Niulize Chochote Kuhusu Injini za Magari Madogo na Pickup za Petroli

Kichuguu

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Messages
8,391
Points
2,000
Kichuguu

Kichuguu

Platinum Member
Joined Oct 11, 2006
8,391 2,000
Mkuu hizi SAE ndo zimejaa dukani
Nadhani jukwaa hili litakusaidia kuelewa namna ya kuchagua SAE number ya gari lako. Usikimbile SAE40 labda kama gari lako ni kuukuu. iwapo hujafikisha km 180,000 tafuta SAE20 na ukielemewa basi chukua SAE30 lakini usiweke SAE40 au zaidi.
 
Boeing 747

Boeing 747

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2018
Messages
1,464
Points
2,000
Boeing 747

Boeing 747

JF-Expert Member
Joined Mar 30, 2018
1,464 2,000
Mkuu Kichuguu na mimi leo nina jambo geni kidogo nimeliona linanitokea kwenye gari....

Gari linaendesheka Vizuri kama kawaida ila nikiwasha AC gari linapungua nguvu sana....nikizima tu AC, hapo hapo unasikia gari linakuwa lepesi sana na linachanganya faster...
Ni ishu mpya kabisa kuwahi kunitokea...
Shida yaweza kuwa ni nini..?
Gari Nissan Note 2005, HR15 Engine, CVT gear box....
 
Kichuguu

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Messages
8,391
Points
2,000
Kichuguu

Kichuguu

Platinum Member
Joined Oct 11, 2006
8,391 2,000
Mkuu Kichuguu na mimi leo nina jambo geni kidogo nimeliona linanitokea kwenye gari....

Gari linaendesheka Vizuri kama kawaida ila nikiwasha AC gari linapungua nguvu sana....nikizima tu AC, hapo hapo unasikia gari linakuwa lepesi sana na linachanganya faster...
Ni ishu mpya kabisa kuwahi kunitokea...
Shida yaweza kuwa ni nini..?
Gari Nissan Note 2005, HR15 Engine, CVT gear box....
Pole sana ndugu yangu; kadhia uliyopata inaweza kutokanana na moja ya sababu tano kuu au zote kwa pamoja kama ifuatavyo, yaani sababu moja ikisababisha nyingine.
(a) Bearing za AC Compressor kuwa zimekufa kwa hiyo inazuia injini kuzunguka freely
(b) Solenoid ya AC clutch kuwa imeaungua. Mara kwa mara AC Clutch solenoid ikifa, huunguza pia fuse kwa hiyo unakosa kabisa AC, ila kama fuse iliyokuwamo ni ya amperage kubwa zaidi ya kawaida basi utapata kadhia hiyo kwani AC inakuwa inachukua umeme wote wa gari, na kuacha sehemu nyingine za injini hazina umeme wa kutosha
(c) Alternator inakaribia kuishiwa nguvu, ukiwasha AC basi umeme wote unasihia huko na kuacha sehemu nyingine za injini hazina umeme wa kutosha.
(d) Pressure switch kwenye Compressor imekufa, kwa hiyo kunaweza kuwa na pressure kubwa sana kwenye compressor kiasi cha injini kushindwa kuizungusha.
(e) Piston moja au zaidi ndani ya Compressor zimekwama, kwa hiyo compressor haiwezi kzunguka

Ili kutest sababu (b) na (c) washa AC wakati taa zinawaka uone kama zitazimika; kutest sababu (d) gusa AC compressor kama ni ya moto sana; kutest sababu (a) na (e) inabidi kuifungua AC kukagua sehemu ndani ya compressor yenyewe.
 
laii

laii

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2016
Messages
402
Points
500
laii

laii

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2016
402 500
Jina langu siyo Kitunguu aisee, hebu badilisha; mimi ni Kichuguu, ".....huwezi kulinganisha Kichuguu na mlima Kilimanjaro"

Bila shaka gari yako huwa inatoa moshi mwingi sana, yaani kuna oil inavuja na kuingia kwenye combustion chamber na kuunguzwa pamoja na mafuta. Iwapo injini yako ina nguvu kama kawaida, basi kuna vipete fulani ambamo valve stem hupita (vinaitwa valve guides) huenda vimepanuka sana na kuacha mwanya wa oil kupenya ndani ya injini. Fundi wako akifungua cylinder head cover anaweza kuvikagua na kuona kama vimepanuka. Ni rahisi kuvibadilisha kwani viko kwenye cylinder head, ila utahitaji cylinder head gasket mpya.

Kama Injini haina nguvu kama zamani na vile vile inakula mafuta mengi sana basi huenda piston rings zako zimekwisha; hapo utahitaji kazi kubwa kidogo ya karibu na overhaul kwani itabidi ufungue injini yote kuweka piston rings mpya. Usifanye makosa ukabadilisha piston kwani unaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi. Kazi ya namna hiyo fundi anaweza kuifanya kikamilifu bila kuangusha injini kabisa; utahitaji cylinder head gasket mpya pia.

