 1AZ ya mwaka 2002, 280,000 km naenda nayo karibu mikoa yote kwa kazi zangu,je recommendations oil ni ipi kati ya 5W-30 na 20W-50?
 
Nina ist naendesha nikiwa na mizunguko mingi. Inatokea inashiwa nguvu na kuzima. ukiwasha Tena inapiga mwendo Kama kawaida. Limetokea mara ya tatu leo. Mara ya kwanza mwezi wa 8 na mara mbili mwezi huu. Tatizo yaweza kuwa Nini?
 
Hii air cleaner uliyoweka ni original? Swali linaanzia hapo? Maana watumiaji wa magari wengi hawapendi vitu original na ambavyo vitasaidia kumaliza tatizo la gari badala yake wanaweka vitu kwa kupenda urahisi
ni Original mkuu
 
gari yangu nikiendesha kwa muda taa ya check engine inawaka nikitoa terminal na kurudishia gari inawaka na taa inazima. ni tatizo gani?
 
Mkuu Kichuguu naomba msaada wa User Manual ya Mitsubish Outlander 2006.
 
Niambie kuhusiana na engine ya Premio 7A 1760 CC
 
Nieleze namna unavyoifahamu Toyota Volts! Ni changamoto gani ilizonazo? Je ni gari imara?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…