Piston rings hufa iwapo hubadilishi air filter yako mapema kwani huruhusu vumbi (ambalo ni silica na ni ngumu kama msasa) kuingia ndani ya cylinder na kusaga hizo piston rings na vile vile iwapo hubadilishi engine oil katika muda unaotakiwa.
Valve guides ndo valve seal mkuu
 
laii

laii

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2016
Messages
402
Points
500
laii

laii

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2016
402 500
Samahani mkuu STP unaweka kwenye tank la petrol au ni unapoweka engine oil mkuu
Injini kuzimika wakati wa idling kunasababishwa na sababu nyingi sana ndogo ndogo ambazo hazina madhara kabisa kwenye injini yako. Ngoja nitaje ambazo ni za kawaida sana.
(1) Inawezekana air filter yako imeshajaa uchafu; iangalie na ukiweza uibadilishe.
(2) Inawezekan air flow sensor imeshachafuka au imekufa. Air flow sensor ni kiwaya chembamba sana kinachoweza kukatika hasa iwapo air filter ni chafu. Kama imechafuka, kuna mafuta ya kuisafishia, na kama imekufa unaweza kubadilisha na kuweka nyingine. Zinagharimu kati ya dola mbili hadi kumi na tano tu.
(3) Inawezekana injector zako zina uchafu, kwa hiyo hazipitishi mafuta wakati pressure ni ndogo. Kama tatizo ni hili, kuna injector cleaners ambazo unaweza kuongeza kichupa kimoja kwe tanki la mafuta likiwa full tank kukusafishia injector hizo.
(4) Inawezekana throttle position sensors kwa upande wa chini haifanyi kazi, kwa hiyo ukiachia accelerator basi computer inakuwa haipati taarifa za position ya accelerator yako kwa hiyo inashindwa kujua ni kiasi gani cha mafuta kinahitajiwa na hivyo inaamua kukata mafuta kabisa. TPS zinazuwa kati ya dola tatu hadi 15 tu.
(5) Inawezekan fuel pressure regulator imeshachoka kwa hiyo inavujisha mafuta kurudi kwenye tank wakati pressure ni ndogo na kuiacha injini na ukame wa mafuta. Hii ikitokea, gari inaaza kupungukiwa na spidi hata ikiwa katika mwendo wa barabarani wa kawaida, kwa hiyo iwapo ukiwa barabarani hunaoni tatizo lolote basi ni wazi hili siyo tatizo ulilo nalo.

Sababu namba (2) hadi namba (4) zikitokea, ni lazima zitaregister kwenye computer ya gari na utapata checki engine light. Kama inakuonesha check engine light, ipeleke kwenye computer scan ujue ni sensor gani. Kama hakuna check engine light, basi kwa asilimia kubwa ni kwa air filter yako imechoka sana.
 
Kichuguu

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Messages
8,391
Points
2,000
Kichuguu

Kichuguu

Platinum Member
Joined Oct 11, 2006
8,391 2,000
Samahani mkuu STP unaweka kwenye tank la petrol au ni unapoweka engine oil mkuu
Weka kwenye tanki la mafuta; chupa moja ya STP kwa full tank ya petroli; inasafisha hizo injectors kwa kwa kama wiki nzima hivi kulingana na unedeshaji wako.
 
Kichuguu

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Messages
8,391
Points
2,000
Kichuguu

Kichuguu

Platinum Member
Joined Oct 11, 2006
8,391 2,000
Carina yangu inachafua engine, nikiiosha leo engine baada ya3-4wks,nakuta engine imechafuka na oil imekua nyeusi, fundi akanishauri nibadilishe valve seal
Hizo valve seals zikiharibika, basi oil inakuwa inaingia ndani ya coimbustion chamber na kuchomwa, utakuwa unapata moshi mweupe hivi kwenye exahust. Ila sasa kama injini inachafuka kwa oil, basi itakuwa ni cylinder head cover gasket ndiyo mbovu. siyo hizo valve guides (kwa jina jingine valve seals). Test mojawapo rahisi sana ya kuona kama oil inaingia kwenye combustion chamber ni hivi. Washa gari, halafu weka chukua kipande cha pamba au toilet paper, weka pale kwenye exhaust kama dakika kumi hivi. Kikishika masizi meusi utakayoweza kuona kirahisi kwa macho yako katika muda huo mfupi, basi ni dalili kubwa kuwa valve guides zimepanuka. Daima kutakuwa na masizi kidogo sana lakini siyo mengi ya kuona mpaka yanatia weusi.

Fundi wako pia anaweza kutoa spark plugs na kuzikagua; ukikuta zina unyevunyevu basi ni dalili moja kukubwa kuwa valve guide seals ziko hoi.

Ngoja nikutafutie picha kukuonyesha tofauti zake. Sijui kama picha hii umeielewa, inaonyesha valve zikiwa zimefunguliwa. Sasa hizo rings number 3 ndizo zenyewe. Picha ya kulia ni valve zenyewe zikiwa zimefungwa kwenye clinder head

1567652868600-png.1198362
1567653076207-png.1198363

Picha ya Clynder head gasket ni hii hapa

1567653378311-png.1198368Oil kuwa nyeusi inategemea sana aina ya oili unayotumia; kuna oils zinazobadilika rangi kuwa nyeusi mapema sana baada ya kupita kwenye injini hata kabla hazijachoka.
 
Kamwene kamwene

Kamwene kamwene

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2019
Messages
767
Points
1,000
Kamwene kamwene

Kamwene kamwene

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2019
767 1,000
Ni kweli kamba matumizi ya AC yanaongeza ulaji wa mafuta kwenye gari...??

Kuna mafundi wanasema ukiwasha gari alafu ukienda kuangalia kwenye exhaust ukikuta inatoa maji basi ujue engine ya gari ni nzima sana(kinanda) mpyaaaaa ??

Naomba kujua kazi ya ABS kwenye gari ?
Tyre za gari inatakiwa ubadirishe kwa muda gani,na zinafungwaje mana nimewai kuskia fundi anasema gari haikimbii sana hizo tyre zimegeuzwa kashata sijui
 
Kichuguu

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Messages
8,391
Points
2,000
Kichuguu

Kichuguu

Platinum Member
Joined Oct 11, 2006
8,391 2,000
Ni kweli kamba matumizi ya AC yanaongeza ulaji wa mafuta kwenye gari...??
Ndiyo; AC inaendeshwa na injini na inahitaji nguvu sana, ndiyo maana ukiwasha AC lazima muunguruma wa gari ubadilike kidogo kwa vile inaaza kunywa mafuta mengi
Kuna mafundi wanasema ukiwasha gari alafu ukienda kuangalia kwenye exhaust ukikuta inatoa maji basi ujue engine ya gari ni nzima sana(kinanda) mpyaaaaa ??
Siyo kweli. Mafuta yakiungua ndani ya injini hutoa Carbon Dioxide na maji katika hali ya mvuke. Wakati gari linawashwa asubuhi lingali la baridi, mvuke huo uifika kwenye exahust huganda na kuwa maji ambayo ndiyo yanayodondoka kutoka kwenye Exhaust. Hiyo itatokea kwa injini yoyote iwe ina matatizo au haina matatzio mradi tu imewaka. Exhaust ikishakuwa ya moto, basi mvuke ule hauwezi kuganda tena na hivyo huwezi kuona maji yakitoka. Ila sasa iwapo gari linatoa maji kwenye exhaust muda wote hata pale ambapo exhaust imeshakuwa ya moto basi ujue kuwa injini ina matatizo makubwa. Ama cylinder head gasket imekufa au engine block ina ufa, kwa hiyo maji ya radiator yanapita moja kwa moja hadi kwenye exahust, na unaweza kuanza kuona kuwa injini inakausha maji mara kwa mara.
Naomba kujua kazi ya ABS kwenye gari ?
Inazuia gari isteleze ukikamata breki ya ghafla. kwenye barabara yenye utelezi ABS huwa inastabilize gari barabarani lakini unaweza kugonja kitu kilicho mbele yako kwa vile gali litaendelea bila kukwaruza barabara mpaka itakaposimama yenyewe. Ukiwa na ABS jiachunge uwe unaendesha kwa makini, breki za ghafla hazifanyi kazi
Tyre za gari inatakiwa ubadirishe kwa muda gani,na zinafungwaje mana nimewai kuskia fundi anasema gari haikimbii sana hizo tyre zimegeuzwa kashata sijui
Fuata maelekzo ya mtengezaji (manufacturer)
 
quake

quake

Member
Joined
Sep 11, 2012
Messages
54
Points
125
quake

quake

Member
Joined Sep 11, 2012
54 125
5w30 ni 56000 pale total mcity boss tena og from france.. hio 80000 itakua castrol ndio wana bei za ajabu za oil nahisi sababu ni brand kubwa wamejitangaza sana..
Kuna mwana specs za gari zinataka 5w-30 yeye akang'ang'ania hio SAE40 kisa ni bei rahisi(kuna sehemu lita 4 wanauza Tsh.28,000) wkt 5w-30 lita 4 nanunua Tsh.80,000,aisee gari yake hua inaunguruma kama tractor/matatizo kwny gari yake ni kila mara imebidi juzi hapa aweke engine nyingine.
 
Kamwene kamwene

Kamwene kamwene

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2019
Messages
767
Points
1,000
Kamwene kamwene

Kamwene kamwene

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2019
767 1,000
Huu uzi umenipa msononeko kidogo sina gari wala pikipiki,lakini nimejifunza mambo makubwa anyway..
Kuna gari ni automatic transmission ila navyoiendesha sasa kama manual transmission..
Iko hivi
Uki start engine inawaka vizuri ukiweka gear D au L au R inazima sasa nikitaka isizime nashika break.
Navyotaka kuondoka nakanyaga pedal ya mafuta na break kwa wakati mmoja alafu naachia break taratibu gari ndio inakubali kuondoka,nikitembea kidogo inaanza kusinzia nakanyaga break tena hapa inasimama kabisa nakanyaga mafuta mengi huku nimeshika break naachia break taratibu gari inaondoka..
Sijawai kuiendesha kwenye foleni mana ningekua na case ya kugonga gari za watu..
Kuna fundi pump ya kuvuta mafuta ipo mbele kwenye engine imekufa,manake hii gari ina pump kwenye tank na myingine ipo mbele kwenye engine
Mwingine akasema computer inatatizo inashindwa kichambua nini sijui
Mwingine akasema tuliweka mafuta machafu,
Engine ya gari ni D4 inatoa moshi kuna muda ukikanyaga mafuta sana wakati umesimama unakuta nyuma kwenye exhaust imemwaga kama unga mweusi hivi chini
 
Gari yoyote ya Automatic ukiwasha lazima uwe umebonyeza brake ama sivyo haliwezi kuwaka. Brake ile pia hufanya kazi kama clutch, kutenganisha injini na gearbox.
 
mng'ato

mng'ato

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2014
Messages
16,682
Points
2,000
mng'ato

mng'ato

JF-Expert Member
Joined Oct 27, 2014
16,682 2,000
Thnxs mkuu,natumia castrol na niko huku mkoani so kidogo gharama zinakua juu kidogo lkn juna sehemu 5w-30 ya total nimeona wanauza Tsh 60,000 ila sijawahi kuitumia mkuu.
5w30 ni 56000 pale total mcity boss tena og from france.. hio 80000 itakua castrol ndio wana bei za ajabu za oil nahisi sababu ni brand kubwa wamejitangaza sana..
 
Boeing 747

Boeing 747

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2018
Messages
1,464
Points
2,000
Boeing 747

Boeing 747

JF-Expert Member
Joined Mar 30, 2018
1,464 2,000
Kweli mkuu...hata huku Arusha total 5w 30 tunauziwa kuanzia 55000/-...
Castrol inahitaji umakini...zina soko sana...hivyo feki zipo...
5w30 ni 56000 pale total mcity boss tena og from france.. hio 80000 itakua castrol ndio wana bei za ajabu za oil nahisi sababu ni brand kubwa wamejitangaza sana..
 
Boeing 747

Boeing 747

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2018
Messages
1,464
Points
2,000
Boeing 747

Boeing 747

JF-Expert Member
Joined Mar 30, 2018
1,464 2,000
Wakiuza 60000/- hiyo total siyo mbaya inategemea unaishi wapi coz maeneo mengi inaanzia 55000/
Mimi naitumia na ninaona mashine ya gari inafanya kaxi vizuri....injini inakuwa nyepesi vizuri
Thnxs mkuu,natumia castrol na niko huku mkoani so kidogo gharama zinakua juu kidogo lkn juna sehemu 5w-30 ya total nimeona wanauza Tsh 60,000 ila sijawahi kuitumia mkuu.
 
Kamwene kamwene

Kamwene kamwene

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2019
Messages
767
Points
1,000
Kamwene kamwene

Kamwene kamwene

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2019
767 1,000
Gari yoyote ya Automatic ukiwasha lazima uwe umebonyeza brake ama sivyo haliwezi kuwaka. Brake ile pia hufanya kazi kama clutch, kutenganisha injini na gearbox.
Ni kweli mkuu sasà yenyewe inatetemeka kiasi kwamba ikitaka kuzima ili isizime inatakiwa ushike break hadi chini kabisa
 
Emmanuel S Jonathan

Emmanuel S Jonathan

Verified Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
168
Points
225
Emmanuel S Jonathan

Emmanuel S Jonathan

Verified Member
Joined Jul 11, 2015
168 225
Wakiuza 60000/- hiyo total siyo mbaya inategemea unaishi wapi coz maeneo mengi inaanzia 55000/
Mimi naitumia na ninaona mashine ya gari inafanya kaxi vizuri....injini inakuwa nyepesi vizuri
mkuu nipo arusha pia napata wapi castrol og au total nataka kwa ajili ya engine ya vtec sport car nadhan 5w30 ndo itafaa kama wadau walivosema apo juu
 
Forum statistics

Threads 1,336,578
Members 512,670
Posts 32,544,087
Top